Inspekta Jenerali wa Polisi IGP Ernest Mangu
amefanya mabadiliko kwa baadhi ya
makamanda wa polisi wa mikoa.
Miongoni mwa makamanda wa mikoa waliofanyiwa
mabadiliko ni pamoja na aliyekuwa kamanda wa Mkoa wa Simiyu, Naibu Kamishna wa
Polisi (DCP) Charles Mkumbo anakwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza na
nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa afisa mnadhimu mkoa wa Manyara Kamishna
Msaidizi wa Polisi (ACP) Gemini Mushi.
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna wa Polisi (DCP)
Valentino Mlowola anakwenda kuwa Kaimu Kamishna wa Intelijensia makao makuu.
Aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala
Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Maria Nzuki amehamishwa makao makuu kuwa
mkuu wa polisi jamii na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa kamanda wa kikosi
cha ufundi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Lucas Mkondya.
Wengine ni aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa
Kilimanjaro Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Godfrey Kamwela
amehamishiwa Polisi Makao Makuu na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Njombe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fulgence
Ngonjani.
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ulrich Matei amehamishiwa Kanda Maalum ya Dar es
Salaam kuwa mkuu wa utawala na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Kigoma Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jafary Mohamed.
Aidha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi
(SACP) Ferdinand Mtui aliyekuwa mkuu wa operesheni maalum polisi makao makuu
ameenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma.
Zaidi ya hao wengine waliyohamishwa ni pamoja na
aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Polisi (SACP) Frasser Kashai amehamishiwa Polisi makao makuu na nafasi yake
kuchukuliwa na aliyekuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Iringa Kamishna Msaidizi wa
Polisi (ACP) Zuberi Mwombeji.
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke
Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Kihenya Kihenya amehamishiwa polisi makao
makuu na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa mkuu wa polisi wa wilaya ya kati
Ilala, Dar es Salaam Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Andrew Satta.
Kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya
Jeshi la Polisi, mabadiliko hayo ni ya kawaida katika kuhakikisha kwamba
usalama wa raia na mali zao unaendelea kuimarika.
Imetolewa na:
Advera Bulimba-SSP
Msemaji wa
Jeshi la Polisi.
Post a Comment