Shirika la kisheria lisilo la kiserikali la Legal Services Facility (LSF) wiki hii litatoa msaada wa komputa 176 zenye thamani ya shilingi million 146 kwa ajili ya vituo 160 vya wasaidizi wa kisheria vilivyoko mikoani—kama sehemu ya mkakati wake wa kuongeza ufanisi na kuboresha utoaji wa huduma za kisheria nchini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari hivi karibuni, komputa hizo zitatolewa wakati wa warsha (itakayofanyika Ijumaa hii Dar es Salaam) kwa viongozi wa mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotoa msaada wa sheria na yanayofadhiliwa na LSF—kutekeleza miradi ya wasaidizi wa kisheria nchini.

Bw Kees Groenendijk, Meneja wa LSF, alisema komputa ni zana muhimu kwa vituo vya wasaidizi wa kisheria na wasaidizi wa kisheria wenyewe wanaotoa msaada wa kisheria nchini. Tangu kuanzishwa kwake miaka mitano iliyopita, LSF imekwishatoa ufadhili wa mabilioni ya fedha, ambazo, pamoja na mambo mengine, zimerahisisha kuanzishwa kwa vituo vya wasaidizi wa kisheria sehemu mbalimbali nchini.
Image result for legal services facility tanzania-Kees Groenendijk,
Mkurugenzi wa Shirika la Legal Services Facility (LSF), Bwana. Kees Groenendijk akizungumza  leo Jijini Dar es Salaam

“Ni ukweli usiopingika kwamba wasaidizi wa kisheria wamekuwa wakifanya vizuri sana linapokuja suala la kuwasaidia wanaohitaji msaada wa kisheria hasa vijijini. Ndiyo maana tumeamua kutoa hizi zana, ambazo naamini vitaongeza ufanisi wa huduma za kisheria. Naamini zitaongeza ufanisi na utendaji wa wasaidizi wa kisheria na vituo vya wasaidizi wa kisheria,” alisema Bw Groenendijk.

Komputa zitatolewa kwa mashirika yasiyo ya kiserikali 27 yanayotoa msaada wa sheria, ambayo ndiyo yatakayotoa hizo komputa kwa vituo vya wasaidizi wa kisheria katika maeneo yao ya kazi. Mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotoa msaada wa sheria yametoa mchango mkubwa sana katika uanzishwaji wa vituo vya wasaidizi wa kisheria kupitia ufadhili wa LSF.

Kwa mujibu wa taarifa ya LSF, warsha inayofanyika wiki hii itatoa nafasi kwa washiriki kujadili mambo mbalimbali na changamoto zake katika kutekeleza miradi inayofadhiliwa na LSF na kupata suluhisho.

Pamoja na hayo, warsha hiyo itawezesha LSF kuelezea njia mkakati yake ya 2016-2021, nini LSF inataka kupata na matokeo yake kwa mashirika yasiyo ya kisherikali yanayotoa ushauri wa kitaalam (RMOs). Masuala mengine yanahudu namna ya kutatua migongano kati ya malengo ya kitaasisi ya RMOs na malengo mkakati ya LSF na namna ya kuongeza matokeo.

Kutakuwa na majadiliano pia juu ya kuyajengea uwezo mashirika yanayofadhiliwa na LSF/yanayotoa ushauri wa kitaalam, namna ya kujenga uwezo kwa wasaidizi wa kisheria na LSF, umuhimu wa kupima kazi na matokeo yake na kuripoti kwa njia ya mtandao.
Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.