Mwana wa Malkia wa Uingereza, Prince Charles matatani kwa kukwepa kodi anakabiliwa na uchunguzi juu ya fedha zake ambazo hazilipi kodi
Wabunge wataka achunguzwe na malipo ya fedha zake ziwe wazi kwa umma
Mwana wa malkia
wa Uingereza, Prince Charles matatani anakabiliwa na shutuma kali za kukwepa
kulipa kodi na upendeleo katika kulipa kodi za nchi na sasa wabunge wanataka
achunguzwe kwa mapato yake halisi na yawe wazi kwa umma wa Uingereza.
Wabunge wa
Uingereza wanadai kwamba malipo yake si wazi na kodi yake anayolipa pia haipo
wazi kama inavyotaka sheria za nchi hiyo ya Uingereza.
Prince Charles
anakabiliwa uchunguzi wa mapato yake na wabunge wanadai uchunguzi wa mwana huyo
wa malkia uwe wazi na safi na njia yeye kufadhiliwa katika vitu mbalimbali viwe
wazi kwa umma.
Kamati ya fedha
za umma ya bunge imesema kuwa mali za kampuni ya Duchy wa Cornwall inayomilikiwa na Prince
Charles, ardhi na faida kubwa kutoka kampuni ya Holdings ambayo kumlipa
Prince Charles zaidi ya Paundi 19milion kwa kila mwaka, hazina kodi za
biashara.
Na wakati huo
huo, Taarifa zinasema kama mrithi mtarajiwa wa malkia wa Uingereza alipaswa
kuwa makini na malipo ya kampuni zake kwenye kodi, ongezeko la thamani na
sheria zingine za kodi, kamati hiyo ya bunge inahoji.
Margaret Hodg ,
Mwenyekiti wa Kamati huru ya Hesabu za Serikali , amesema idadi ya hatua
zinahitajika kuchukuliwa ili kuleta wamiliki wa kampuni ya Duchy ' ili waieleze vizuri kamati ya bunge.
Duchy , ni
kampuni ya majengo inayomilikwa na Prince Charles yenye thamani ya Paundi za Kiingereza 847million
,
Bibi Hodge
amesema: ' Duchy inafurahia msamaha wa kulipa kodi hata kama inafanya kazi kwa
faida kubwa na biashara za aina mbalimbali. Lakini Bibi Hodge anadai kutoa
msamaha wa kodi kwa kampuni kama hiyo ni
kuwaumiza washindani wake ambao hulipa kodi
kwa mujibu wa sheria za nchi.
Mwisho
Post a Comment