Wazazi na walezi wa kijiji cha Jendele na Vijiji jirani wameshauriwa kuwapeleka watoto wao Skuli za Maandalizi mapema wakiwa na umri wa miaka mitatu ili kuwajengea uwezo na ufahamu wakiwa na umri mdogo.
Hayo yameelezwa leo na Mratibu wa Jumuiya ya Skuli za
Maandalizi za Madrasa Mohamed Othman Dau wakati alipokuwa akizungumza na walimu
pamoja na wanafunzi wa Skuli ya Maandalizi Nuru Islamia iliyopo Kijiji cha
Jendele.
Amesema kumpeleka mtoto Skuli katika umri huo
ni kumkuza mtoto kiakili na kimwili kwani kufanya hivyo inampekea kuwa na
ufahamu nzuri katika masomo yake.
“ Ni vyema wazazi waone ni muhimu
kuwapeleka Skuli za Maandalizi watoto wao kwani kufanya hivyo ni kuwaandaa
katika msingi bora wa kielimu,alisema Mratibu wa Jumuiya Mohamed Othman Dau”.
Afisa Lishe Shemsa Nasour Mselem amesema ni
vyema wazazi kuzungumza na watoto wao wakati wakiwa tumboni kwani kufanya hivyo
humjengea mtoto huyo kufahamu haraka wakati akisha zaliwa.
Aidha amesema ni bora wazazi kuwapatia watoto
wao chakula chenye mchanganyiko wa virutubisho mbali mbali kwa ajili ya
kuwajenga watoto hao miili yao kwani kufanya hivyo huwafanya kuwa na Afya
bora .
Nao wazazi wa watoto hao wamesema wamefarajika kwa
kupatiwa mafunzo hayo kwani wengi walikuwa hawafahamu namna ya kuwaandaa watoto
wao na kuwapatia lishe bora.
Hata hivyo wamesema kwamba wameshukuru Jumuiya
ya Maendeleoya ukuwaji wa Mtoto (CCD) kwa kupatiwa mafunzo ya naman ya
kuwaandaa watoto wao wakiwa na umri mdogo jinsi ya kujifunza kucheza
kabla kupelekwa Skuli za Maandalizi.
Post a Comment