Lowassa alitoa kauli hiyo mjini Dodoma katika kikao cha
bunge kinachoendelea akisema nchi inakosa viongozi jasiri wenye kusimamia
utekelezaji wa mambo waliyoamua katika Nyanja mbalimbali za maendeleo.
“wananchi, wanasiasa, wabunge, viongozi wanalalamika
hatuwezi kuwa na jamii ya kulalamika lazima mtu mmoja ajitokeze na kufanya
maamuzi magumu lazima ajivishe joho la ujasiri ili mambo yaende,’ amesema
lowassa
Amesema nchi ina tatizo kubwa la uswahili mwingi wa kukaa na
kushidwa kutekeleza mambo yaliyoamualiwa kwenye vikao kiasi cha kufanya kila
mtu kulalamika kwa wakati wake
Lowassa amesema kuwa hata matokeo makubwa sasa au “Big
results Now” haiwezi kutekelezwa kwa sababu ya uswahili na mazingira ya hapa
Tanzania na Malaysia ni tofauti hapa ni uswahili tu ndio unaosumbua taifa letu
lishindwe kusonga mbele.
“Tukishakubaliana mambo ni lazima yafanyike. Ni lazima
tuondokane kuwa nchi ya kulalamika kuanzia kiongozi wa juu mpaka mwananchi,”
alisisitiza
Lowassa aliendelea kusisitiza kwa kusema katika kutekeleza
mipango ya serikali kama ilivyopangwa bila woga wala kigugumuzi lazima viongozi
wote waliopewa dhamana ya kuongoza waongoze kwa vitendo waache uswahili ili
taifa liweze kusonga mbele.
Tunakubaliana naye kwa sababu, siku za hivi karibuni tumeona
wamiliki malori wakikataa kulipa tozo ya asilimia tano kwenye mizani ya
serikali wakati sheria ya ongezeko la asilimia hizo tano lilipitishwa na bunge
na waziri mwenye dhamana John Pombe Magufuli alikuwa sahihi kwa kusimamia
sheria lakini kawa kawaida Magufuli alipigwa stop na viongozi wake kwanini?
Sheria za nchi hazifuatwi yale yale uswahili.
Lowasa ambaye ni mbunge wa Monduli (CCM) amesema kuwa ni
vema serikali ingekuwa na mipango michache yenye kutekelezeka na tija kwa
taifa.
Aliongeza kuwa kama angekuwa kiongozi wa serikali angejikita
kwenye vipaumbele vitatu ambavyo ni ajira, Reli ya Kati na elimu kuliko kuwa na
vipaumbele vingi visivyotekelezeka.
Alibainisha kuwa tatizo kubwa linaloifanya serikali ishindwe
kufanya vizuri kwenye maeneo mbalimbali ni kujiwekea vipaumbele vingi huku
rasilimali zake zikiwa chache na wakati mwingine zile zinazopatikana hazitumiwi
vizuri.
Mwisho.
Damas Makangale
Post a Comment