Na Mwandishi
wetu, Arusha
Baraza la
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kupitia Program ya Imarisha Uchumi na Mama
(SAMIA) linalenga kuyaongeze uwezo wa biashara na ujasirimali makundi ya
Kinamama, Vijana na makundi maalum wa Mkoani Arusha hasa wanaofanya shughuli za
kitalii na biashara za nafaka zinazosafirishwa kwenda nchi za Afrika Mashairi.
Kauli hiyo
ilitolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Bi. Beng’i Issa wakati wa Baraza
hilo lilipozindua Program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia (IMASA) inayotekelezwa
na baraza hilo kuwa MKoa wa rusha kuwa makundi hayo yataongezewa uwezo w
kibiashara hasa katika maeneo ya utalii na nafaka zinazounzwa nje ya nchi.
Katibu
Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC}, Bi. Beng’i Issa
akizungumza na mwakundi ya kinamama, vijana na makundi maalum wakati baraza
hilo lilipozindua Program ya Imarisha Uchumi na Mama (SAMIA} mkoani Arusha.
Picha na Mwandishi wetu, Arusha.
“Mkoa huu wa Arusha ni wa kimataifa na umeshamili shughuli za kitalii na ni mpaka wa kusafirisha mazao ya nafaka kwa nchini za Afrika Mashariki,” na alioneza kusema program hiyo inalenga kuwaongezea ujuzi na uwezeshaji ili waweze kutumia fursa kama hizo kwa mafanikio makubwa zaidi.
Alisema
Royal Toure aliyofanya Rais Mama Samia Samia ilikuwa na mafanikio makubwa
katika mkoa huo ambao ni Jijiji kwa hiyo program zote zinazolisha utalii
zitatapata mafanikio kupitia utalii na IMAMA imejielekeza kwa fanya biashara
wadogowadogo na wajasirimali katika sekta hiyo wanufaike na kufikia viwango vya
kimataifa.
Alifafanuwa
kwamba Arusha ni jiji na makundi ya kinamama, vijana na makundi maalum yamekuwa
na mwamuko na shughuli zao hasa akimama kwa vile jiji linapokea watalii
wanaposhuka, mikutano ya kitaifa na kimataifa inafanyika hapo.
Pia alisema
akinamana wengi wanafanya shughuli za kuuza nafaka nje ya nchi na Tanzania
ndiyo inayolima mazao ya nafaka na kulisha nchi za Afrika Mashiriki kati ya
Tanzania na Kenya na hiyo ni fursa nzuri kwa watanzania kuvuka mpaka na kufanya
biashara nchi nyingine.
Alisema mkoa
huo makundi hayo yalionyesha mwitikio mkubwa wa kuipokea programa ya IMASA na inakadiliwa kulikuwa
zaidi ya washiriki 1500 wanawake, vijana, watu wenye ulemavu na wanaume.
Mshauri wa
wa Rais Masuala ya Wanawake, Bi. Sophia Mjema alisema wale wote
walioanjiandikisha wataingizwa katika kanzidata na aliyataka makundi hayo kuchaangamki
fura hiyo kupitia IMASA.
Mshauri wa
Rais Masuala ya akiwa na mwakundi ya kinamama, vijana na makundi maalum wakati Baraza
la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) lilipozindua Program ya Imarisha Uchumi
na Mama (SAMIA} mkoani Arusha kulia kwake ni Katibu Mtendaji wa baraza hilo,
Bi.Beng’i Issa. Picha na Mwandishi wetu, Arusha.
“IMASA imejipanga kutoa uwezeshaji kwa akinamama, vijana na makundi maalum na hasa akinamama na hakuna atakaye achwanyuma,” na aliongeza kusema kila mmoja katika mtaa wake, kitongozi chake, wilaya yake anahitajika kujiandikisha kuingia katika mfumo.
Naye Bi.
Sophia Amiri Makazi wa Arusha alisema wamepokea mafunzo kutoka IMASA na wanaona
kuwa inalenga kuwakwamua watanzania akinamama ambao bado wapo chini.
” Program
inataka kutunyanyuma akimama na makundi mengine na itamwezesha mwanamke
anayeishi katika nyuma ya nyasi kuishi katika nyuma ya bati,” na aliongeza
kusema anampongeza Rais Mama Samia kupitia baraza hilo kwa kupelekea programa
hiyo
Alisema
katika mkoa huo akinamama wanajishughulisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi
na ujio wa program hiyo inawawezesha kupata maarifa na uwezeshaji kukuza
biahara na ujasirimali.
Baraza la Uwezahaji Wananchi Kiuchumi NEEC
kupitia programa IMASA lipo katika hatua ya kutoa mafunzo kwa makundi ya
kinamama, vijana na Makundi Maalumu na kuwaingiza katika kanzidata na badaye
watapatiwa uwezeshaji ili waweze kukuza shughuli za biashara na ujasiriamali,
MWISHO
Post a Comment