Ni kinyume cha sheria kumuweka mtu ndani kwa zaidi ya masaa 24
KITENDO cha jeshi la polisi kuwaweka ndani mahabusu zaidi ya saa 24
bila kuwapeleka mahakamani au kuwapa dhamana ni ukiukwaji wa sheria na uvunjifu
wa ,katiba ya nchi.
LSF Chief Executive
Officer, Kees speaking at the official
launching of the national paralegal forum held in Dodoma yesterday.
|
Hayo yalisemwana jana hapa Dodoma na Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge
ya katiba na sheria, Mohamed Mchemgerwa alipokuwa akifungua kongamano la siku
mbili la kitaifa la msaada wa kisheria kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na
visiwani.
“Ni kinyume cha sheria kuweka watu ndani zaidi ya muda uliwekwa kisheria.
Lakini watanzania wengi hawajua hili…hii inatokana na uelewa finyu wa naswala
ya kisheria,” alisema Mchemgerwa, wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo
liloandaliwa na Shirika la Legal Services Facility (LSF).
Alisema wapo watu ambao wanakutana na matatizo mbalimbali pamoja na kuwekwa
ndani bila ya makosa kutokana na kutokujua sheria.
Mchengerwa alisema watu wengi hawajui kama kuna dhamana ya polisi ambapo
mtuhumiwa hatakiwi kukaa mahabusu zaidi ya saa 24 bila kupelekwa mahakamani au
kupewa dhamana.
Katika kongamano hilo,Mchengerwa
alisema watoa msaada wa kisheria wanatakiwa kutoa msaada huo katika kila wilaya
hususani maeneo ya mjini na vijijini.
"Wapo watu ambao wako gerezani na hawana kosa lakini kutokana na tatizo
la uelewa mdogo wa kisheria wamekuwa wakifungwa.
"Jamii bado haijui kama kuna dhamana ya polisi pia ni kosa la kisheria
kumweka mahabusu mtuhumiwa zaidi ya saa24 bila kumpeleka mahakamani au kumpatia
dhamana"alieleza.
Aliwataja wasaidizi wa kisheria kama nguzo muhimu ya kuwasaidia kuelemisha
watanzania kuhusu maswala haya ya kisheria na jinsi ya kupata haki zao pindi
wanapopatwa na matatizo mbalimbali ya kisheria.
Kwa upande wake mmoja wa watoa msaada wa kisheria kutoka Zanzibar, Abdullkarim
Saidi alisema licha ya kazi kubwa wanayofanya ya kutoa msaada wa kisheria,
wasaidizi wa kisheria nchini bado wanakabiliwa na changamoto nyingi.
Alisema changamoto hizo ni pamoja na kukosekana kwa usafiri pamoja na fedha
za kuendesha shughuli zao kwa ufanisi, na kuongeza kuwa “tunafanya kazi katika
mazingira ambayo si rafiki kutokana na kutembea kwa umbali mrefu.”
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa LSF Bw. Kees Groenendijk
amesema shirika lake limeweka mikakati madhubuti ya kuwasaidiza wasaidizi wa
kisheria waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi, ikiwa ni pamoja na
kuwawezesha kifedha na kitaaluma ili waweze kuwasaidia na kuwafikia watanzania
wengi zaidi wenye matatizo mbalimbali ya kisheria.
Kwa mujibu wa Kees, mpaka sasa shirika la LSF limeshatoa
zaidi ya shilingi billion 20 kwa mashirika mbalimbali yanajishughulisha na
utoaji wa huduma za kisheria—lengo kuu likiwa ni kuwasaidia watanzania kupata
haki zao.
Participants to the
paralegal forum following proceedings of the meeting
|
Chairman of the
Parliamentary Committee on Constitution and Legal Affairs, Mr. Mohamed Omary Mchengerwa,
speaking at the opening of a national paralegal forum held in Dodoma
|
Zanzibar paralegal,
Abdulkarim Mussa Said, reading a speech on behalf of paralegals at a forum held
in Dodoma
|