Mike ‘Iron’ Tyson asimulia mikasa, vituko, ukatili katika maisha yake ya ujanani  


.Pamoja ya kuwa mbabe alikuwa anaogopa kwenda jela


.alilazimika kwenda kuhani kwa mchungaji asifungwe jela 
Bingwa wa Zamni wa masumbwi bondia, Mike Tyson au kama alivyokuwa amezoeleka Mike "Iron" Tyson

 Jinsi Mike Tyson alivyojaribu kwenda kwa mchungaji kuhani asifungwe gerezani baada ya kumdhalilisha mpenzi wake katika simulizi hilo jipya Mike ‘Iron’ Tyson anazungumzia maisha yake ya kikatili enzi hizo.

Mike Iron Tyson katika moja ya matukio yake ya karibuni katika fani ya kuigiza

Bingwa huyo wa zamani wa uzito wa juu duniani (Heavyweight) anasimulia maisha yake ya kufilisika, madawa ya kulevya, ulafi katika maisha na kuvunjika kwa ndoa zake kadhaa tangu enzi za Robin Givens.


Anasema pamoja na yote hayo lakini amejitahidi kuwa baba mzuri na mume safi kwa watoto na mke wake mpya, Tyson amesema kwamba kufungwa jela kumemsaidia kubadilika kwa sababu bila hivyo angekuwa mtu wa ovyo sana na mkatili.  

Amesema kwenye mazungumzo na gazeti moja huko nchini Marekani kwamba hakuwahi kupata malezi bora ya mama wala baba kwani mama yake alikuwa mnywaji sana wa pombe na mara nyingi alikuwa analala na wanaume wengi kila siku katika sehemu waliyokuwa wakiishi. 

Alifafanua kwamba alikuwa anapenda kutizama mikanda ya cinema ya Mohammed Ali ‘The Greatest’ ambayo ilimsaidia kufikia ndoto zake za kuwa bingwa wa dunia wa uzito wa juu duniani na mwanamasumbwi.


Anasema kuwa mke wake wa kwanza Robin Givens na mama yake walikuwa wasanii nguli katika maisha na makahaba lakini pia kama haitoshi mke wake wa pili alimdanganya Tyson kuwa ana ukimwi lakini kumbe ulikuwa uongo mtupu.

Wakati wa Kusikiliza kesi yake ya ubakaji Tyson alikuwa anadhani ni kitu cha kawaida pindi Jaji Patricia Gifford alivyokuwa akisoma hukumu ya ubakaji, ilikuwa ni Machi 26, 1992, wiki sita baada ya kukaa lupango alipokuwa akisomewa hukumu ya kumbaka na kumdhalilisha mrembo Desiree Washington (18) alikuwa anakabiliwa na adhabu ya miaka sitini jela.
Aliyekuwa mke wa Mike Tyson, Robin Givens

Lakini kesi hiyo ilikosa ushahidi wa kutosha kwamba Tyson alimbaka mrembo lakini kosa la kudhalilisha (Sexual harrassement) lilifanya afungwe miaka sita lakini alikaa miaka mitatu jela.
Enzi za furaha akiwa ndani ya ndoa yake, Mike Tyson na Robin Givens

“siku ya hukumu na kutiwa hatiani ya kwenda jela miaka sita nilijua ndio siku ya kuokolewa toka katika maisha ya ovyo, kiburi, ukatili na ulevi wa madawa ya kulevya umewadia,” amesema Tyson

Alizaliwa katika Hospitali ya Cumberland katika Fort Greene, Brooklyn, Tyson kamwe hakuwahi kumjua baba yake mzazi lakini cheti cha kuzaliwa kimeandikwa Percel Tyson mtu ambaye anaamini ndio baba yake mzazi lakini hajawahi kukutana naye.


Mama yake  Loma Mae anasema 'baba yake wa kibaiolojia,  ni ' Jimmy ' Curlee ' Kirkpatrick Jr.’



Mike Tyson akiwa katika picha ya pamoja na mshirika wake mkubwa katika masumbwi na promota wake Don King pamoja na mkewe Robin Givens mnamo mwaka 1996

Anasimulia zaidi kwamba mama yake alivyopoteza ajira kama matron katika nyumba ya wanawake mahabusu katika jiji la Manhattan ndipo alipoanza kunywa pombe masaa 24 na kulala na wanaume ovyo.


Mwisho 

Chanzo cha habari Na Damas Makangale, Moblog Kwa Msaada wa Mtandao
Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.