BENKI YA TAIFA YA BIASHARA (NBC) imezindua huduma mpya ya NBC BENKI NILIPO ambapo mteja anaweza kupata huduma zote za kibenki kupitia simu yake ya mkononi, kompyuta mpakato kama kulipia bili na huduma zingine popote pale alipo.
 
Meneja Masoko wa Benki ya NBC, Maria Alina Kimaryo (katikati), Mkuu wa Kitengo cha Njia Mbadala cha benki hiyo, Raymond Mutagahywa (kushoto) na Mshauri wa Bidhaa wa benki hiyo, Canicius Joseph wakizindua huduma mpya  ya NBC Benki Nilipo jijini Dar es Salaam leo. Wateja wa benki hiyo sasa wanaweza kupata huduma za kibenki kwa kutumia program maalum ya NBC katika ‘play store’ hivyo kupata huduma za kibenki kupitia laptop zao, tablets na simu za mkononi za smartphones.
Akizungumza kwenye uzinduzi rasmi wa huduma hizo jana jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Masoko wa Benki hiyo, Maria Alina Kimaryo alisema kwamba huduma hizo mpya ni rahisi kutumia na kurahisisha shughuli za mteja kwa kupitia simu yake ya mkononi na kompyuta mpakato kwa njia ya intaneti kwa kutoa na kulipa bili zake za luku, dawasco, dstv na huduma zingine.

“Watu wengi wanaangalia ni njia gani rahisi ya kuangalia akaunti zao kwa masaa 24 kwa siku kwa kutizama salio kulipa bili kupitia simu zao za mkononi ili kuweza kuokoa muda na ndipo benki ya NBC ilipoamua kuja na huduma hizi za kipekee nchini ya BENKI NILIPO ili kurahisisha shughuli za biashara na za kijamii nchini,” aliongeza

Aliongeza kwamba huduma hizo mpya zimetengenezwa kwa ajili ya kwenda na wakati wa mazingira ya sasa ya jamii yenye sayansi na  teknolojia ambapo mteja anaweza kufanya shughuli zote za kibenki bila kulazimika kwenda benki au kuwa na akaunti na benki ya NBC,

Kimaryo alisema kwamba ndani ya huduma hiyo mteja anaweza kupata taarifa za akaunti yake, kuhamisha fedha kwenda kwenye akaunti yake mwenyewe na akaunti nyingine za NBC kwa watu wengine na kuendesha akaunti yake akiwa ndani au nje ya nchi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Njia Mbadala za Kibenki, Raymond Mutagahywa alifafanua kwamba benki hiyo itaendelea kutoa huduma bora na bunifu kwa ajili ya wateja wao huku wakienda sambamba na maendeleo ya sayansi na teknolojia kwa kuboresha huduma za kibenki nchini.

Alisema kwamba uzinduzi wa huduma hiyo mpya nchini ni kiashiria tosha kwamba benki hiyo imejipanga kuendelea kutoa huduma na bidhaa bora kabisa za kibenki hapa nchini na kuwarahisishia watanzania kwenye huduma za kibenki nchini.

Mutagahywa aliongeza kwamba kupitia huduma hiyo ya kipekee nchini wateja wa benki hiyo wanaweza kutuma fedha kwa wapendwa wao ambao pia watakuwa hawana akaunti na benki hiyo na wateja wa NBC wanaweza pia kuweka fedha kwenye ATMs mahali popote.



Mshauri wa Bidhaa wa Benki ya NBC, Canisius Joseph (kulia), akionyesha jinsi huduma mpya ya NBC Benki Nilipo inavyofanya kazi wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma hiyo jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwake ni Meneja Masoko wa NBC, Maria Alina Kimaryo, Mkuu wa Kitengo cha Njia Mbadala cha benki hiyo, Raymond Mutagahywa na Meneja Mahusiano wa NBC, William Kallaghe.

Meneja wa ATM na Kadi wa Benki ya NBC, Wambura John (katikati) akimwonyesha mmoja wa mteja, Nusra John (kulia) jinsi anavyoweza kutoa pesa katika ATM ya benki hiyo bila ya kuwa na kadi kwa kutumia huduma ya NBC Cash Popote katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya NBC Benki Nilipo jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Meneja Huduma za Jamii wa benki hiyo, Irene Peter.


Mkuu wa Kitengo cha Njia Mbadala cha benki hiyo, Raymond Mutagahywa  (Kkushoto), akizungumza wakati  wa uzinduzi wa huduma mpya ya  NBC Benki Nilipo jijini Dar es Salaam leo. Kushoto kwake ni Meneja Masoko wa NBC, Maria Alina Kimaryo na Mshauri wa Bidhaa wa benki hiyo, Canisius Joseph.


Meneja Mahusino wa Benki ya NBC, William Kallaghe (kushoto) akiweka mambo sawa katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam leo.

Add caption

Baadhi ya maofisa wa benki hiyo waliohudhuria uzinduzi wa huduma mpya ya NBC Benki Nilipo jijini ar es Salaam le
























Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.