Baadhi
ya wafanyakazi wa Airtel mwishoni mwa wiki wameitembelea shule ya
msingi ya Kiromo iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani na kutoa mafunzo ya
awali juu ya matumizi ya kompyuta kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Wafanyakazi
hao wamedai kuwa kujitolea kwenda kutoa mafunzo katika shule hiyo
ambayo ilijengwa na kampuni yao kupitia mradi wa shule yetu sio jambo la
msimu tu kwani wana mpango wa kuendelea kutoa huduma hiyo mara kwa mara
katika shule mbalimbali nchini.
Mkurugenzi
wa idara ya Fedha ya Airtel, Bw. Kalpesh Mehta alisema Airtel inaelewa
wazi ni jinsi gani matumizi ya vifaa kama kompyuta hurahisisha kazi
nyingi katika jamii na hivyo imeamua kwenda kutoa mafunzo ya ujumla kwa
wanafunzi wa shule hiyo kwa dhumuni la kuleta mchango chanya kwenye
jamii.
“Kompyuta
ni kifaa muhimu sana ambacho hurahisisha kazi mbalimbali zinazofanywa
kwa ajili ya maendeleo ya jamii hivyo inabidi wanafunzi waanze kujifunza
juu ya umuhimu wa kifaa hiki mapema katika kusaidia maendeleo ya jamii
huko mbeleni.” Alisema Mehta.
Kwa
upande wake Mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya Kiromo, Bw. Joseph
Ngunangwa alisema masomo hayo yametoa hamasa kubwa sana kwa wanafunzi wa
shule hiyo kwa sababu yamewafanya wahisi masomo hayo yana urahisi na
sio magumu kama walivyokuwa wakifikiria.
“Wanafunzi
walikuwa na mitazamo kwamba wanaojifunza kompyuta ni tabaka flani tu la
watu na walikuwa wakihisi kwamba kompyuta ni somo gumu lakini leo
wametiwa moyo na wafanyakazi wa Airtel na wameanza kuona kuwa somo hilo
ni rahisi na yeyote anaweza kulisoma na kufaulu vyema,” alisema
Pangahela.
Mwalimu
huyo aliongeza kuwa kupitia masomo hayo idadi ya wanafunzi watoro
imepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na sababu kuwa wengi huja shule kwa
ajili ya kujifunza kompyuta.
Kwa
upande wao wanafunzi wa shule ya Kiromo waliwashukuru wafanyakazi wa
Airtel kwa kuonesha ukarimu mkubwa sana na kusema kuwa wanatamani masomo
hayo yangekuwa yanafanyika kila siku.
Si
mara ya kwanza kwa wafanyakazi wa Airtel kuzitembelea shule na kutoa
mafunzo kama hayo vile vile Kampuni hiyo hutoa misaada ya vitabu
mbalimbali vya kiada nchini na kuchangia katika ujenzi wa taifa hususani
katika sekta ya elimu.
Post a Comment