Na Mwandishi Wetu
Lazima
tukubali tukatae, kilichomtokea Zitto jana, kufukuzwa CHADEMA, it is a shock
kwa wengi, ila wale makini wachache na yeye mwenyewe akiwemo, walijua fika kuwa
kuna siku hii siku ingefika!.
Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge la Tanzania, ya Kamati ya Mashirika ya Umma (PAC) Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Zuberi Kabwe |
Tangu Zitto Zuberi
Kabwe (ZZK) alipotangaza wazi nia yake ya kugombea urais wa 2015 kupitia
Chadema, nimenote humu jf, watu wanatetemeke, kuweweseka na hata kutishika eti
ZZK ni mamluki na kitendo cha kuitangaza nia hiyo, kuna lengo la kukisambaratisha
Chadema!.
Maudhui ya
mada hii ni kuwachambau makundi 10 yanayomsupport au kumpinga ZZK na uamuzi
wake huu. Naomba nikiri, kichocheo kilichonifanya kuanzisha uzi huu ni mada ya
Mchambuzi ...
Kwa kuanzia,
naomba kwanza ku declare my interest!. Namsupport ZZK kuonyesha nia na sio
kutangaza rasmi nia hiyo!.
Tofauti ya
kuonyesha nia mapema na kutangaza rasmi nia mapema ni hizi zifuatazo!.
Kuonyesha nia:
Kubehave ki "presidential hopeful" ili kujenga nia "will"
utakayoitumia kama "power" ili kukipata unachokitaka. (Where there is
a will, there is a way!"). Faida ya kuonyesha nia mapema ni kukipa chama
na sisi wananchi fursa ya kukupima ili muda muafaka ukifika, Chama ndicho
kikushauri kijana chukua fomu gombea, unaonekana unatufaa.
Kutangaza rasmi
nia: Ni kitendo cha kujitangaza rasmi nia kuwa mtu utagombea urais wa Tanzania
mwaka 2015. Kwa utaratibu wa sasa, mtu huwezi kutangaza utagombea urais, ten a
ukatangaza wazi mchana kweupe kwenye kadamnasi ya watu!,
kwa sababu,
wagombea ni wa vyama!. ZZK hakupaswa kutangaza wazi ki vile, this was a
mistake, mimi ZZK ni rafiki yangu, na pia nimeshamwambia maoni yangu kwenye
hili. Kwa jinsi alivyotangaza is as if alishafikia uamuzi hivyo kutishia kuwa
Chadema isipomsimamisha yeye, patachimbika!. Hili nimelieza wazi katika mada
yangu ya Urais wa ZZK 2015: Ngoma Ikivuma Sana....
Baada ya kutoa
utangulizi huo, sasa naomba nije kwenye hoja yangu haya makundi 10 ya watu
wanao muunga mkono ZZK na wanaompinga ZZK wako wenye busara, wako waoga, wako
wadini, wako wa wakabila, wako wa ukanda, wako wanafiki, wako waumini,
wakowafuasi, wako washabiki, wako wakweli.
Waoga; Hili ni
kundi la kwanza na ndilo kundi kubwa, hawa wanampinga ZZK kwa uoga tuu usio na
sababu zozote za msingi. Hawa ni wale waliozoea mazoea, hivyo hiogopa
mabadiliko yoyote yawe positive au negative, kwao ni uoga tuu!. Kwa vile ZZK ni
mwana Chadema, na mwana chama yoyote anayo haki ya kugombea nafasi yoyote ya
uongozi ndani ya chama na ndani ya nchi.
ZZK ameitumia
haki hiyo kuelezea nia yake bila kuvunja sheria, tararibu wala kanununi yoyote
ya chama. Natoa mwito kwenu nyie enyi waoga, open up be ready for changes for
the better!. Ukombozi wa nchi hii utaletwa na wele tuu wenye kukubali
mabadiliko na sio ving'ang'anizi!.
Wadini;Kama
ilivyo kwa Tanzania, nchi kama nchi haina dini, ila watu wake wa na dini zao!.
Wadini ni wale ambao, wanajiona dini zao ni bora zaidi ya dini za wengine,
hivyo yoyof refence hivyo huweza kuteau mtu yoyote kutoka positio yoyote na
kumgeuza kuwa ni mtu wa top office bila reference yoyote.
Wale wanaotaza
ma kwa jicho la udini, wakijuiliza kwa nini fulani kapewa nafasi fulani kwa
sifa zipi na vigezo vipi, wakifikosa na kuja kuangalia dini ya mhusika, basi
watamlebo JK ni mdini, hata kama bte asiye dini yao, wao wanamuona huyo sio!.
JK ni
Muislamu, appointment powers zake hazina any terms baadhi ya wateule hawa
wanaso sifa na wangestahili nafasi his regardless wao ni dini gani!
Ndio maana kwa
baadhi ya teuzi za JK tukubali tukatae anatea as he pleases lakini kwa wengine,
dini ni kigezo!. Chadema nacho kama chama hakina dini, ila wanachama, wafuasi
wake na washabiki wake wote wana dini zao. Kwa hao wadini wa Chadema
kwao,nafasi za juu kabisa za uongozi wa Chadema, lazima zishikwe na watu wa
dini fulani!, ZZK alipogombea uenyekiti kiliwaka na mwenyewe akanywea!
Uchaguzi
unakuja tena na this time tutamchagiza Prof. Safari kugombea Uenyekiti,
nashauri subirini muone kitakachotokea!. `Vivyo hizo wako wanaompinga ZZK kwa
dini yake, hawa watampinga Mkandara, Watampinga Arfi na Watampinga Prof. Safari
kugombea top position yoyote kwa sababu tuu ya dini zao.
Hawa wapo,
tukubali tukatae!. Dawa yao hawa sio kuwabadilisha, bali kuyalazimisha
mabadiliko, ili hayo mabadiliko ndiyo yawabadilishe na huo udini wao uwawashe
kama koti la chawa na kujikuta wanalazimika kulivua!
Wakabila; Hili
nalo ni kama lile la udini, Tanzania kama nchi, haina kabila, ila wananchi wake
makabila yao, viongozi nao wana makabila yao. Ukabila ni ile hali ya kuona mtu
wa kabila lako ndio bora zaidi.
Enzi za
Nyerere, kwa vile alitoka Musoma, watu wa Musoma, wakajikuta wana upper hand
Ikulu na kwenye Majeshi ndio maana tuliwashuhudia kina Musuguri, Mwita Marwa,
Waitara etc, huku kule Ikulu kina Apiyo etc. Waziri fulani akiwa wizara fulani,
inatokea wengi wa wakuu wa taasisi za wizara hiyo ni kabila lake!.
Hata JK baada
ya kuingia ikulu, wako watu fulani wa kabila lake, ndugu au jamaa zake,
wamefika hapo walipo kwa kubebwa tuu!, tena angalau wengine baada ya kubebwa,
"ukibebwa bebeka" wamebebeka na ku perform!. Wako waliobebwa, lakini
hawabebeki, they are non performers kabisa, lakini wanaendelea kuwepo tuu na
sana sana ni kuhamishwa tuu huku wakiendelea ama kuto perform, au kuborongo ila
wapo!. Chadema nacho kama chama, hakina kabila, ila wanachama na viongozi wake
wana makabila yao!. Hakuna asiyejua kuwa kuna viongozi wenu wakuu wamefikaje
hapo walipo!.
Hakuna
asiyejua kuna mtu yuko bungeni na bintiye na mkwewe kwa sababu tuu ya kabila na
nasaba!. Sasa kuna wanaompinga ZZK kwa sababu tuu ya kabila lake!. Wangwe
alipotamka kugombea uenyekiti, kilichofuatia sote tunakijua!
Chadema ni
chama cha kitaifa, kiko over and above ukabila, hivyo tutahakikisha nafasi za
juu za uomgozi, zinashikwa na wenye sifa regardless ni wa makabila gani, ndio
maana nitamchagiza tena ZZK agombeaa sio tuu urais, bali aanzie Uenyekiti wa
Chadema ambao unautangulia urais na hauna kizingiti cha umri!
Na kuna
ukabila mbaya kabisa usiotamkwa wazi, lakini umo mioyoni mwa wenye
ukabila,"eti watu wa makabila fulani fulani, kamwe hawawezi kushika urais
wa nchi hii!". Tutaukomesha!
Ukanda; Huu ni
kama ulivyo udini, na ukabila, Tanzania kama nchi, haina kanda fulani ambazo ni
preferencial, maeneo yote ni sawa mbele ya taifa!. Ila lazima tukubali,
tukatae, kuna maeneo fulani, watu wake wameneemeka zaidi kuliko maeneo
mengine!.
Sasa kuna
baadhi ya watu wa maeneo haya yaliyoneemeka, hujiona wao ni bora zaidi kuloko
watu wa maeneo mengine, hivyo kufikia stage ya kujiona wao wanastahili
preferential treatment kwenye kila kitu, hali inayopelekea wale watu wa maeneo
ambayo hayajaneemeka sana, kujiona wako sidelined au marginalized!.
Ili
kujionyesha na wao wapo, ndio hivi sasa wanajitutumua!. Hakuna ubishi Kaskazini
kuna neema kuliko kwingine kote!. Chadema nayo ime gain stronger momentum
maeneo kuliko maeneo mengine ambayo its gaining now!
Hili
limewapelekea baadhi ya manazi kujidhania nafasi fulani za uongozi its their
rightful kutokana na kanda yao!, ndio maana utasikia safari hii rais lazima
atoke kanda fulani!. Kwa vile ZZK hatoka Kaskazini, kuna wanaompinga kwa hilo
tuu na hawa wakanda, hata akiibuka Prof. Mwesiga Baregu au Prof. Safari ambao
wanazo sifa zote kugombea uenyekiti au urais, nao watapingwa tuu!
Ili kuiondoa
hii dhana potofu ya ukanda, tunataka kushuhudia nafasi za juu zikishikwa na
watu wenye sifa, regarless wanatoka kanda gani sambamba na haki za kugombea, na
hata ikitokea top positions zote zikashikwa na watu wa kabila moja kanda moja,
lakini watakuwa wamezipata kwa merits za sifa na uwezo, na sio kwa ukanda na
ukabila wao!
Wanafiki; Hawa
ni watu wanaujua uwezo wa kiukweli wa ZZK kma rais na amiri jeshi mkuu, lakini
kwa sababu, wamezoe kujikomba komba kwa watu wao, wanajifanya kumpinga tuu ili
wasionekane watovu wa nidhamu!
Vivyo hivyo
kwa wanamsupport ZZK, kuna wale wanaomsupport na kumchagiza ili kuona Chadema
inasambaratika. Wengi wa hawa hawana nia ya dhati ya mageuzi, bali wanataka ZZK
apunguze kitisho cha lanss;ide victory ya Chadema come 2015 (if it will
change!).
Washabiki;
Miongoni mwa wanaomsupport ZZK, wako wanaomsupport au kumpinga kwa ushabiki
tuu, kama walivyo mashabiki wa simba na yanga. Hata ZZK aboronge vipi, wao kama
mashabiki, watamchagiza tuu na kumshagilia mpaka mwisho.
Na kwa wasio
mashabiki, hata afanye mema vipi hawa watambeza tuu. Uzuri wa ushabiki ni
mapenzi tuu na sometimes hauna sababu zozote za msingi za kupenda au kuchukia!.
Mfano kuna wanaoipenda yanga kwa sababu fulani na kuna wanaipenda yanga kwa
bila sababu yoyote!.
Kuna mashabiki
wa Yanga ambao wao hawaimaind Simba lakini kuna mashabiki wa yanga wanaichukia
Simba bila sababu yoyote!.
Mfano mimi
siipendi kabisa rangi yoyote ya kijani na manjano!, kitu chochote chenye kijani
na manjano kinanichefua, hivyo kujikuta naichukia Yanga kwa sababu tuu ya rangi
hizo, kama yanga wangebadili rangi na kuwa blue na nyeupe, nisinge ichukia
Yanga!. Vivyo hivyo ZZK ana washabiki wake na wengine wana mashabiki wao
wengine, hivyo kuna wanaimpinga ZZK kwa ushabiki tuu lakini hawana hoja zozote
valid ni kwa nini ZZK or why not ZZK!.
Waumini;
Waumini ni stage ya juu zaidi ya washabiki, hawa wana muaminia na kumkubali.
Kuna watu wanamuaminia ZZK na kumkubali hivyo kumuunga mkono!.
Katika
kumuaminia na kumkubali, pia kuna watu wana waaminia na kuwakubali wengine wote
wenye uwezo wa urais. Miongoni mwa waumini hawa, wale ambao wanawaaminia
wengine ambao sio ZZK, watampinga ZZK kwa uwezo wao wote na hiyo upinzani wao
ni justified kwa wanachokiamimni.
Wafuasi; Hawa
ni zaidi ya washabiki na waumini, hawa ni followers wa ZZK ambao watamfuata
popote atakapokuwepo ndipo nao watakuwepo. Followers mwanzo walikuwa washabiki,
waka graduate na kuwa waamini, waka pata masters kwa kumfuata na kujiunga
Chadema.
Kwao hawa ZZK
ndio everything!. Sambamba na hao, pia figures nyingine za Chadema, nao wanao
wale wanaowafuatilia, hawa ambao sio wafuasi wa ZZK, hawa kwa vyovyote vile,
watampinga ZZK au mwingine yoyote atakayejitokeza.
Huu ufuasi
ukivuka mipaka unageuka kuabudu!. Wako wafuasi wanao waabudu wale viongozi wao
na kuwaona kama miungu!. Sasa ikitokea mtu akajitokeza kuwapinga hawa miungu
watu ndani ya Chadema, mtu huyo atachukiwa na kubatizwa kila aina ya jina
"katumwa", "msaliti", "pandikizi" etc, etc!.
Baada ya uchaguzi wa 2010, kuna watu waliaminishwa mgombea wa Chadema
alishinda, NEC wakauchakachua ushindi ule na kumtangaza mgombea wa CCM!.
Sasa wengi wa
hawa mashabiki, waumini na wafuasi, wanaamini na waabudu, tayari wanaye mgombea
wao kwa 2015 na sio ZZK!, kitendo cha ZZK kutangaza nia, kimawatetemesha,
wanatishika na kuweweseka humu jukwaani kila kukicha!. Mimi nilibahatika
kuzungumza off-the record na mgombea fulani hivyo naujua msimamo wake, ndio
maana nikawashauri.
Wenye Busara:
Hawa ni wale ambao wanazo akili za kiutu uzima, hawa wanaelewa ushindi wowote,
hupatikana kwa team work na sio individual ambitions za kuitwa rais!. Hawa
wanapiga mwenendo wa ZZK kutangaza kugombea kwa sababu baadhi ya matamshi na
maamuzi ya ZZK, yanaongozwa na feelings, emotions na ego, sio kwa critical
thinking na tafakuri makini, hivyo huwa ni maamuzi ya papara na yasiyo na tija
yoyote kwa mustakabali wa Chadema.
Hawa
wanampinga ZZK bila chuki, wanaamini ni ujana na utoto, akikua atatulia. Wengi
katika kundi hili ni ma great thinkers, ZZK kama ana masikio, atakuwa
amewasikia!.
Wakweli;Hili
ndilo kundi la mwisho na lina watu wachache. Hawa ni wale ambao wanampinga ZZK
kwa sababu za ukweli au wanamsupport ZZK kwa sababu za ukweli. Ukweli daima
huwa ni mchungu, ukweli huwa unauma, ukiwa mkweli daima utachukiwa na sometimes
you may pay the price!.
Sometimes
ukiwe mkweli mno, hili ni kosa kwa siasa zetu zilizogubikwa unafiki, majungu,
fitna na mambo kibao ya kiajabu ajabu!. Kosa kubwa la ZZK ni kuwa mkweli
daima!.
Mimi pia niko
kwenye kundi hili, nafahamu kwa sasa ZZK ndie mtaji mkubwa zaidi Chadema kuliko
mtu mwingine yoyote!. Nahisi hata ushindi wa wale vijana wa Kigoma, he has a
hand!. Yako mambo mengi huwa ninayaandika humu, huwa naishia kupingwa!. Sifa
kuu ya ukweli siku zote husimama!.
Kwa vile
Chadema wamejipanga kushinda 2015, ziko hoja ambazo ni za ukweli na lazima
Chadema wasimame nazo ikiwemo ya kutompuuza ZZK hata kidogo na kuendelea
kumwacha akipayuka payuka, he needs to be contained more kuliko hivi alivyo let
loose!. Chadema ndiyo inayomuhitaji zaidi ZZK kuliko ZZK anavyoihitaji
Chadema!.
2015 inakuja,
kuna vyama vinajipanga kuchukua nchi huku vingine vinajipanga kutetea viti
vyao. Katika kutimiza azma hiyo, viko vyama vinajipanga kimipango mkakati huku
vikieleza vitafanya nini, na kuna vyama vinaendeleza mahubiri, kucheza makida
makida na kuchezea shilingi chooni!.
Siku ya siku
ikifika, hatutaki watu waje kutulilia tena humu as if hawakuambiwa!. ZZK
ametangaza tuu nia, msitetemeke, msiweweseke wala msitishike, just do the right
thing and and in doing that right thing, make sure you do it
Makala ni kwa
msaada wa Jamii Forums
Mwisho.
Post a Comment