...Waahidi kuendelea kutoa huduma bora, viwango vya kimataifa
....Kwenye gesi waunga mkono juhudi za Dkt Samia suluhu hassan nishati safi, mazingira
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam,
Kampuni ya mafuta ya Total Energies imefungua wiki ya huduma kwa wateja kwa kutoa ahadi ya kuendelea kutoa huduma bora ya mafuta yenye viwango vya juu, vilainishi vya injini na vifaa vya magari kwa viwango vya kimataifa, Makangale Satellite inaripoti.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kwenye uzinduzi wa kituo cha mafuta cha makanya magomeni jijini Dar es Salaam, Total Energies, Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano , Getrude Mbakile alisema kwamba kampuni hiyo imejipanga kuendelea kutoa huduma kwa wateja wake vya viwango vya kimataifa.
“Tunawashukuru sana wateja wetu kwa kuendelea kutuamini na kutupa ushirikiano wa kutosha kwenye sekta hii muhimu ya usafirishaji , magari, vifaa na vipuri vya vyombo vya moto sie tutaendelea kutoa vifaa na vilainishi vya mafuta kwa ajili ya magari yao kwa uaminifu mkubwa, aiongeza Bi Mbakile kwa msititizo
Aliongeza kwamba kwa kufungua kituo cha mafuta eneo la magomeni , makanya jijini ni juhudi za makusudi za kampuni hiyo kuleta huduma zao karibu na wateja wao ili waweze kupata huduma zote kwa urahisi zaidi na za uhakika.
“Kituo hiki kimezinduliwa rasmi leo lakini kina miezi mitatu tu tangu kianze kufanya kazi na mwitikio wa wateja wetu ni mkubwa mno kutoka na huduma zinazotolewa hapa ni za viwango vikubwa , alisema Bi Mbakile.
Naye, Mkurugenzi wa kampuni ya Arasco Energies, ambao ni wakala mkubwa wa Total energies, Bw Thabit Ameir alisema kwamba kampuni hiyo Total energies imefungua kituo hicho kipya katika juhudi za kuwaletea wateja wao karibu na huduma zao za mafuta na vilainishi mbalimbali vya mafuta kwenye magari, pikipiki na vyombo vingine vya moto.
“Tutaendelea kutoa huduma bora kabisa zenye viwango vinavyokubalika duniani na kusherekea wiki ya huduma kwa wateja tumeamua kufungua kituo hiki hapa magomeni makanya ili kusogeza huduma hizi karibu na watanzania,” alisema Bw Ameir
Kwa upande , Afisa Masoko wa kampuni hiyo anashughulikia gesi , Bw Allan Ngogolo alisema kwamba kwa upande wa gesi kampuni hiyo itaendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita , chini Dkt Samia Suluhu Hassan kuhusu nishati safi ya kupikia ya gesi na kutunza mazingira.
“Tunatoa wito kwa mawakala wakubwa na wadogo waje kufanya biashara na sisi si tu mafuta hata gesi na kuhakikisha kwamba huduma hii ya nishati safi inaendelea kusambazaa hadi maeneo ya pembezoni , mikoani na vijini nchini kote,” alifafanua.
Ngogolo aliongeza kwamba nia ya kampui na kuona watanzania wengi hasa wa vijini wanaanza kutumia nishati za safi kwa ajili ya kupikia na kuondokana na matumizi ya mkaa na kuni ambao unasababisha uchafu wa mazingira.
Mwisho
Post a Comment