Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Bank of Africa Tanzania Limited
imewahikisha wafanyabiashara wadogo wadogo na wa kati kwamba itaendelea kutoa
mafunzo kuhusu matumizi ya fedha, kuweka kumbukumbu za biashara na elimu ya
kodi kwa wateja wake ili kuhakikisha wanakua pamoja.
Akizungumza na waandishi wa Habari hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bi Esther Cecil Maruma alisema kwamba warsha hiyo yenye kauli mbiu “TUKUE PAMOJA” ilikuwa ni ahadi ya benki hiyo kutoa huduma na msaada kwa wafanyabishara wadogo na wa kati (SME) nchini.
Mkurugenzi Mtendaji huyo Aliongeza kwamba katika kufanikisha ukuaji wa kifedha na uthabiti wa biashara zao. Warsha hiyo ililenga kutoa elimu ya kifedha kwa kina, ambapo mada kama vile uwasilishaji wa rekodi za biashara, masuala ya kodi, na mikakati ya kuongeza uwezo wa huduma za kibenki ili kuchochea ukuaji wa mtaji zilijadiliwa kwa nia ya kuwainua wafanyabiashara
Baadhi ya wafanyabiashara wadogo wadogo na wa kati wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa kwao kwenye programu ya “TUKUE PAMOJA” iliyoandaliwa na BANK OF AFRICA hivi karibuni jijini Dar es Salaam"Katika mipango wetu wa kimkakati ya miaka mitatu, sekta hii nyeti ya wajasiriamali imepewa kipaumbele kwa njia ya kipekee, ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya kifedha kwa wateja wetu. Takwimu zinaonyesha kuwa sekta hii inachangia karibu asilimia 30 ya mapato ya taifa na katika biashara 10, 9 ni biashara zinazomilikiwa na wafanyabiashara wadogo wadogo na wa kati (SME), hivyo ni muhimu kuhakikisha tunawajengea uwezo,”
Aliogeza “Tangu tulipoanza rasmi programu
hizi mnamo mwaka 2021, benki tayari imefikia wateja 500 wafanyabiashara wadogo
wadogo (SME) na lengo la mwaka huu ni kufikia wateja 170. Matunda ya kile
tunachofanya yanaonyeshwa katika matokeo mazuri tunayoshuhudia, ambapo faida ya
benki imeongezeka kwa asilimia 33 kutoka Tsh 6.03 Bilioni hadi Tsh 9 Bilioni,
kwa kulinganisha matokeo ya Juni mwaka jana na Juni mwaka huu." alisema
Bi. Maruma.
Mkurugenzi Mtendaji huyo wa benki hiyo
alifafanua kwamba "benki pia imeweza kupata matokeo mazuri katika mikopo
chechefu, na katika kipindi kilichofikia Juni benki imefikia asilimia 1.5 ya
mikopo chechefu, hii ni chini ya kiwango kinachohitajika na Benki Kuu ya
Tanzania cha asilimia 5." Matokeo haya yanatuambia kuwa wateja wetu ni
wazuri na wanalipa mikopo yao vizuri."
"Ningependa kutoa shukrani zangu za
dhati kwa wateja wetu wote wa Bank of Africa Tanzania kwa kuendelea kutuunga
mkono na pia naomba kwa wajasiriamali wa Tanzania, hasa wafanyabiashara wadogo
wadogo na wa kati ((SME); kwamba benki iko tayari kuhakikisha mafanikio yao,
kama kauli mbiu ya programu yetu "TUKUE PAMOJA" benki ina azma ya
kuendelea kuwekeza katika sekta hii. Hii inaelezewa kwa uwazi katika mpango wa
kimkakati wa miaka mitatu wa benki yetu, ukiwa na bajeti ya Tsh 62.23 Bilioni iliyopangwa
kwa sekta ya wafanyabiashara wadogo wadogo na wa kati (SME) pekee kwa mwaka
2022-2024, na kwa kipindi cha mwaka jana tumetoa mikopo ya takriban Tsh 47.87
bilioni, huku zaidi ya Tsh 20.67 bilioni tayari zikiwa zimekopeshwa mwaka huu
hadi Juni, zikifaidisha zaidi ya wateja 16,000 wa SME." alisema Bi. Maruma
Kaimu Mkuu wa Huduma za Kibenki kwa wateja
wa Binafsi na Reja Reja, Bi. Mwamvua Majeshi aliwahakikishia wafanyabiashara
kwamba huduma za mikopo zitapewa kwa wakati bila kuchelewa kulingana na kanuni
za kbenki hapa nchini.
“Kwa Bank of Africa, wateja wetu
kuhudumiwa kupitia matawi yetu, hata hivyo, benki pia imewekeza katika huduma
za kidijitali kama vile huduma za benki kwa simu (B-Mobile), huduma za benki za
mtandao (BOAWeb-Internet Banking) na hivi karibuni tumezindua huduma ya Bank of
Africa WAKALA yenye mawakala zaidi ya 200 nchini.” alisema Bi. Majeshi.
Kwa upande wao , mfanyabiashara , Bw Frank
Chaula aliyehudhuria programu hiyo aliipongeza BANK OF AFRICA kwa jinsi ilivyo
wawezesha kupitia mikopo na kuinua biashara zao na kuomba benki iendelee
kuboresha huduma zake ili kufaidisha Watanzania wengi zaidi.
“Tunashukuru BANK OF AFRICA kwa semina hii
muhimu na leo nimejifunza nidhamu ya matumizi ya fedha , kuweka kumbukumbu,
mauzo na manunuzi kwenye biashara kwa kweli nimepanua uelewa kwenye biashara
nawashukuru sana,” alisema Bw Chaula
Naye, Elia Komba ambaye ni msafirishaji
alisema kwamba mafunzo waliyopata kuhusu biashara na elimu ya mambo ya kodi
yatawasaidia katika kufanya biashara zao kwa kushirikiana na Mamlaka Kodi
Tanzania (TRA) jinsi ya kuweka hesabu vizuri ili kuongeza tija kwenye biashara
zao.
Naye mwezeshaji kwenye semina hiyo ya siku
moja , Bw Eric Crispin alisisitiza muhimu wa kuwa na nidhamu kwenye matumizi ya
fedha kwenye biashara zao za kila siku ili kuweza kukua kibiashara.
“ni muhimu kuwa na nidhamu kwenye matumizi
ya fedha na kuwa na utaratibu wa kuwa na kuweka malengo na bajeti kwa kila
matumizi yako ya kila siku na kuweka mifumo ya kutunza kumbukumbuku ya fedha,”
aliongeza.
Post a Comment