Nchi za Afrika zinaweka mikakati inayolenga kukomesha uzalishaji na matumizi ya dawa bandia na sizizo na viwango, tatizo kubwa linalorudisha nyuma maendeleo ya nchi za Africa.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Dr. Agnes Kijo, akiongeza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Jukwaa la Kudhibiti Ubora wa Madawa Afrika (African Medicines Quality Forum-AMQF) jijini Dar es Salaam. Aliyekaa katika ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dr. Faustine Ndungulile, na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo Afrika (NEPAD), Margareth Ndomondo—wadau walijadili mbinu za kukomesha uzalishaji na usambaji wa dawa bandia na zisizo na viwango—mkutano uliandaliwa na NEPAD,  The United States Pharmacopeia convention (USP), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA),

“Lengo letu kuu ni kuhakikisha ubora wa dawa zinazotumiwa na waafrika,” amesema Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dr. Faustine Ndungulile, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Jukwaa la Kudhibiti Ubora wa Madawa Afrika (African Medicines Quality Forum—AMQF).  Kongamano hili limeandaliwa na Shirika la Maendeleo Afrika (NEPAD), The United States Pharmacopeia convention (USP), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA),
Kwa mujibu wa Waziri Ndungulile, dawa bandia na sizizo na viwango ni tatizo kubwa barani Afrika, linalohitaji mikakati madhubuti, na kusisitiza kuwa Afrika mikakati haiwezi kufanikiwa bila ushiriakiano wa wadau wote.
“Dawa bandia na sizizo na viwango zinagharimu pesa nyingi nchi za Afrika. Kuna watu wanakufa kwa ajili ya dawa hizi, pia kuna watu walazimika kutumia dawa nyingine za ziada. Zote hizi ni gharama kwa mwananchi mmoja mmoja na Serikali zetu kwa ujumla,” amesema Waziri Ndungulile.
Kama njia ya kudhibiti ongezeko la madawa bandia na sisizo na viwango, nchi za Afrika sasa hivi zinaweka mpango mkakati wa pamoja unaolenga kudhibiti usambaji na matumizi wa dawa bandia. Ameutaka Mkakati huo kama AMQF—jukwaa jipya la Africa lengo lake kuu ni kuweka mikakati mipana itakayotatua matatizo na changamoto zinazotokanazo na madawa yenye ubora hafifu yanayosambazwa kwa matumizi barani Afrika.  Kuanza kwa Jukwaa la AMQF kunakuja wakati kukiwa na ongezeko kubwa la matumizi ya madawa bandia na yasiyo na kiwango, yaliyokwisha muda wake katika sehemu mbalimbali barani Afrika, ikiwemo Tanzania.

Kwa mujibu wa shirika la afya duniani yaani ‘WHO’ asilimia 42 ya taarifa zinahusu madawa bandia na madawa yaliyokwisha muda wake, huripotiwa katika nchi za Afrika.

“Kupitia jukwaa hili matatizo ya ubora ya madawa yatashughulikiwa kikamilifu na hatimae kukomesha kabisa uzalishaji na usambazaji wa madawa bandia na zisizo na viwango katika masoko ya Afrika,” amesema Waziri.

Kwa mujibu wa Waziri Tanzania Tanzania ni moja ya nchini iliyofanikiwa kwa kiasi kikubwa katika udhibiti wa dawa bandia, jambo lilosababisha “Mkutano huu ufanyike hapa kwetu ili nchi zingine za Afrika zipate nafasi ya kujifunza kutoka kwetu.”
Aliongeza kwamba Tanzania imeweza kujitosheleza kwa dawa za kutosha na zenye viwango vya kimataifa na changamoto kubwa ilikuwa na kudhibiti dawa zinazoingia kwa njia ya panya ambapo tayari mamlaka husika (TFDA)  imeanza kushughulikia, kwa kufungua ofisi za kanda zinazolenga kupunguza mianya ya dawa zinazoingia kwa njia ya panya.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Bi Agnes Kijo alisema “Tanzania ina mahabara ya kisasa, zilizosambaa sehemu mbalimbali nchini…yote haya ni kuhakikisha ubora na viwango vya dawa zinazosambazwa katika masoko yetu na kutumiwa na watu.”
“Katika mkutano huu jambo kuu litakuwa na kwa namna ngani tunaweza kudhibiti dawa bandia kwenye masoko na kuhakikisha kwamba wazalishaji pia wanatoa dawa zenye ubora unaokubalika katika soko,” alisisitiza Bi Kijo.
Mkuu wa Mipango wa NEPAD, Margareth Ndomondo, amesema “Mamlaka za uthibiti lazima zitengeneze mifumo ya pamoja ikayosaidia kudhibiti usambazaji na matumizi katika nchi za Afrika kwa urahisi.”
Mkutano huo imekutanisha washiriki kutoka nchi 18 za Afrika –ikiwa ni pamoja na Nigeria, Ghana, Ethiopia, Uganda, Malawi, Zambia, Zimbabwe, Cameron, Ivory Coast, Mali, Burkina Faso, Mauritania, Senegal, Sierra Leone, Sudan, Guinea, and South Africa pamoja na mawakala barani Afrika kama vile Wakala wa Afya Afrika Magharibi (WAHO) na wafadhili wa maendeleo kama vile Shirika la Afya duniani yaani WHO, Shikla la misaada la Marekani yaani USAID pamoja na Benki ya Dunia.
Wawakirishi kutoka nchi zaidi ya 18 za Afrika wakifutia mijadala katika Mkutano wa Jukwaa la Kudhibiti Ubora wa Madawa Afrika (African Medicines Quality Forum-AMQF) jijini Dar es Salaam—unaolenga kukomesha uzalishaji, usambazaji na matumizi ya dawa bandia na zisizo na viwango.

Mwakilishi wa Shirika la United States Pharmocopeia Convention (USP, Bi. Emily Kaine, akiongea wakati wa Mkutano wa Jukwaa la Kudhibiti Ubora wa Madawa Afrika (African Medicines Quality Forum-AMQF) jijini Dar es Salaam—unaolenga kukomesha uzalishaji, usambazaji na matumizi ya dawa bandia na zisizo na viwango.

Mkuu wa Kitengo cha Mipango katika Shirika la Maendeleo Afrika (NEPAD), Bi. Margareth Ndomondo akiongea wakati wa Mkutano wa Jukwaa la Kudhibiti Ubora wa Madawa Afrika (African Medicines Quality Forum-AMQF) jijini Dar es Salaam—unaolenga kukomesha uzalishaji, usambazaji na matumizi ya dawa bandia na zisizo na viwango.

Mwakilishi wa Shirika la United States Pharmocopeia Convention (USP, Bi. Emily Kaine, akiongea wakati wa Mkutano wa Jukwaa la Kudhibiti Ubora wa Madawa Afrika (African Medicines Quality Forum-AMQF) jijini Dar es Salaam—unaolenga kukomesha uzalishaji, usambazaji na matumizi ya dawa bandia na zisizo na viwango.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dr. Faustine Ndungulile (katikati), akiongea na waandishi wa habari baada ya kufungua Mkutano wa Jukwaa la Kudhibiti Ubora wa Madawa Afrika (African Medicines Quality.

Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.