KUFUNGULIWA KWA MFUMO WA PAMOJA WA UDAHILI KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017
Baraza la Taifa la Elimu ya
Ufundi (NACTE), linapenda kuutangazia Umma na wadau wote wa Elimu nchini, kuwa
mfumo wa Udahili wa pamoja yani Online Central Admission System (CAS),
umefunguliwa rasmi tarehe 4 Machi, 2016, saa 6 mchana, kwa kupokea maombi ya
mwombaji katika kozi mbalimbali, ikiwemo ngazi ya, Astashahada, Stashahada na
Shahada kwa mwaka wa masomo 2016/17. Mfumo utajumuisha kozi zifuatazo;
1. Astashahada na Stashahada
2. Shahada za Elimu ya Juu
Mwombaji wa Astashahada na
Stashahada anaweza kuomba kwa ajili ya eneo moja au zaidi katika maeneo ya
taaluma yafuatayo;
1. Biashara na Utalii, mfano; Uhasibu, Meneja rasilimali
watu, Wanyama pori, Mipango.
2. Sayansi shirikishi, mfano; Kilimo, Uhandisi, Mifumo ya
mawasiliano, Usanifu majengo, Mifugo.
3. Afya, mfano; Uganga, Maabara, Ufamasia, Uuguzi
Ada ya maombi ni kama ifuatavyo;
1. Kwa eneo la Afya ada ya maombi ni Tshs 30,000/=.
2. Kwa eneo moja kati ya maeneo mengine yaliyobaki, ada ni
Tshs 20,000/=
3. Kwa zaidi ya eneo moja la taaluma, mfano; Afya pamoja na
Ualimu, ada ni Tshs 30,000/=, muombaji anaruhusiwa kuchagua maeneo yote.
4. Kwa waombaji wa Shahada za Elimu ya juu, ada ya maombi ni
Tshs 50,000/=
Mwisho wa kutuma maombi haya ni tarehe 31/05/2016.
Bonyeza hapa kufanya maombi
Imetolewa na:
Baraza la Taifa la Elimu yaUfundi, 4 Machi, 2016
Source: http://nacte.go.tz/