...hasa kwa wale wanaonunua magari kwa mara ya kwanza, na hawana uzoefu wa kuendesha gari, na pia wale wote ambao wanaweza wakawa wana uzoefu wa kuendesha gari mijini, lakini hawana uzoefu wa kuendesha gari kwenye barabara kuu za kwenda mikoani.

Lakini ni vema kila mtu aliye dereva akasoma ninachoeleza hapa, inaweza kuokoa maisha yako ya familia yako, na wengine wanaoendesha magari au kuwa abiria.

Ndugu zangu, ukiweza kuendasha gari hapa Dar, au hata mikoani mijini, haina maana utaweza kuendesha gari pasipo tatizo kwenye barabara kuu. Nimeshuhudia watu wengi sana waliokufa kwa sababu baada ya kununua gari walikuwa na mchecheto wa ku-drive kwenda kwao kijijini.

Kuendesha gari kwenye barabara kuu ni tofauti sana na kuendesha gari mijini. Kwenye barabara kuu challenge zake ni kubwa sana kwa sababu gari zinaenda kwa kasi, na pia kuna mambo mengi ya ghafla yanayoweza kujitokeza ambayo kama huna uamuzi wa haraka kama dereva utakufa tu kabla ya kufika mwisho wa safari yako. Ukifanya kosa hata dogo barabara kuu unaweza kufa, tofauti na mijini.

Kwa mfano, ku-overtake katika barabara kuu ni jambo linatakiwa lifanywe kwa makini sana. Na pia kila unapoingia kona kali au blind spot kwenye barabara kuu weka akilini kwamba unaweza kukutana na kitu upande wako, basi linaloenda kasi, lori au trekta liloharibika, mifugo, shimo kubwa, mawe yaliyoporomoka, ajali nk. Pia unaweza kukutana ghafla na dereva mzembe anae-overtake kwenye kona na yuko upande wako.

Usithubutu ku-overtake sehemu ambayo huoni mbali mbele, na usikaribie sana gari unayotaka ku-overtake kabla ya kui-overtake. Na unapo-overtake kama una gari manual gear, rudi gia za chini kwanza ili kujenga spidi ya ku-overtake. Kama una gari automatiki, ikibidi itoe gari kwenye overdrive (unabonyeza kiswitch cha Overdrive na kuna kataa katawaka kwenye dashboard kuonyesha Overdrive iko off), hasa kama ulilkuwa umepunguza mwendo. Mara nyingine toa gia kwenye "D" na rudi kwenye "2" ili kujenga spidi ya ku-overtake, na ukishamaliza rudi kwenye D na Overdrive. Hili ni muhimu sana kwa gari za ambazo ukikanyaga accerator gari inakawia kuchanganya. Overtake kwa haraka, sehemu ambayo iko salama, na ni vizuri gari unayoi-overtake dereva wake ajue unamu-overtake. Unaweza kumpigia honi kidogo ya kuibia kama kuomba - usipige kwa nguvu ukamuudhi. Epuka kuovertake sehemu ya barabara yenye mashimo, maana dereva wa mbele anaweza kurudi upande wako ili akwepe shimo wakati tayari unamu-overtake.

Siri moja ya ku-overtake salama ni uvumilivu - overtake nzuri haitaki haraka.

Na pia kosa linaloua watu wengi sana ni ku-overtake kwa kukisia kwamba hakutakuwa na gari inayokuja upande wa pili zile sehemu ambazo huoni vizuri mbele. Hata kama barabara haina magari mengi usithubutu kukisia kwamba hakutakuwa na gari (gambling overtake).

Na pia katika barabara kuu kuna suala la uchovu - fatigue. Hili ni jambo jingine linaua sana watu wasio na uzoefu wa kuwa katika barabara kuu. Ni mbaya hata zaidi ikiwa utakaposimama mahali kwa chakula ukanywa bia - hata moja tu, kwa sababu itakuletea sana usingizi. Epuka kula vyakula vizito kama ugali na maharage, au kula hadi ukashiba sana! Ukisikia usingizi simama upumpzike, toka ndani ya gari, tembea kidogo, kabla ya kuendelea na safari. Kama ikibidi tumia Redbull (sio zaidi ya mbili).

Na jambo jingine muhimu sana la kukumbuka ni kwamba ukiingia barabara kuu, ukaendesha kwa muda fulani, akili yako inazoea spidi kali kiasi kwamba huoni tena kama unaenda spidi kali. Unaweza ukawa unaenda 140km/h ukaona kama unaenda 80km/hr. Hili huwa mara nyingi linasababisha kuacha njia na kupinduka, au kuingia kona ukiwa na spidi kubwa na gari kupinduka. Nadhani umesikia sana ajali zinazosemwa zilitokea kwa sababu dereva alishindwa kumiliki gari - ni kwa sababu akilini dereva aliona haendi spidi.

Na pia jambo jingine muhimu sana kukumbuka ni kwamba, unapoenda safari yoyote ya mbali ambayo utaendesha gari mfululizo kwa zaidi ya masaa manne, au kwa spidi zaidi ya 100km/hr, hakikisha tairi zako hazina umri zaidi ya miaka mitano, la sivyo utapata basti hata kama tairi inaonekana bado mpya kwa

kuitazama. Tairi ikizidi miaka mitano haifai kusafiria safari ya mbali, japo unaweza ukaendelea kuitumia kwa safari za mijini.

Nimeona niseme haya kwa sababu nawapenda ndugu zangu. Sitaki mufe barabarani, au mniue mie na familia yangu. Wapeni taarifa wengine ili tuzidi kuepuka vifo hivi vya barabarani ambavyo vingi vinazuilika.

Neno langu la mwisho, ili uendeleee kuwa salama barabarani ni kwa lugha ya kiingereza; BE PATIENT kwa lolote unalotaka kufanya ukiwa unaendesha gari. Zingaitia hilo, utakuwa salama.

  • Makangale Satellite  imenukuu ujumbe huu kama ulivyo kutoka www.wavuti.com
Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.