Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif amesema Jamhuri ya Kiislamu inalipa umuhimu mkubwa suala la uhusiano wake na nchi za Afrika ikiwemo Afrika Kusini.
Zarif
ameyasema hayo akiwa mjini Pretoria Jumatano usiku na kuongeza kuwa, ‘Afrika
Kusini ni moja ya nchi muhimu katika bara la Afrika na moja kati ya nchi zenye
ushawishi mkubwa kimataifa.’
Amesema
Iran inataka kuboresha uhusiano wake na nchi hiyo ya Afrika huku akielezea
matumaini aliyonayo kuwa sekta binafsi na za kiserikali za nchi mbili zitatoa
msukumo mkubwa katika uhusiano wa kiuchumi, kibiashara na kiufundi.
Zarif
yuko Afrika Kusini kuhudhuria kikao cha 11 cha Tume ya Pamoja ya Ushirikiano ya
Iran na Afrika Kusini. Kikao hicho kinafanyika leo na Zarif ameelezea matumaini
yake kuwa kitakuwa na natija nzuri itakayopelekea kukurubisha uhusiano wa nchi
mbili katika nyanja za viwanda na biashara.
Kikao hicho kitafanyika chini ya uenyekiti wa
Zarif pamoja na Waziri wa Ushirikiano na Uhusiano wa Kimataifa wa Afrika Kusini
Bi. Maite Emily Nkoana-Mashabane. Zarif pia anatazamiwa kukutana na maafisa wa
ngazi za juu wa Afrika Kusini akiwemo Rais Jacob Zuma.
Mwisho.
Picha
ya Mohammad Javad Zarif
Chanzo:
Iran Swahili Radio
Post a Comment