NAIBU SPIKA WA BUNGE ATINGA KWENYE SHOW YA LADY JAY DEE MJINI DODOMA
Mwanamuziki Nyota wa Kike nchini Judith Wambura a.k.a Lady Jay Dee anayetamba na kibao chake cha #NdiNdiNdi amefanya onyesho alilolipa jina la #NaamkaTenaTour katika viwanja vya Royal Village, onyesho lililohudhuriwa na watu na watu mbalimbali akiwemo Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, Waheshimiwa Wabunge, Mkuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez pamoja mashabiki wake mkoani Dodoma.
Mratibu wa show ya Lady Jay Dee ya Naamka Tena Tour ya mjini Dodoma, Mh. Catherine Magige akizungumza machache na kutambua uwepo wa Naibu Spika wa Bunge na waheshimiwa wabunge wenzake katika viwanja vya Royal Village mjini humo.
Malkia wa Bongo Flava, Lady Jay Dee katika ubora wake.
Mwanamuziki Lady Jay Dee na The Band wakitoa burudani kwa wakazi wa Dodoma na vitongoji vyake katika harakati za kuwafikia mashabiki wake wote nchini nzima kwa show aliyoi' brand' kama Naamka Tena Tour.
Mkali wa R & B kwenye Band ya Lady Jay Dee, John Music akitoa burudani kwa wakazi wa Dodoma.
Vijana watanashati wa bendi Lady Jay Dee wakitoa burudani kwa mashabiki wa Dodoma.
Hoyce Temu, Esther Bulaya, Shyrose Bhanji na Hamisi Kigwangalla wakipiga shwangwe kwa Lady Jay Dee alipokuwa jukwaani.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson kwenye viwanja vya Royal Village ilipofanyika show ya mwanamuziki Lady Jay Dee mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Alvaro Rodriguez (kulia) akiteta jambo na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Mh. Shyrose Bhanji kwenye show ya Lady Jay Dee iliyofanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
Mh. Esther Bulaya akiserebuka na Hoyce Temu katika show ya Lady Jay Dee iliyofanyika mwishoni mwa juma mjini Dodoma.
Mh. Halima Mdee, Mh. Catherine Magige, Mh. Esther Bulaya pamoja na Hoyce Temu wakiserebuka.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Alvaro Rodriguez akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Kawe, Mh. Halima Mdee walipokutana kwenye show ya Lady Jay Dee.
Mwanamuziki Lady Jay Dee na Band yake wakishambulia jukwaa.
Mashabiki wa Lady Jay Dee wakiserebuka kwa raha zao.
Pichani juu na chini ni Umati wa wakazi wa mjini Dodoma eneo la VIP wakiwemo waheshemiwa wabunge wakisakata muziki wa Lady Jay Dee.
Upendo waliounyesha watu wa Dodoma kwa mwanamuziki Lady Jay Dee.
Mh. Halima Mdee akipata Ukodak na wananchi wa Dodoma wanaomkubali. PICHA ZAIDI INGIA HAPA