Nchini Afrika Kusini kumetokea ghasia na purukushani dhidi ya raia wa kigeni ambapo huvamiwa na kuendeshewa kipigo hadi kufariki. Makundi ya raia huvamia maduka ya wageni na kupora mali ziliomo.
Baadhi ya wazawa hutuhumu wageni kuwa wanapora ajira zao, kufanya uhalifu na kuyapa gharama mashirika ya kiutu nchini mwao.

Ghasia hizo zilisababisha mamia ya raia wakigeni kuondoka.
Hivi majuzi, raia 390 wa Malawi walioponea chupuchupu mashambulizi hayo walipokelewa kwa vilio walipowasili mjini Blantyre. Mabasi 6 ya abiria yanaarifiwa kuwasili mjini humo na raia 390, miongoni mwao wakiwa wanaume na wanawake wa kati ya umri wa miaka 18 – 30 na wazazi wenye watoto wachanga.

Waziri wa Mawasiliano wa Malawi Kondwani Nankhumwa alisema, ‘Tumefurahia kuona raia wetu wako salama. Raia wengine zaidi watawasili nchini siku baadaye.’ Waziri huyo alijumuika na ndugu na jamaa wa karibu wa raia hao ili kuwapokea katika uwanja wa kitaifa wa Blantyre.

Baada ya kuwasili salama salmini nchini Malawi, raia waliokuwa na majeraha walifikishwa katika hospitali ya Queen Elizabeth Central (QECH).

Nako nchini Nigeria, Baraza la seneti nchini humo limomba mfalme wa Kizulu afikishwe katika mahakama ya jinai ya Kimataifa (ICC) iliyopo The Hague, Uholanzi kutokana na mashambulizi yalionendeshwa dhidi ya raia wa kigeni waliopo nchini Afrika kusini na kusababisha vifo vya watu saba.

Mfalme wa Kizulu, Goodwill Zwelithini amekana kuwa kauli yake ndiyo sababu ya raia wa kigeni kushambuliwa hadi kuuawa nchini humo wiki mbili zilizopita.
Kabila la Wazulu ni kabila kubwa nchini Afrika kusini ambapo linakadiriwa kuwa na idadi ya watu milioni 11 na huwa wakitekeleza na kuheshimu maombi hutoka kwa Mfalme wao.
David Mark, msemaji wa Seneti nchini Nigeria alifahamisha kuwa unyama wanaoendeshewa raia wakigeni nchini Afrika Kusini ni jambo lisilokubalika hata kidogo na kuomba mfalme Goodwill afikishwe mahakamani.

Msemaji huyo alifahamisha kuwa haiwezekani kamwe kwa kiongozi kusimama katika hadhara nakusema kuwa raia wa kigeni wanapaswa kuondoka, matamshi haya yamechochea chuki na ni jambo lisilokubalika. Alisema Afrika Kusini inapaswa kuwafunza raia wake historia na kukumbuka msaada wa Nigeria kwa Afrika kusini katika kipindi cha ubaguzi wa rangi "apartheid".

Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.