Chuo cha BBC cha Uandishi wa Habari, (BBC Academy, College of Journalism) chafungua upya tovuti ya Kiswahili kwa ajili ya waandishi wa habari duniani kote.

Chuo cha BBC cha Uandishi wa Habari kimeanzisha upya tovuti ya Kiswahili katika mfumo (mtindo) mpya na maswala mapya.
Tovuti yenyewe inaweza kupatikana kwenye simu ya mkononi, tabiti (tablet) na komputa kubwa.

Lengo la tovuti ya Kiswahili ni kuonesha mtindo wa uandishi katika idhaa za lugha mbali-mbali zinazotangaza katika Idhaa Kuu ya Dunia ya BBC, na ni sehemu ya jukumu la BBC la kuhudumia jamii na kusambaza ujuzi wake ili kunufaisha waandishi wa habari wa Kiswahili dunia nzima.

Ali Saleh, Mhariri wa Idhaa ya Kiswahili:

"Baada ya serikali za Afrika Mashariki kuruhusu vyombo vingi vya habari binafsi kuanzishwa, vinatoa ushindani mkubwa kwa vyombo vya habari vya kimataifa. Ingawa vyombo hivyo vimestawi na kuzidi kukua, vyombo vinavyojitegemea vinakabiliwa na tishio katika nchi kadha, ambako waandishi wa habari wamekimbia kwa sababu ya kulengwa kwa mashambulio na mashtaka. Serikali katika nchi ambako BBC inasikika zinatayarisha sheria kali kupunguza uhuru wa kujieleza, haki ya kutofichua chanzo cha taarifa, na kuwafunga waandishi wa habari kwa yale waliyotangaza."
Tovuti ina maeneo matatu muhimu, ufundi wa uandishi, lugha ya Kiswahili, na maadili ya BBC.

Kupitia sehemu hii ufundiutapata ushauri kuhusu televisheni, redio na mtandao, utangazaji, uandishi, mitandao ya jamii na mengi mengineyo.

Katika sehemu hii wahariri na waandishi wa BBC wanaeleza namna ya kutangaza na kuandika taarifa za televisheni na jinsi ya kuandika ripoti kuhusu michezo. Tovuti inatoa mwongozo jinsi ya kuthibitisha habari zilizoko kwenye mitandao ya jamii.

Katika sehemu yavigezo, kuna ushauri kuhusu msimamo wa kutopendelea upande wowote, ukweli, uhuru, maslahi ya jamii, uwajibikaji na sheria.

Lakini msingi wa kila tovuti ni lugha. Sehemu yalugha inatoa ushauri kuhusu lugha isiyopendelea upande wowote, lugha sahihi, tahajia, ufupisho, majina ya kigeni na ufundi wa kutafsiri na mengineyo.

Sehemu ya lugha ya tovuti ina vielelezo vilivyotengenezwa maalumu kulingana na utamaduni wa Kiswahili. Juhudi zimefanywa kuelezea sehemu hii kwa picha zinazoonesha Idhaa iliyohusika ya BBC pamoja na wasikilizaji na watazamaji.
Pamoja na tovuti ya Kiswahili, Chuo cha Uandishi wa Habari cha BBC, (College of Journalism) piya kinaanzisha lugha tatu nyengine,Burmese,Pashto naVietnamese. Tovuti hizo nne zinafanya jumla ya tovuti za chuo cha BBC zilizoanzishwa upya kufikia 11.

Katika miaka mitano iliyopita BBC College of Journalism, imeanzisha jumla ya tovuti 27 katika lugha tofauti.
Unaweza kusoma tovuti za BBC College of Journalism bila ya kutozwa pesa kokote uliko duniani.

KATIKA miaka mitano iliyopita BBC College of Journalism, imeanzisha jumla ya tovuti 27 katika l
ugha tofauti. Unaweza kusoma tovuti za BBC College of Journalism bila ya kutozwa pesa kokote uliko duniani.

Chanzo:BBC Swahili
Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.