Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam,

WITO umetolewa kwa taasisi za serikali, mamlaka, wafanyabiashara na wadau wengine wa maendeleo kuwashirikisha watanzania kwenye miradi mikubwa kama moja ya hatua ya kuwakuza ili kuchochea mapato ya nchini kwa ujumla.

Akizungumza wakati akifunga kongamano la nne la Ushiriki wa watanzania kwenye uchumi na uwekezaji (Local Content) ambapo lilihudhuriwa na washirikia takribani 300 hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati , Dkt Dotto Biteko alisema kwamba ushirikishaji wananchi kuingia kwenye miradi mikubwa kutafungua milango ya ukuaji wao.

“Ushirikishaji wanachi kuingia katika miradi mikubwa ya kimkakati ya kitaifa ni moja ya hatua ya kuwakuza watanzania kushiriki katika uchumi wao na taifa kujiepusha na fedha zake kwenda nje nchi kwa vile kwa muda mrefu miradi mikubwa ilikuwa inatekelezwa na wageni ambao faida walikuwa wanazipeleka nchini kwao na kukuza uchumi wa mataifa yao,” alisisitiza Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati

Aliongeza pia hii ni hatua muhimu kwa vile taifa letu katika kipindi hiki lipo katika hatua ya kujenga miradi mbalimbali ya kimkakati ambayo kimsingi lengo lake ni kuchochea uchumi na kukuza ustawi wa wananchi hivyo kupitia mkakati huo wananchi hawataachwa nyuma na uchumi utaimarika Zaidi.

Dkt Biteko alisema kwamba serikali ipo tayari kutoa fursa kwa watanzania kuweza kushiriki kwenye miradi hiyo na watanzania wajitokeze kuchangamkia fursa hizo na kwa sasa kuna mradi kama ya Bomba la mafuta kutoka Uganda kupitia Tanga, mradi mwingine wa bomba la mafuta Uganda kuja hapa nchini na muhimu watanzania wakapambana kupata kazi hizo.

“Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan pia alisema kuna upanuzi wa bomba la mafuta la Tazama , kuna mafuta mengi yanakwenda Zambia tunataka kufanya upanuzi mkubwa na kupunguza msongamano wa malori yanayoingia Dar es Salaam kuja kuchukua mafuta na hii miradi yote inataka ushiriki wa watanzania,” alisema Dkt Biteko.

Dkt Biteko pamoja na mambo mengine katika kuchangamkia hizi fursa aliwaasa taasisi za serikali na watanzania kuacha kuendekeza vitendo vya rushwa wakati wa kutoa au utafutaji na mchakato wa kupata tenda hizo za kazi hasa miradi hii ya kimkakati.

 

“Tuache vitendo vya kutoa rushwa ili kupata tenda za kiserikali hii muhimu katika kudumisha umuhimu wa kuzingatia ushiriki wa watanzania kwenye shughuli za uwekezaji na biashara, alisisitiza Dkt Biteko kwenye kongamano hilo ambapo lilihudhuriwa pia na wawekezaji kutoka nje,”

“Madhara ya kutoa fedha huku na kule ile kupata kazi matokeo yake ukipata kazi husika unashidwa kuikamilisha kwa sababu ya kutumia fedha nyingi na kukosa faida , matokeo namba zinagoma jamani tuache vitendo hivi vya rushwa,” alifafanua Dkt Biteko

Aliendelea tuache tabia pia za kusema bado hatujawa tayari kuendelea kujitafuta na hili jambo ndio linawarudisha nyuma watanzania kama kuamini kazi kubwa za miradi ya kimkakati hapa nchini.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchini, Ofisi ya Waziri Mkuu , Sera , Bunge na Uratibu, Bi Jenista Mhagama alisema kwamba serikali kupitia ofisi ya waziri mkuu itaendelea kuhakikisha watanzania wanpata fursa ya kushiriki kwenye uwekezaji na uchumi wa nchini yao.

“Mheshimiwa mgeni rasmi kwa upande serikali tutahakikisha kwamba tunakuwa na sera ya kitaifa ya ushirikia wa watanzania kwenye miradi hii na uchumi kwa ujumla kwa kutunga sheria na kanuni mbalimbali ili kupanua wigo wa watanzania kwenye biashara na uwekezaji,” aliongeza Bi Mhagama.

Akizungumza kwenye kongamano hilo la nne Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi Beng’I Issa alisema kwamba kongamano hilo hufanyika kila baada ya miaka miwili na hutoa fursa kwa wadau, serikali na wafanyabiashara kufanya tathimini ya ushiriki wa watanzania kwenye uchumi wao.

 “tangu tumeanza na sera na kanuni hizi za kuwataka wawekezaji kutoka nje wanaoshika miradi mikubwa kutoa fursa kwa watanzania kushiriki kwenye shughuli zao za kiuchumi na tumepata mafanikio makubwa sana idadi ya watanzania inaongezeka kila siku,” alisema Bi Issa

Aliongeza kwamba baraza hilo litaendelea kujenga uwezo wa watanzania kushirki kwenye miradi hiyo ya kimkakati ili waendelee kupata ajira, kutengeneza bidhaa ambazo zitapata masoko ya uhakika na kuweza kuinua kipato cha mtu mmoja mmoja.

Bi Issa alifafanua kwamba kongamano hilo lilianza rasmi 2017 na lengo la kuwa nayo kila baada ya miaka miwili ni kuongeza uelewa wa watanzania umuhimu wa kushiriki kwenye uwekezaji unaofanyika hapa nchini na kuweza kuzitambua fursa huku serikali ikiendelea kutengeneza mazingira mazuri kw awatu wake kushiriki kimamilifu.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Dotto Biteko (Katikati) akimpa tuzo, Bw Waisile Bairi , Meneja Mahusiano wa AKO Group kwa kutambua mchango wao katika kutekeleza dhana ya ushiriki wa watanzania kwenye uchumi na uwekezaji (Local Content) , Kulia kwa Naibu Waziri Mkuu , Mwenyekiti wa Bodi wa (NEEC) Profesa Aulelia Kamuzora na mwanzo kulia ni Katibu Mtendaji wa (NEEC) Bi Beng’I Issa 


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati , Dkt Dotto Biteko (Katikati) akimpa tuzo , Bi Neema Kweka msimamizi wa Sheria za wazawa kwenye mradi wa Bomba la Mafuta , kulia kwa Naibu Waziri Mkuu , Mwenyekiti wa Bodi wa (NEEC) Profes Aulelia Kamuzora na mwanzo kulia ni katibu Mtendaji wa (NEEC0 Bi Beng;I Issa 

Alisema kwamba baraza limefanikiwa kuunda mwongozo wa (Local content) na kutengeneza kamati za Taifa katika sekta zote

Aliongeza kwamba tangu kuanza kwa mfumo wa (Local content ) ajira 162,968 za moja kwa moja zimepatikana lenye ongezeko la 37.8% na vijana wenye umri kati ya miaka 18 hadi 35 walipata ajira 112,572 ambayo ni sawa na 69.1% ya ajira zote.

Alisema kwamba ajira za vijana 70% zilikuwa za ujuzi wa chini na 19% zilikuwa na ujuzi wa kati na 11% zilikuwa za ujuzi wa juu huku kampuni takaribani 3,360 za kitanzania zimepata fursa katika sekta za uziduaji (madini, mafuta na gesi) fedha, bima, uwekezaji, nishati, ujenzi, uchukuzi na ununuzi zimepiga hatua kubwa kwenye local content.

“Juhudi moja wapo za serikali ni kutungwa kwa sheria na kanuni zinazozingatia masuala ya ushirki wa watanzania , kwa mfano wakandarasi waliongia ubia ni 64 , haya ni mafanikio makubwa, “alisema Bi Issa

Alisema kwamba idadi ya miradi ya ujenzi iliyotekelezwa ni 4,539 yenye thamani ya Tsh 8.5 Trilioni na miradi iliyotekelezwa na wakandarasi wa ndani ilikuwa 4,404 yenye thamani ya Tsh 3.6 Trillioni.

“Kwa uhakika tumepiga hatua kubwa sana na miradi iliyotekelezwa na wakandarasi wa kigeni ilikuwa ni 135 yenye thamani ya Tsh 4.9 Trillioni na ushiriki wa wakandarasi wa ndani ulikuwa ni 97% na thamani ya mradi ni 42.4% na ushiriki wa wakandarasi wan je ulikuwa ni 3% na thamani ya miradi ilikuwa 57.6%,” alifafanua Katibu Mtendaji huyo

idadi ya watanzania kwenye ushiriki wa uwekezaji na biashara hapa nchini umeongezeka na upatikanaji wa ajira unaleta matumaini na  uwekezaji , masoko na kutengeneza bidhaa

Aliongeza kwamba kongamano hilo lilihudhuriwa na washiriki takribani 300 kutoka sekta mbalimbali binafsi , taasisi za umma na wawekezaji wa ndani na nje ya nchini chini wa uratibu wa  Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).

Na katika kongamano hilo baadhi ya makampuni ya ndani na nje yalipata tuzo ya kutambua mchango wao na kufanikiwa kwa kutekeleza kwa vitendo dhana ya ushiriki wa watanzania kwenye uwekezaji na uchumi (Local Content)

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.