ILIKUWA kama filamu fulani hivi. Leodgar Tenga alitumia saa nne,
kuanzia saa tano asubuhi mpaka saa nane kumkabidhi ofisi Jamali Malinzi
juzi Jumamosi. Baada ya kukabidhiwa rungu Malinzi akawaambia wajumbe
wote 18 wa Kamati ya Utendaji; “Tukutane mara moja.”
Angetile alipoulizwa alisema; “Nimepata taarifa hizo lakini sina cha kuzungumza kwa sasa, bado natafakari nitatoa tamko kesho (leo Jumatatu) au keshokutwa(Jumanne).” |
Wakapanda gari wakaelekea kwenye hoteli moja
iliyoko Kariakoo, jijini Dar es Salaam. Baada ya kufika hapo akataja
ajenda halafu akashtua hadhira baada ya kutamka kwamba hana imani na
Katibu Mkuu, Angetile Osiah. Hivyo akamtaka atoke nje ya kikao hicho ili
ajadiliwe ndipo wajumbe walipomuunga mkono Malinzi kwa hoja na kutaka
Angetile apigwe chini na nafasi yake akaimu Ofisa Habari, Boniface
Wambura ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari na mwanasheria.
Ndipo jana Jumapili, Malinzi akatangaza rasmi
uamuzi huo na kusema kwamba Angetile ambaye mkataba wake unamalizika
Desemba amepewa likizo yenye malipo mpaka mkataba wake utakapokwisha
Desemba.
Malinzi alitwaa madaraka hayo baada ya kumshinda
Athuman Nyamlani katika uchaguzi wa shirikisho hilo uliofanyika Jumapili
ya wiki iliyopita.
Malinzi ambaye Fifa na CAF zimekubali ushindi
wake, alisema uteuzi wa Wambura ulianza rasmi juzi Jumamosi na aliziomba
klabu, vyama vya wilaya, vyama vya mikoa, vyama shiriki na wadau wa
soka wampe ushirikiano Wambura kwenye utendaji wake.
Angetile alipoulizwa alisema; “Nimepata taarifa
hizo lakini sina cha kuzungumza kwa sasa, bado natafakari nitatoa tamko
kesho (leo Jumatatu) au keshokutwa(Jumanne).”
Awali baada ya kushinda hata kabla kukabidhiwa
ofisi Malinzi alitangaza kufuta kamati zote za shirikisho hilo na kuunda
nyingine mpya kwavile hana imani na ufanisi wake kwavile nyingi
zilikuwa zikipepesuka kwenye uamuzi.
Malinzi ameahidi kusafisha vitengo mbalimbali vya TFF na kurejesha hadhi ya utendaji kwenye soka la Tanzania.
Chanzo: Gazeti la Mwanaspoti
Chanzo: Gazeti la Mwanaspoti
Post a Comment