Tanga
Baraza la Uwezehaji Wananchi Kiuchumi {NEEC} limewashauri viongozi wa Mkoa wa Tanga kuunga mkono program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia {IMASA} ambayo inalenga kuyafanya makundi ya kinamama, vijana na makundi maalum kushiriki katika uchumi wa nchi yao.
Ushauri huo ulitolewa na Mshauri wa Rais Masuala ya wanawake wakati a uzinduzi wa program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia {IMASA} ambayo inatekelezwa na Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi {NEEC) kuwa viongozi wanahitajika kuunga mkono program hiyo ambayo inalenga kuyakomboa makundi hayo kiuchumi.
“Kuunga mkono program hii ni kuyapati kazi makundi haya katika fursa zinazopatikana serikali na kuyaonesha fursa zilizopo katika mkoa huo,” na aliongeza kusema kuwa kwa kufanya hiyo makundi hayo yanaweza kuw sehemu ya uchumi wa nchi yao.
Akifafanua zaidi, Bi, Njema alisema kunakazi za kufanyia marekebisho barabara, wapatiwe makundi hayo pamoja na shughuli za kulisha mikutano na makongamano na fursa mbalimbali wapatiwe wafanye wapate fedha.
Alisema kwa sasa programa hiyo ipo katika hatua ya kuyasajili makundi na kuyaingiza katika kanzidata na badaye yaweze kupata uwezeshaji na kuanzisha au kuendeleza shghuli za kiuchumi za kilimo, kuongeza thamani mazao, kufuga kuku na shughuli nyingine.
Pia alisema program hiyo inahitaji kuona makundi hayo yanatumia fursa ya kumiliki biashara kubwa hata kumiliki hotel kubwa na kusema mapinduzi ya uchumi yanaanza katika mkoa na katika nchi hivyo kunahitaji mshikamano katika utelezaji.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Batilda Burian alisema wamjipanga kuhakikisha makundi hayo kule yaliko katika kata, mitaa na vijiji yananufaika na program hiyo kwa vile inalenga kuwakwamua kuondokana na hali duni ya vipato.
“ Kazi ya kusajili itaendele katika kata, mitaa na vijiji ili kila makundi haya yasajiliwe na kupata fursa katika program ya IMASA,” na aliongeza kusema mkoa wake utaongoza kwa vile wamejenga utayari na kufanya kazi kwa bidii.
Alisema mkoa unafursa nyingi watahkikisha makundi hayo yanazitumia kuanzisha biashara ili waweze kupiga hatua kivipatoa kukidhi mahitaji ya familia zao.
Bi. Nifa Hassan alisema program hiyo imempa mafunzo y ujasiriamali na inalenga kuwapatia uwezeshaji kutunisha mitaji yao ambayo ni midogo na hiyo itasaidia kuondoa adha ya upatakanaji wa mikopo.
“Natamani kuwa mfanyabiashara mkubwa na hii program ndiyo itakayoniwezesha kufikia ndoto zangu za kiuchumi,” na pia alisema programa hiyo ni chombo cha watu wa hali ya chini.
Bw. Kasim Kimeya alisema mafunzo hayo yamemwezesha kujifunza siri za kufanikiwa katika shughuli za kijasirimali hivyo anawataka vijana wenzake kuitafuta program hiyo waweze kuinufaika nayo.
“Program hii ni ukombozi kwa wafanyabiashara wadogo na haimwachi mwananchi wengi tutaingia humo ambapo dhamira yake ni kuwakwamua wananchi wa kipato cha chini,” alisema Bw. Kimeya.
Alisema yeye anafanya shughli za ufugaji wa kukua na sasa baada ya mafuno hayo anaenda kuimarisha biashara yake ya ufugaji wa huo ili kupata kipato kizuri kwa familia yake.
Post a Comment