VYOMBO VYA HABARI

Kuendesha gari katika msimu huu wa sikukuu
 Image result for uber taxi
Uber huendesha modeli fanisi inayoitwa bei hai, ambayo huwawezesha watumiaji kupata gari wakati wanaihitaji sana - hasa wakati wa siku za mwaka zenye shughuli nyingi, kama vile Siku ya Kuamkia Mwaka Mpya au baada ya hafla kubwa ya michezo

DAR ES SALAAM, Tanzania, Desemba 13, 2016/ -- Msimu wa sikukuu ukianza nchini Tanzania, tunakabiliana na changamoto ya mwaka: tutawezaje kufika nyumbani sikukuu zikiisha? Ijapokuwa ni rahisi sana kuwajibika, watu wengi bado huendesha magari wakiwa wamelewa. Tumeshughulikia mambo msingi ya kusafiri katika msimu huu wa sikukuu, ili daima uweze kufanya maamuzi salama.  

Panga mapema
Je, unafikiria kinywaji chako cha baada ya kazini kinaweza kujumuisha glasi nyingine zaidi kuliko ulivyotarajia? Panga mapema na utumie Uber (www.Uber.com) kwenda kazini. Unaweza hata kupanga safari yako mapema ili usiwe na wasiwasi kuhusu kutatiza sikukuu zako hadi dereva wako awasili. Au, kama sherehe itakupata kwa ghafla, tumia Uber kwenda nyumbani, acha gari lako ofisini na ulichukue wikendi. Wakati hatua hii inaweza kuonekana kama kazi ya ziada mara ya kwanza, ni bei nafuu ikilinganishwa na kuhatarisha usalama wako na usalama wa wengine kwa kunywa na kuendesha gari.

Jua kuwa utapata dereva, hata wakati kuna shughuli nyingi
Katika misimu ya likizo, mara kwa mara kuna wasiwasi kuwa hakutakuwa na madereva wa kutosha. Hiyo si uongo lakini kwa kuwa jukwaa la Uber linaendelea kukua na kubadilika, Uber huendesha modeli fanisi inayoitwa bei hai, ambayo huwawezesha watumiaji kupata gari wakati wanaihitaji sana - hasa wakati wa siku za mwaka zenye shughuli nyingi, kama vile Siku ya Kuamkia Mwaka Mpya au baada ya hafla kubwa ya michezo.

Wakati kuna mahitaji mengi, ni muhimu kuwa kuna madereva wa kutosha kwenye jukwaa hili ili kuwahudumia wale wanaotafuta gari. Kwa sababu hii, Uber huongeza nauli ili kuwahimiza madereva zaidi kuja kwenye jukwaa hili.

Hesabu ya bei hai huongeza bei kiotomatiki ili kuwahimiza madereva zaidi kuja kwenye jukwaa hili na kushughulikia mahitaji haya. Wakati mahitaji na ugavi umesawazishwa, bei hurejea kawaida kwa haraka. Utajua wakati bei hai inatumika, kwa sababu utaarifiwa kuanzia wakati unapofungua app, na kukumbushwa unapokuwa ukiomba safari yako. Bei hai uhakikisha kuna magari yanayopatikana wakati wowote unapofungua app hiyo.

Vipengele vya usalama
Tumejitolea kwa usalama na tunataka kila mmoja kuwa na imani kuwa Uber ni chaguo thabiti msimu huu wa sikukuu.Teknolojia yetu huifanya iwe rahisi kufanya maboresho ya usalama ambayo hayakuwa hapo awali kabla ya Uber. Wakati dereva anapokubali ombi lako, unaweza kuona jina lake la kwanza, picha, na nambari ya leseni ya gari. Magari yote hufuatiliwa kwa kutumia GPS na unaweza kushiriki Muda Unaokadiria Kuwasili hivyo kuwawezesha wapendwa wako kuona safari yako kwa wakati halisi (hata kama hawana app ya Uber).

Pesa ziko salama
Je, huna kadi? Hakuna shida! Unaweza bado kusafiri na sisi na ulipe kwa pesa taslimu. Chagua tu chaguo la PESA TASLIMU, safiri na ulipe nauli moja kwa moja kwa dereva wako mwisho wa safari. Safari zote za Uber zinafuatiliwa kwa kutumia GPS na tunajua eneo lako katika kila safari ili kuhakikisha usalama wa wahusika wote. Tumewahimiza pia kuweka pesa kwenye benki mara kwa mara na kubakia na hela kidogo kama iwezekanavyo (pesa za kulipia mafuta na kununua bidhaa). Hadi sasa hatujaona ongezeko lolote la uhalifu katika nchi zinazoendesha chaguo za malipo ya pesa taslimu.

Je, unahitaji msaada? Tuko hapa kila wakati kwa ajili yako
Tunajua kwamba kuna wakati unahitaji kuwasiliana: pochi ilisalia ndani ya gari, au pengine nauli si sahihi. Sasa, kuwasiliana ni rahisi kama kutumia jukwaa letu. Tumeunda mtandao mkubwa wa vituo vya usaidizi ili kutoa usaidizi 24/7. Kitendaji chetu cha Msaada ambacho ni rahisi kutumia ndani ya app hujibu maswali yako yote. Bofya tu "Msaada" na maelezo yote unayohitaji yako hapo.

Furahia, bila kuwa na wasiwasi kuhusu safari yako
Licha ya haya yote, msimu wa likizo ni wakati wa kuwa bila mawazo. Unahusu kushughulikia mambo machache ili uweze kufurahia. Kwa kunufaika na chaguo za kushiriki gari, hustahili kuwa na wasiwasi kuhusu kuegesha gari, kumpa dereva bakshishi (madereva wetu hubaki na kiasi kikubwa cha nauli), 'kuzidisha kikomo' au jinsi utakavyofika nyumbani. Wakati huduma hii inafurahisha, rahisi, na inapatikana hivi, hakuna sababu ya kutochagua kuwajibika.   
Kusambazwa na APO kwa niaba ya Uber.

Kwa maelezo zaidi:
Samantha Allenberg
Uber Communications Africa
Tel: +27 82 453 7495
Email: Samantha.Allenberg@Uber.com

Jessica Gois - Jenni Newman
Public Relations (Uber South Africa - PR Agency)
Tel: + 27 (0) 82 777 5427
Email: Jessica@JNPR.co.za 
Mitandao ya Kijamii:
Twitter: @UberNigeria | Facebook: /UberNigeria | Instagram: @UberNigeria

Kuhusu Uber:
Lengo mahususi la Uber ni kusaidia watu kupata usafiri kwa kubonyeza kitufe tu – mahali popote na kwa kila mtu. Tulianza mwaka 2009 kwa kutatua tatizo dogo – ni kwa jinsi gani unaweza kupata usafiri kwa kubonyeza kitufe? Baada ya miaka sita na zaidi ya bilioni ya safari fupi, tumeanza kutatua hata matatizo makubwa: kupunguza mrundikano na uchafuzi wa mazingira katika miji yetu kwa kubeba watu wengi kwa kutumia magari machache.
Mtandao wa Uber kwa sasa unapatika kwenye nchi zaidi ya 75 ndani ya mabara 6 na zaidi ya miji 475. Kuomba usafiri, watumiaji wanapaswa kupakua app (ni bure) kwa ajili ya Android, iPhone, Blackberry 7, au kujiunga kupitia tovuti ya www.Uber.com/go. Kwa taarifa zaidi na maswali tembelea tovuti yetu: www.Uber.com.
CHANZO
Uber
Maudhui multimedia
Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.