Siku moja baada ya nguli ya sheria za katiba nchini, Dakta Sengodo Mvungi kuaga dunia nchini Afrika Kusini, Jeshi la Polis Kanda Maalum Ds, linamshikilia mtuhumiwa mmoja John Ikondia Mayunga (56) kwa kosa la kushiriki kikamilifu kwenye mauaji ya mwanasheria huyo na mjumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba.
Marehemu, Dakta Sengodo Mvungi wakti wa uhai wake |
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar
es Salaam, Kamanda wa Kanda Maalum Dsm, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi
(ACP) Suleiman Kova amesema mtuhumiwa huyo ni mkazi wa kiwalani walipata
taarifa kwa raia wema kwamba alishiriki kikamilifu kwenye tukio hilo
lilosababisha kifo cha Dakta Sengodo Elibariki Mvungi.
Kamanda wa Kanda Maalumu Dsm, Kamishna msaidizi wa jeshi la Polisi, Suleman Kova |
“mnamo
tarehe 12/11/2013 Polisi walipata taarifa kutoka kwa raia mwema kwamba kuna mtu
ambaye amehusika na tukio la mauaji ya Dakta Mvungi na kwamba kipindi hicho
mnamo saa 12 jioni mtuhumiwa alikuwa maeneo ya mtaa wa Twiga jangwani akiwa
anaangalia Televisheni,” amesema Kamishina Kova
Kova
amesema kwamba mtuhumiwa alitambuliwa na kukamatwa kisha kuhojiwa na Polisi na
alikubali kwamba alihusika na akawaongoza askari hadi nyumbani kwake kiwalani
Migombani.
Alifafanua
kwamba taratibu za upekuzi zilifanyika na katika upekuzi vilipatikana silaha
ambayo ni bastola aina ya REVOLVER N0. BDN 6111 pamoja na risasi ishirini na
moja.
Kova
amesema kuwa mtuhumiwa alikiri kwamba katika vitu vitu vilivyoibwa nyumbani kwa
dakta Mvungi ni pamoja na bastola hiyo aidha siku ya tukio hilo walitumia
milipuko kutishia ili kufanikisha uporaji huo.
Kamanda
Kova alisisitiza kwamba mtuhumiwa huyo ni wa kumi kukamatwa kuhusiana na tukio
hilo na bado operesheni kali inaendelea ili kuhakikisha kuwa yeyote aliyehusika
na tukio hilo anakamatwa kwa nguvu za dola.
Mwisho.
Na
Damas Makangale, Moblog
Post a Comment