Rais wa zamani wa Zambia Rupiah Banda, amekana mashitaka katika kesi inayomhusisha na ufisadi wakati wa kampeni za uchaguzi wa mwaka 2011.
Kiongozi huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 76, anatuhumiwa
kupokea lori 10 kutoka kwa tawi moja la kampuni ya ujenzi ya kichina na kukosa
kutangaza kuwa alipokea lori hizo.
Baada ya miaka mitatu madarakani, Banda alishindwa na rais
wa sasa Michael Sata katika uchaguzi wa mwaka 2011.
Hii ni kesi ya pili ya ufisadi inayomkumba Banda tangu
kuondolewa kinga dhidi ya kushitakiwa mnamo mwezi Machi.
"ninaelewa mashitaka na ninayakanusha ,'' amesema Banda
alipofikishwa mbele ya Hakimu na kusomewa mashtaka dhidi yake.
Inadaiwa kuwa rais huyo wa zamani, alisajili lori hizo
alizopokea kutoka kwa kampuni ya kichina ya Anhui ,kwa majina ya jamaa zake
pamoja na mfuasi wake mmoja na kisha kuyatumia wakati wa kampeni zake mwaka
2011.
Serikali ya Rais Sata imeanzisha uchunguzi kuhusu madai ya
ufisadi dhidi ya waliokuwa viongozi katika serikali ya Banda.
Lakini wakosoaji wa Rais Sata wanasema kuwa anatumia mbinu
hii kuwakandamiza wakosoaji wake.
Mnamo mwezi Machi, Banda pia alikana mashitaka ya ufisadi
dhidi yake kuhusu mkataba aliotia saini na kampuni ya mafuta ya Nigeria ambayo
viongozi wa mashtaka wanaamini ulinuiwa kufaidi familia ya Banda.
Rupiah Banda aliongoza Zambia kwa miaka mitatu
Mwisho
Picha: Rupiah Banda
Chanzo: BBC Swahili
Post a Comment