N a Mwandishi Wetu Lindi
Baraza la Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi (NEEC) limewataka viongozi wa Mkoa wa Lindi kutengeneza mkakati
kabambe utakaozuia mimba za utotoni kwa wasichana ambazo zinawasabishia kukatisha
masomo na badaye kushindwa kujishughulisha na shughuli za kiuchumi kutimiza
ndoto zao.
Kauli hiyo ilitolewa na Katibu
Mtendaji wa baraza hilo, Bi. Beng’i Issa wakati baraza hilo lilipozindua programa ya Imarisha Uchumi na Mama Samia
(IMASA)mkoani humo kuwa kunahitajika kuweka
mkakati wa kuzuia mimba za utotoni ili wasichana waweze kutimiza ndoto zao za
kiuchumi baada ya kuhitimu masomo yao.
“Mkoa huu unamatatizo ya
wasichana kuacha masomo hata wakiwa wamefaulu kujiunga na shule za sekondari
hawaendi na inakadiliwa asilimia 30 hukatisha masomo kutokana na mimba za
utotoni,” mimba za utotoni zinakatisha ndoto za kiuchumi za wasichana.
Alisema program ya IMASA imekuja
kuwezesha Makundi ya kinamama, vijana na makundi maalum hivyo makundi ya vijana
yakipata elimu ni nyenzo kubwa ya
kufikia malengo yao ya kiuchumi na ukizingatia mkoa huo unfursa nyingi za
kiucumi.
Bi. Beng’i alisema mkoa huo wananchi
wanajishughulisha na kilimo cha korosho,alzeti,uvuvi, mazao ya mwani, hivyo programa
hiyo itashirikiana na mkoa huo kuweka vipaumbele ili kuandaa programa kwa ajili
ya uwezeshaji wake.
Alisema program ilipokelewa vizuri mkoani humo na wananchi walitamani sana
program ianze haraka na washiriki wengi walikuwa ni wafanya biashara, wakulima
, wakulima wa kuongeza thamani mazao na madalali wa kilimo.
Pia aliutaka mkoa huo kuendelea
na program zao za kawaida katika kilimo cha korosho, ubanguaji korosho kuongeza
thamani mazao na uvuvi na zile za uwezeshaji za asilimia kumi na
kuendelea kufuata maelekezo ya serikali.
Katibu wa Shirikisho la Watu Wenye
Ulemavu Manispaa ya Lindi, Bi.Zuhura Meza alisema anamshukuru Rais mama samia
kuanzisha program hiyo ambayo imekuja kuwainua kiuchumi wanawake kupitia
mafunzo ya ujasirimali na uwezeshaji watakao pewa.
“Nikilirudi nyummbani naenda
kuwaelimisha watu wenye ulemavu wale ambao hawajajisajili na program ili nao waende
kujishajili kupata fursa ya mafunzo na uwezeshaji,” alidai fursa hii imekuja
kuwakomboa watu wenye ulemavu.
Naye Mkulima wa Mwani kutoka kata
ya Lindi Mjini ya Kitumbi Kwela Manispaa Lindi, Rukia Selemen alisema yeye ni
mkulima na mchakataji wa bidhaa za mwani anashukuru ujio wa program hiyo kufika katika
manispa yao kutoa elimu ya ujasirimali na itamwezesha kufanya
vizuri zaidi.
Mjasilimali toka Kilwa Masoko Bi.
Fatuma Juma alisema anajishughuli na usindikaji wa mzao mbalimbali yakiwemo ya
maziwayogati, juice ya mwani na anatengeneza bidhaa za urembo kama nguo na
alidai kwa kusema kuwa program hiyo imewaingiza katika mfumo na kufanya kazi
kwa ubora,
“Program hii imetupatia elimu ya ujasairimali na pia inalenga kutupatia uwezeshaji,” na alisema wao wamejipanga kupokea uwezshaji huo ili waweze kukuza mitaji yao pamoja na biashara na ujasiriamali.
Post a Comment