August 2017

Mtindo wa karate mkongwe  duniani, Okinawa Goju Ryu wa chama cha  Jundokan  Tanzania chini ya mwakilishi wake Sensei Rumadha Fundi  mwenye Dan 4,“Yondan” pia mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 38 ya mafunzo ya sanaa ya Karate mtindo wa Goju Ryu chini ya walimu wakuu wengi maarufu toka Okinawa, Japan kama vile Master Mario Higaonna(IOGKF), Master Masataka Muramatsu( Goju Ryu Kyokai), Teruo Chinen( Jundokan International), na hatimae Kancho Yoshihiro Miyazato, mwenyekiti wa (Jundokan So Honbu, Naha, Okinawa)Master Tetsunosuke Yasuda, Master Tsuneo Kinjo na Master Tetsu  Gima.

Tunatarajia kufanya mitihani ya mikanda mieusi miezi ijayo madaraja tofauti kupitia dojo za “ Kaizen dojo” Jamhuri na dojo dada ya Hekalu la Kujilinda Zanaki dojo. Hii ni moja ya jitihada za kusambaza mwenendo huu kwa kina na pia ufundishaji wa mbinu za utumiaji wa tafsiri za “Kata” uijulikanao kama “Bunkai”, au uchambuzi wa matumizi ya mbinu za kujilinda. Mitihani yote itafanywa na sensei Rumadha Fundi chini ya utaratibu wa “Syllabus”  ya Jundokan, Okinawa.

Lengo pia ni kuzungumzia yale yote yaliojiri katika semina kuu ya Jundokan bara la Ulaya chini ya master wake toka jijini Naha, Okinawa mwezi wa Julai 2017. Ufundishaji sahihi wa mfumo huu ni moja ya malengo kuhakikisha tu kwamba wana Jundokan duniani mkote wapo kwenye msimamo mmoja katika uchambuzi na ufanyaji wao wa Kata na matumizi yake.

Pia wakati huohuo, kutakuwa na semina ya wanafunzi wa ngazi za mikanda mieusi wa Jundokan Tanzania ikiwemo na dojo ya Zanaki katika kuwawezesha wanafunzi wake kuuliza na kupata majibu ya matumizi yao ya ufanyaji Kata kama jinsi ipasavyo chini ya chama hicho chenye ufahasa wa mtindo huo unaofuata nyanyo za mafunzo ya Master Chojun Miyagi, mwanzilishi wa mtindo wa Okinawa Goju Ryu.

Hivyo, hii ni moja ya fursa kubwa kwa wana Jundokan kuweza kushiriki semina hii chini ya mwakilishi wa Jundokan Tanzania, ama kamaijulikanavyo “Tanzania Shibu-Cho”, sensei Rumadha Fundi. Sensei Rumadha, amesisitiza kwa niaba ya chama hicho kwamba Kila mwanafunzi wa mkanda mweusi, hana budi kuhudhuria semina za walimu angalau mara moja kila miaka miwili na kupata usahihisho muhimu kimafunzo. Hilo ndio lengo kuu hata kipindi kile kwa mwanzilishi wa Okinawa Goju Ryu Tanzania, marehemu Sensei NC Bomani kufanya ziara za mara kwa mara kwenda huko Naha, Okinawa kupata marekebisho toka kwa magwiji wa Karate duniani na chimbuko lake.

Pia vilevile, Tanzania imepatiwa mwaliko wa kuhudhuria maadhimisho ya miaka 65 tokea kuanzishwa kwa chama cha Jundokan itayofanyika November 2018 mjini Naha, Okinawa, Japan. Chama hicho kilianzishwa na mwanafunzi mkuu wa Master Miyagi aitwae Master Eiichi Miyazato sensei 1957 ambae pia alikuwa ndio mwalimu wa sensei Nantambu C Bomani. “ Chuo kinacho fundisha nyayo au mwenendo wa Master Chojun Miyagi”. Ikimaanisha, hamna mabadiliko yeyote kimafunzo na Kata zake kama jinsi alivyokuwa akifundisha mwanzilishi wake Chojun Miyagi sensei.


























































WATAALAMU na wanazuoni wamekubaliana haja ya kupitia mpango wa maendeleo endelevu wa viwanda, SIDP (1996-2020), ili kwenda na wakati kwa kubadili kilimo na kuiweka nchi katika njia bora ya kufikia uchumi wa viwanda. Kauli hiyo imetamkwa kwa namna tofauti na wataalamu hao ambao wamekutana jijini hapa kuangalia uhusiano uliopo kati ya viwanda, mabadiliko ya tabia nchi na kilimo; na ni namna gani sera ya viwanda inaweza kupitiwa upya kuakisi mahusiano haya. Warsha hiyo iliyoandaliwa na ESRF na CUTS International imelenga katika kuelezea umuhimu wa kuangalia mahusiano ya sera ya maendeleo ya viwanda na mabadiliko ya tabia nchi, usalama wa chakula na biashara. 

Wakijadili mada mbalimbali zilizowasilishwa katika semina hiyo iliyofanyika ESRF, wataalam hao walitambua umuhimu wa pekee wa kupitia upya sera hiyo ili iweze kuonesha muunganiko fasaha uliopo kati ya viwanda, kilimo na biashara; na hatua/mikakati ipi iwepo kukinga adhma hii ya viwanda dhidi ya athari za mabadiliko ya tabia nchi. Wamesema kwamba kwa kuunganisha sera ya maendeleo endelevu ya viwanda na uchakataji wa bidhaa za kilimo na kilimo chenyewe kunaleta mwanya wa kuweka msingi imara katika mchakato wa maendeleo na hasa viwanda. Pia, kwa kuwa na sera madhubuti, nchi itaweza kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwekeza katika sekta ya Viwanda, hususani viwanda vinavyotegemea maligafi za sekta ya kilimo.


Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene akitoa neno la ukaribisho kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida wakati wa mkutano wa awamu ya pili ya kuangalia Tabia nchi, Uboreshaji kilimo, na mahusiano yake na biashara kwa jumuiya ya Afrika Mashariki (PACT EAC2), uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 
Katika mkutano huo ilikubalika haja ya kuwa na mikakati ya utetezi kwa kuangalia tafiti zitakazofanywa juu ya kinachojiri katika maendeleo kwa kuzingatia mabadiliko ya tabia nchi, usalama wa chakula na biashara. Zaidi ya yote, pia wadau waliona kuna haja kubwa ya kuwa na tafiti itayoweza kuonesha ni kwa kiasi gani sera ya SIDP (1996-2020) imeweza kuchangia katika ukuaji wa viwanda Tanzania, na changamato zipi imekumbana nazo ambazo zinapaswa kutatuliwa na kuanishwa wakati wa mapitio ya sera hii. Akiwasilisha hoja yake ndugu Solomon Baregu, Mtafiti wa ESRF na Meneja wa Mradi wa PACT EAC 2, amesema kwa kuangalia hali halisi ya sasa ipo haja kwa wataalamu kutambua changamoto zinazojitokeza katika maendeleo endelevu ya viwanda na kukiangalia kilimo kama msingi wa uimarishaji wa viwanda. 

Aidha alisema kwamba kwa kuangalia hali ya sasa ipo haja kubwa ya kubadili kilimo cha Tanzania ili kuboresha maisha ya wananchi na kuimarisha viwanda kwa kuvipatia mali ghafi ya kutosha na yenye ubora. Alisema ni vyema kuelewa uhusiano uliopo katika sera za maendeleo ya viwanda na kilimo ili kuwa na mpango mahsusi wa utetezi kwa lengo la kuimarisha viwanda. Katika mkutano huo washiriki pia walipitia mambo mbalimbali na hatua zinazochukuliwa kupitia sera ya mpango wa maendeleo wa viwanda unaomalizika 2020.


Mkurugenzi Msaidizi wa idara ya Ushirikishaji Kikanda kutioka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bi. Sekela Mwaisela akisoma hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo wakati wa mkutano wa awamu ya pili ya kuangalia Tabia nchi, Uboreshaji kilimo, na mahusiano yake na biashara kwa jumuiya ya Afrika Mashariki (PACT EAC2), uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano ESRF jijini Dar es Salaam.

Miongoni mwa mambo yaliyojitokeza kwenye mazungumzo ya tafiti ni umuhimu wa kuoanisha sera mbalimbali katika kilimo na viwanda kuzihuisha na kuzipa mwelekeo wenye maana kama chachu katika kuimarisha uchumi wa viwanda. Walisema ipo haja ya kuangalia sera hizo ili ziwe msaada katika kuimarisha kilimo na kutoa ushindani kwa viwanda vinavyotegemea bidhaa za kilimo ili kujiimarisha. Aidha katika mazungumzo kwenye mkutano huo imeelezwa kuwa ingawa serikali kupitia wizara zake mbalimbali na Ofisi ya Makamu wa Rais wamechukua hatua kadhaa kuwa na matokeo bora katika utetezi wa bidhaa za viwanda zinazotokana na kilimo, kukosekana kwa uangalizi na utekelezaji wa pamoja kumeleta shida kwa wananchi. Sera ya sasa ya maendeleo endelevu ya viwanda (SIDP) imetengenezwa mwaka 1996 na itaisha 2020 lakini bado ipo haja ya kuweka mahusiano katika utekelezaji wa mpango huo wa maendeleo, kwani kwa mazingira ya sasa hakuna mahusiano na kuna vikumbo katika sera mbalimbali. Wamesema kwamba sera hiyo haitoi mwanya wala mahusiano kati ya viwanda vya kuchakata mazao ya kilimo, mabadiliko ya tabia nchi, biashara na usalama wa chakula.


Mtafiti wa ESRF na Meneja wa Mradi wa PACT EAC 2, Solomon Baregu akiwasilisha namna bora ya kufanya utafiti wenye lengo la kuoanisha mpango wa maendeleo endelevu ya viwanda na mabadiliko ya tabia nchi na kilimo wakati wa mkutano huo wa kuzungumzia mradi wa PACT-EAC2 uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Aidha walisema kwamba mpango wa pili wa maendeleo (2016/17-2020/21) unaonesha haja ya kuweka Tanzania katika njia ya viwanda kwa kuijengea nchi uwezo wa kuzalisha katika kilimo na pia katika ufugaji. Haja ya kubadilisha Kilimo inatokana na ukweli kuwa ni moja ya sekta zinazoingiza kipato cha kigeni kwani inachangia asilimia 29.1 ya pato la taifa, huku ikichangia asilimia 30 ya fedha za kigeni. Aidha ndio chanzo pekee cha uhakika cha biashara ikitoa asilimia 65 ya mahitaji ya viwanda (ghafi) na asilimia 90 ya chakula cha taifa huku ikiajiri asilimia 66.9 ya nguvu kazi ya Taifa. 

Ndugu Peter Lanya, aliekua Makamu Mwenyekiti wa TCCIA, akitoa ufafanuzi zaidi alisema kwamba kunatakiwa mabadiliko katika sera hiyo ili kuupa usasa kwa kuwekeza kwenye mahusiano ya kilimo, mali ghafi kama taifa likitaka kuendelea kuelekea uchumi wa viwanda. Naye ndugu, Joseph Kihaule, Afisa Mkuu wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Raisi, alisema kwamba kuna haja ya kubadilika katika kilimo ili kuweza kufanya vyema huku akisema mazungumzo ya kimataifa ya kupata muafaka, hususani yahusuyo mabadiliko ya tabia nchi, ni muhimu yakaunganishwa na sera mbalimbali ili kuimarisha kilimo na upatikanaji wa chakula.


Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa TCCIA, Peter Lanya akizungumzia SIDP 1996-2020 wakati wa mkutano wa awamu ya pili ya kuangalia Tabia nchi, Uboreshaji kilimo, na mahusiano yake na biashara kwa jumuiya ya Afrika Mashariki (PACT EAC2), uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa idara ya Ushirikishaji Kikanda kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bi. Sekela Mwaisela.

Awali akifungua semina hiyo Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na uwekezaji (viwanda) Adelhelm Meru alishukuru taasisi za ERSF na CUTS International kwa kuona umuhimu wa kuwa na mkutano huo wanne wa kitaifa kuzungumzia mradi wa PACT-EAC. Katika hotuba yake iliyosomwa na Mkurugenzi msaidizi Wizara ya Viwanda Ushirikishaji Kikanda, Bi. Sekela Mwaisela alisema kwamba wizara inatambua haja ya kuweka pamoja viwanda na uchakataji wa mazao ya kilimo kwa kuwa inasaidia kuweka sawa maendeleo ya viwanda. Alisema kwamba kazi iliyofanywa na ESRF inaiweka wizara hiyo katika nafasi bora zaidi ya kufanya mabadiliko ya muhimu kufikia mwaka 2020. Alisema sera hiyo iliyoanza 1996-2020 imepita katika maeneo matatu ambayo yalilenga kuimarisha uwezo wa viwanda (1996-2000), matumizi ya teknolojia (2000-2010) na uimarishaji wa viwanda 2010-2020. Alisema SIDP imesaidia kuimarisha viwanda na sasa lazima kuwepo na uangalizi ili kuwepo na mahusiano mazuri kati ya sera zote zinazotegemewa kuwezesha maendeleo endelevu ya viwanda.


Afisa Mkuu wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira, Joseph Kihaule akichangia maoni katika mkutano huo uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida katika hotuba yake iliyosomwa na Prof. Fortunata Makene amesema ipo haja kubwa ya kuwepo kwa mabadiliko katika SIDP kutokana na mahusiano yake na sekta nyingine hasa yenye uhusiano na kilimo. Katika mkutano huo wa awamu ya pili ya kuangalia Tabia nchi, Uboreshaji kilimo, na mahusiano yake na biashara kwa jumuiya ya Afrika Mashariki (PACT EAC2), Dk Kida alisema kwamba taasisi yake imefurahi kutoa mchango kwa ajili ya kusaidia kuimarisha viwanda nchini. Alisema mkutano huo unaoangalia namna ya kuboresha sera ya viwanda, SIDP (1996-2020), kabla ya utafiti utakaoanza baadae ni muhimu katika kuona kwamba kilimo kinaboreshwa sanjari na SIDP kwa kuweka mahusiano ambayo awali yalikosekana katika sera ya SIDP.


Pichani juu na chini sehemu ya washiriki wakichangia maoni wakati wa mkutano huo uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano ESRF jijini Dar es Salaam.

Alisema kwa taifa la Tanzania ili lisonge mbele ni vyema masuala muhimu katika SIDP yakaangaliwa ili kutekeleza mipango ya maendeleo ya viwanda kwa kuhusisha na uchakataji wa mazao ya kilimo. Aidha alisema katika utafiti utakaosaidia kuboresha SIDP majukumu ya biashara ya kimataifa katika maendeleo ya viwanda na tabia nchi haviwezi kudharaulika. Alisema utafiti utakaofanywa utasaidia kuongeza ‘nyama’ zaidi katika mikakati ya maendeleo kwa kufanya utetezi kwenye mabadiliko ya tabia nchi, biashara na usalama wa chakula kwa kufanya mabadiliko makubwa katika uchakataji bidhaa za kilimo kwa kutambua pia makubaliano ya kimataifa ambayo Tanzania ni mshiriki, hususani UNFCCC na WTO.





Picha juu na chini washiriki kutoka taasisi mbalimbali za serikali na sekta binafsi walioshiriki kwenye mkutano huo.[





Picha ya pamoja ya washiriki.

SHIRIKA la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limekabidhi vifaa vya radio kwa radio za jamii nne vyenye thamani ya mamilioni ya shilingi. Unesco imesema kwamba utoaji wa vifaa hivyo umelenga kuongeza usikivu wa mawimbi ya radio katika maeneo ya vijijini. Shughuli ya kukabidhiana imefanyika Agosti 17 mwaka huu. Akizungumza wakati wakukabidhiana vifaa hivyo Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues alisema kwamba UNESCO inatambua kazi nzuri zinazofanywa na radio hizo za jamii za kuwafikia wananchi wengi zaidi.


Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (kushoto) akizungumza jambo wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya radio jamii iliyofanyika katika ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam.

Aidha alisema ni muhimu sana kwa radio hizo za jamii kujiangalia na kujitunza zenyewe ili wasiingie katika matata na kuchapisha au kutangaza stori baada ya kukamilika kwake. Alisema ipo haja kwa vyombo vya habari kufanyakazi kwa mujibu wa taratibu zao na kuhakikisha kwamba hawachapishi habari ambazo zinahatarisha uwapo wa uandishi unaozingatia maadili. Meneja wa radio ya Jamii ya Baloha FM, Samada Maduhu aliishukuru UNESCO kwa kusaidia kituo chake na kwamba wanatarajia kufikia wilaya tano.


Meneja wa radio ya Jamii ya Baloha FM ya Kahama, Samada Maduhu, akitoa neno la shukrani kwa ofisi za Unesco wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa hivyo yaliyofanyika katika ofisi za Shirika hilo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa mtaalamu wa Mawasiliano Unesco, Nancy Kaizilege Angulo.


Alishukuru UNESCO kwa kuwawezesha kufika katika wilaya tano na kwamba kwa msaada huo wataokoa shilingi laki saba kwa mwezi kuazima transmita. “Radio yetu inawafikia watu 500,000 lakini kwa kupatiwa hivi vifaa tutaweza kufikia watu milioni 1 katika wilaya zaidi ya tano za Kahama, Shinyanga Vijijini, Nyang’wale na Mbogwe mkoani Geita na pia Nzega na Uyui mkoani Tabora ,” alisema meneja huyo .

 Kwa mujibu wa Maduhu, kama wasingelipata transmita hiyo wangelikuwa wanatumia sh milioni 8.4 kwa mwaka.


Ofisa Utawala na Rasilimali Watu wa Radio Jamii ya Pangani FM, Rehema Kilapilo akitoa shukrani kwa uongozi wa Unesco wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa vya redio iliyofanyika katika ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake, Ayubu Kalufya wa radio ya jamii Uvinza alisema kwamba kituo chake kilikuwa kinakodisha transmita kwash laki tano na kufanya kwa mwaka mzima kutumia sh milioni 6. Alisema kwa kupata vifaa hivyo walikuwa wanaachama na ukodishaji huo. Kwa mujibu wa Kalufya, transmita hiyo mpya itawafikisha mbali zaidi katika pwani za Ziwa Tanganyika na hivyo kuleta mabadiliko yanayokusudiwa. Kalufya alisema wananchi wakisikia mambo mbalimbali ya kuwaelimisha na wao wakapata nafasi ya kutoa maneno yao haki za binadamu zitakuwa zimeheshimiwa sana nchini.


Mkurugenzi wa Radio Jamii Uvinza FM, Ayubu Kalufya (kulia) akitoa neno la shukrani kwa hivyo Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (kushoto) wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa vya radio hizo yaliyofanyika kwenye ofisi za shirika hilo jijini Dar es Salaam.

Aliishukuru Unesco kwa kuendelea kuwasaidia na kusema kama si kwa msaada wa UNESCO jamii zilizopo pembezoni zisingepata nafasi ya kutoa madukuduku yao. Radio nyingine zilizonufaika na msaada huo ni Pangani FM. Radio hiyo sasa inaweza kusikika Tanga nzima badala ya Pangani pekee. Katika orodha ya redio zilizopatiwa vifaa ipo pia Mkoani FM ya kutoka Zanzibar.


Picha juu na chini ni Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues na Ofisa Utawala na Rasilimali Watu wa Radio Jamii ya Pangani FM, Rehema Kilapilo wakisaini hati za makabidhiano ya vifaa katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi za UNESCO jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Maofisa kutoka sekta ya mawasiliano UNESCO.





Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akikabidhi hati ya makubaliano na moja kati ya vifaa hivyo kwa Ofisa Utawala na Rasilimali Watu wa Radio Jamii ya Pangani FM, Rehema Kilapilo wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za shirika hilo jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Maofisa kutoka sekta ya mawasiliano Unesco Dar es Salaam.


Picha juu na chini ni Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues na Meneja wa radio ya Jamii ya Baloha FM ya Kahama, Samada Maduhu kwa pamoja wakisaini hati za makabidhiano ya vifaa hivyo katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi za UNESCO jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Maofisa kutoka sekta ya mawasiliano UNESCO Dar es Salaam.
 


Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akikabidhi hati ya makubaliano na moja kati ya vifaa hivyo kwa Meneja wa radio ya Jamii ya Baloha FM ya Kahama, Samada Maduhu wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za shirika hilo jijini Dar es Salaam.


Picha juu na chini ni Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues na Mkurugenzi wa Radio Jamii Uvinza FM, Ayubu Kalufya kwa pamoja wakisaini hati za makabidhiano ya vifaa hivyo katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi za UNESCO jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Maofisa kutoka sekta ya mawasiliano UNESCO.

 


Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akikabidhi hati ya makubaliano na moja kati ya vifaa hivyo kwa Mkurugenzi wa Radio Jamii Uvinza FM, Ayubu Kalufya wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za shirika hilo jijini Dar es Salaam.





Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akigonga 'cheers' na wawakilishi wa redio jamii zilizopokea vifaa hivyo kwenye hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za shirika hilo Unesco jijini Dar es Salaam.

MWENYEKITI wa Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi amezitaka Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kushirikiana katika kutumia utajiri wake mkubwa wa raslimali kunufaika kiuchumi. Ushirikiano huo ni pamoja na kuzindeleza raslimali hizo na kutumia nembo moja ya kibiashara ili kuzalisha mabilionea wakubwa duniani. Mwenyekiti huyo alisema hayo katika mkutano wa Taasisi za Sekta Binafsi za Tanzania na Kenya zilizokutana jijini Dar es salaam kujadili kwa pamoja namna ya kuondoa vikwazo vya kufanya biashara baina ya wafanyabiashara wa nchi hizo mbili.

 
Mwenyekiti wa Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi akizungumza wakati akifungua mkutano wa Taasisi za Sekta Binafsi za Tanzania na Kenya zilizokutana jijini Dar es salaam kujadili kwa pamoja namna ya kuondoa vikwazo vya kufanya biashara baina ya wafanyabiashara wa nchi hizo mbili uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Pamoja na kutoa wito huo Dk Mengi pia amempongeza Rais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli pamoja na serikali yake kwa kuwa mstari wa mbele kuboresha ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Kenya. Aidha alisema dhamira yake ya kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda itasaidia kuwakwamua Watanzania kutoka katika umaskini. Katika mazungumzo hayo ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania –TPSF Dr Reginald Mengi na Ujumbe wa Kenya umeongozwa na Gavana wa Taasisi ya Sekta Binafsi ya Kenya – KEPSA Bw. George Owuor. 

 
Gavana wa Taasisi ya Sekta Binafsi ya Kenya – KEPSA Bw. George Owuor akimpongeza Mwenyekiti wa Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi kwa kutoa risala nzuri ya ufunguzi wa mkutano huo. 

 Akizungumza katika mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Bw. Godfrey Simbeye amesema mkutano huo umeitishwa kutokana na kujitokeza vikwazo vya kufanya biashara baina ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Kenya, jambo linalokwamisha malengo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya kujenga uchumi unaoongozwa na sekta Binafsi. Kwa upande wake Kiongozi wa Ujumbe wa KEPSA Bw. George Owuor amesema Wafanyabiashara wa Kenya wanapenda sana kushirikiana kibiashara na wenzao wa Tanzania, na wangependa kuona vikwazo vinavyokwamisha mahusiano ya kibiashara vinaondolewa.


Gavana wa Taasisi ya Sekta Binafsi ya Kenya – KEPSA Bw. George Owuor akiwasilisha mada kuhusu kupunguza pengo la biashara kati ya Tanzania na Kenya na kutumia fursa zilizopo na kutanua biashara nje ya mipaka katika mkutano wa Taasisi za Sekta Binafsi za Tanzania na Kenya zilizokutana jijini Dar es salaam kujadili kwa pamoja namna ya kuondoa vikwazo vya kufanya biashara baina ya wafanyabiashara wa nchi hizo mbili uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Meneja anayeshughulikia Utafiti, Uchambuzi na Sera wa Taasisi ya Sekta Binafsi ya Kenya – KEPSA, Victor Ogalo (kushoto) akitoa mada kuhusu changamoto za kisera za Tanzania na Kenya katika mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia walioketi ni Gavana wa Taasisi ya Sekta Binafsi ya Kenya – KEPSA Bw. George Owuor na Mwenyekiti wa Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi wakifuatilia kwa umakini mada hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Bw. Godfrey Simbeye (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Alaska Tanzania, Jennifer Bash wakifuatilia mada mbalimbali zikizokuwa zikiwasilishwa ukumbini hapo katika mkutano wa Taasisi za Sekta Binafsi za Tanzania na Kenya zilizokutana jijini Dar es salaam kujadili kwa pamoja namna ya kuondoa vikwazo vya kufanya biashara baina ya wafanyabiashara wa nchi hizo mbili uliofanyika jijini Dar es Salaam.


Pichani juu na chini ujumbe wa Tanzania na Kenya ulioshiriki mkutano wa Taasisi za Sekta Binafsi za Tanzania na Kenya zilizokutana jijini Dar es salaam kujadili kwa pamoja namna ya kuondoa vikwazo vya kufanya biashara baina ya wafanyabiashara wa nchi hizo mbili uliofanyika jijini Dar es Salaam.



Gavana wa Taasisi ya Sekta Binafsi ya Kenya – KEPSA Bw. George Owuor na mwenyeji wake Mwenyekiti wa Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi katika mkutano huo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Bw. Godfrey Simbeye akijibu maswali kwa waandishi wa habari (hawapo pichani). Kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi.

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.