WABUNGE wa Seneti jimbo la Hawaii nchini Marekani limekuwa jimbo la kwanza nchini Marekani hivi karibuni kupitisha kwa kura moja muswada wa sheria ya ndoa za mashoga na kuhalalisha mapenzi ya jinsia moja katika jimbo hilo.
Wafuasi wa ndoa za jinsia moja katika Hawaii sherehe katika mji wa Honolulu |
Serikali
ya jimbo la Seneti lapitisha kwa kura 19 kwa 4 za waliopiga muswada huo wa ndoa
za mashoga nchini huo.
Gavana
wa jimbo la Hawaii aliyechaguliwa kidemokrasia anasema atasaini muswada huo wA
sheria za ndoa za mashoga bila kuchelewa Ili kutoa haki ya watu wanaoamini
hivyo, sheria hiyo inatazamiwa kuanza rasmi kutumika tarehe 2 Desemba mwaka
huu.
Wafuasi wanaodai ndoa za jinsia moja |
Taarifa
zinasema kuwa ndoa za jinsia moja nchini Marekani zimepitishwa katika majimbo
14 na wilaya moja ya Columbia.
Waandishi
wanasema muswada huo wa sheria za ndoa ya jinsia moja itafanya jimbo la Hawaii
kuwa maarufu kwa harusi za mashoga na wasagaji kupita majimbo yote nchini
Marekani.
Watafiti
katika Chuo Kikuu cha Hawaii wamesema kwamba sheria hiyo itakuza utalii kwa mapato USD 217m (£ 136m ) ndani
ya miaka mitatu ijayo.
"Natarajia
kusaini kipande hii muhimu cha sheria, ambayo inatoa usawa wa haki za binadamu
kwa watu wa jinsia moja kufunga ndoa kisheria na kulinda uhuru wa kuabudu na wa
kidini,” amesema gavana wa jimbo la Hawaii Neil Abercrombie
Rais
wa Marekani Barack Obama amekaribisha kura ya Jumanne wiki hii kwa kusema “. Nimekuwa
daima najisikia fahari kuzaliwa katika jimbo la Hawaii na kura hii ya leo
inanifanya nijisikie fahari zaidi na zaidi ,’ amesema
Wengi
wamepokeza baada ya kesi ya mwaka 1990 katika jimbo la Hawaii ambapo wanawake
wawili waliomba kibali cha kufunga ndoa lakini wakazusha mjadala mkubwa kuhusu
ndoa za jinsia moja nchini nzima.
Ilipelekea
karibu majimbo 30 kupiga marufuku ndoa za jinsia moja na kusababisha baraza la
Congress kupitisha sheria ya ulinzi wa ndoa mwaka 1996.
Na
sheria hiyo ya ulinzi wa ndoa ilifafanua kwamba ndoa ni kati ya mwanaume na
mwanamke lakini sheria hiyo ya ndoa ilipigwa chini Mahakama Kuu nchini Marekani
mwanzoni mwa mwaka huu.
Kura
za jumanne katika jimbo la Hawaii limeongeza kasi ya haki za mashoga kuweza
kufunga ndoa nchini Marekani.
Wakati
huo huo, Maseneta wa jimbo la Illinois walipitisha muswada wa ndoa za jinsia
moja mapema mwezi huu na gavana wa jimbo hilo, Pat Quinn amesema atasaini kuwa
sheria tarehe 20 November mwaka huu.
Mwisho.
Na
Damas Makangale, Moblog kwa Msaada kwa Mtandao
Post a Comment