.watanzania
wahimizwa kununua bidhaa zinazotengenezwa na wazawa
WANAWAKE
Wajasirimali nchini wameaswa kuzingatia umuhimu wa ubora kwenye bidhaa zao
wanazozalisha kwa kuzingatia viwango vya kitaifa na kimataifa ili kupata soko
la uhakika ndani na nje ya nchi. Moblog linaripoti.
Akizungumza
kwenye kilele cha wiki ya Wajasirimali Wanawake Tanzania (MOWE) Mke wa Waziri
Mkuu, Mama Tunu Pinda amesema wanawake wanaweza kufanikiwa endapo watazingatia
ubora wa vifungashio (Packaging) wanavyotumia kwenye bidhaa zao.
Mama Tunu Pinda, Mke wa Mheshimiwa Waziri Mkuu Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda |
“Nimedokezwa
kwamba baadhi ya wajasirimali wamejisajili na kupata kiandishi-anuani yaani
Barcodes, hapa Tanzania, mfumo huu umeanza kutumika hivi karibuni na
wajasirimali wengi wameshawishiowa kujiunga ili bidhaa zao ziweze kutambuliwa
kitaifa na kimataifa,’ amesema
Mama
Pinda amesema kwamba watanzania wote wake kwa waume lazima wapende kununua
bidhaa zinazotengenezwa hapa nyumbani ili kuweza kuwainua wajasirimali wazawa
hasa wakinamama kwa kuunga mkono kampeni ya “Be Tanzanian, Buy Tanzanian”
inayohimiza kuwa Mzalendo, Nunua bidhaa za kitanzania.
Amesema
hata hivyo, kuna baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na baadhi ya vikundi vya hapa
nyumbani bado hazijaweza kumudu ushindani wa soko na kukubalika kuuzwa kwenye
maduka makubwa yaani supermarkets.
Mama
Pinda aliongeza kuwa changamoto nyingine kubwa inayowakabili wajasirimali wenhi
ni kutozingatia viwango vinavyotambulika katika soko la ndani la nje ili bidhaa
za wazawa ziweze kupenya kwenye soko la kitaifa, kikanda na kimataifa kwa
maslahi mapana ya wajasirimali na nchi kwa ujumla.
“kwenu
akinamama wajasirimali na wale waliohidhuria wasio wajasirimali ni matumaini
yangu kuwa mmetumia fursa hii kubadilishana mawazo na kujenga mitandao ya
kusaidiana na kuendelezana,” alisisitiza
Kwa
upande wake, Mratibu wa kitaifa wa Programu ya kuendeleza Ujasirimali kwa
Wanawake Tanzania kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO) Noreen Toroka amesema
shirika la kazi linafarijika kuchangia katika mipango na program za serikali za
kuchangia ukuaji wa ajira kwa kupitia program za ILO katika kumuendeleza
mjasirimali mwanamke nchini.
“kwa
takribani miongo miwili ILO imekua ikifanya kazi kuhakikisha ujasirimali
unachangia ajira na kipato kwa kina mama na tunajivunia kuwa kati ya wadau
wengi walio katika kujengea uwezo washirika wetu idara za serikali, asasi za
kifedha na zisizo za kifedha katika kuwainua wajasirimali wakinamama Tanzania,”
amesema
Toroka
amesema katika kuendeleza wakinamama nchini ILO imetoa mafunzo ya ujasiriamali
kwa wanawake zaidi ya 500 na kuwaunganisha na huduma za kifedha na wataalamu wa
ujasiriamali kwa elimu ya biashara na stadi za kazi.
“Kupitia
washirika wetu ILO imefikia wakina mama 100 Mkoani Lindi na tunashukuru wadau
wtu WAMA Foundation na program yao ya village savings and loan, wakinamama hao
walipata mafunzo ya ujasiriamali na tunategemea watapata mikopo nafuu ili
waweze kuanzisha, kuboresha na kupanua biashara zao,” aliongeza
Mwisho
Habari na Damas Makangale
Post a Comment