Mwandishi Wetu, Beijing, China

Waandishi wa habari waandamizi kutoka Tanzania, Zimbambwe, Sudani Kusini, Ivory Coast and Uturuki wameshiriki mafunzo kwa vitendo nchini China hivi karibuni.

Mafunzo hayo yalihusu maendeleo ya teknolojia na mapinduzi yake ili kuleta matokeo chanya kwenye sekta ya habari na mawasiliano ya umma, na maendeleo ya taifa kwa jumla.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo  yaliyopewa kauli mbiu ya “Semina juu ya usimamizi wa vyombo vikuu vya habari katika nchi zilizo katika mpango wa ukanda na barabara” (Seminar on Senior Management of Mainstream Media in countries along the Belt and Road Initiative, -  ukanda mmoja na  njia moja ) Bw Augustino John Tendwa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) alisema mafunzo hayo yanayoendelea yamejikita katika kuleta fikira, ubunifu na matumizi ya kidigitaki katika kuleta mapinduzi ya tekolojia katika nchi za washiriki.

Afisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bw Augustino John Tendwa (wa kwanza kulia) akishiriki kwenye mafunzo ya mapinduzi ya teknolojia yanavyoweza kuleta matokeo chanya kwenye sekta ya habari na maendeleo ya Tanzania kwa jumla.

Bw Tendwa alieleza kwamba washiriki wa mafunzo hayo ya vitendo walipata fursa ya  kutembelea makao makuu ya kampuni ya kimataifa ya teknolojia – Laird Technologies – kujifunza kwa vitendo maendeleo ya kiteknolojia yanayofanyika nchini China.

Wakiwa jijini Beijing, washiriki waliweza kujionea kwa karibu namna kampuni hiyo inavyoendesha uzalishaji wa vifaa vya hali ya juu vya kielektroniki, vikiwemo vifaa vya mawasiliano ya wireless, udhibiti wa joto, mitetemo na teknolojia ya kupunguza mwingiliano wa sumaku-umeme (EMI shielding).

Picha ya pamoja ikiwaonyesha maafisa habari kutoka Tanzania, Zimbambwe, Sudani Kusini, Ivory Coast and Uturuki wakihudhuria semina ya mafunzo kuhusu teknolojia inavyoweza kutumika kuleta maendeleo kwenye sekta za maendeleo kupitia vyombo vya habari na mawasiliano ya umma.

“Kampuni kama Laird ni mfano halisi wa namna China inavyowekeza katika ubunifu na utafiti wa kisayansi kwa ajili ya maendeleo ya teknolojia duniani. Hii ni fursa ya kujifunza na kutafuta maeneo ya ushirikiano kwa maendeleo ya sekta ya viwanda na teknolojia nchini kwetu,” alisema Bw Tendwa.

Aliongeza kwamba mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo waandishi na maafisa wa serikali kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika kuhimiza maendeleo kupitia ushirikiano wa kimataifa chini ya mpango wa ukanda na barabara.

Ushiriki wa Tanzania kupitia waandishi na maafisa waandamizi kutoka taasisi za serikali na vyombo vya habari ni ishara ya dhamira ya kukuza maarifa, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na atumizi ya teknolojia katika maendeleo ya taifa.














This is the most recent post.
Older Post

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.