Na Mwandishi Wetu
WAKAZI wa Temeke wamehamasika na kuamua kuunda vikundi vya usafi wa mazingira, ‘Usafi Clubs’, ikiwa ni moja ya matunda ya mradi wa kuwawezesha wakazi wa mijini, ‘Urban Legal Empowerment’ unaolenga kusaidia jamii ya watanzania kupata haki zao za kuishi katika mazingira salama na safi, haki za kiuchumi na za kijamii.  
Kupitia mradi huu, unaotekelezwa na shirika la LEAT kwa ufadhili wa LSF, wakazi wa Temeke pamoja na kata zake, viongozi wa serikali za mitaa na jamii kwa ujumla wamehamashishwa kutunza mazingira katika maeneo wanayoishi au kufanyia shughuli zao za kila siku.
“Kama sehemu ya utekelezaji wa mradi huu, LEAT tumetoa elimu kwa wananchi, viongozi wa kata, madiwani, na wanafunzi, kuhusu sheria za mazingira, kanuni, na namna gani elimu hii itakavyowezesha wananchi kutunza na kuboresha mazingira yao,” amesema Bi. Glory Kilawe, Mratibu wa mradi kutoka LEAT.
Baada ya kupata elimu, wakazi wa Temeke wameunda vikundi vya mazingira, maarufu kama “Usafi Clubs”—ambavyo vinatumika kama vyombo vya kuhamasisha usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali wilayani Temeke.
Tunawashukuru LEAT kutupatia elimu hii nzuri ya mazingira, kujua sheria na taratibu mbalimbali zinazohusu mazingira,” anasema mmoja wa wakazi wa Temeke, Hassan Juma, katika kikao maalum cha kutathmini utekelezaji wa mradi wa LEAT wilayani humo.
Hemed Pazi, Mwenyekiti wa Kituo cha Wasaidizi wa Kisheria-Temeke (Temeke Paralegal Centre), anasema wamefanikiwa kuunda vikundi (Usafi Clubs) vinne—viwili viko kata ya Mbagala and 2 kata ya Mianzini–kama sehemu ya utekelezaji wa mradi huo.
“Kinachotufurahisha zaidi ni kwamba hata viongozi wa serikali za mitaa ni sehemu ya vikundi ni wajumbe wa Usafi Clubs. Hii inatia moyo, kwa sababu uwepo wa viongozi hawa unafanya vikundi hivi viaminike kwa jamii, na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake,” kwa mujibu wa Pazi.
Diwani wa Kata ya Mianzini, Abdallah Kipende amesema elimu inayotolewa na Usafi Clubs mitaani imebadilisha tabia na mitazamo ya wakazi wengi kuhusu maswala ya mazingira, hata kuwawezesha kununua vyombo na mapipa  ya taka kwa ajili ya majumbani na mitaani, kuacha kabisa tabia ya kutupa taka ovyo, kama walivyozoea siku za nyuma.
“Sasa hivi, jamii  ya Temeke iko makini sana katika maswala ya mazingira; kila mtu sasa anajua usafi wa mazingira maana yake nini. Kama kuna mtu (leo hii) anataka kujenga kiwanda au kuleta uwekezaji wowote Temeke, lazima ajiandae kujibu maswali magumu ya wananchi kama vile mbinu gani atakazotumia kutunza na kulinda mazingira,” alisema  Kipende.
Mbali na kuwezesha uundaji wa vikundi vya mazingira, LEAT imesaidia kutatua migororo ya mazingira 19, kuelimisha wanafunzi zaidi ya 600, kusambaza machapisho mbalimbali yanayohusu mazingira kwa jamii, kuandaa midahalo na vipindi maalum vya television na radio –kujadili maswala ya mazingira—kama sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Urban Legal Empowerment katika wilaya ya Temeke.
Mradi huu umebuniwa na kufadhiliwa na shirika la Legal Services Facility (LSF) na lengo kuu la mradi huu ni kuwezesha watanzania waishio mijini, hasa wasiojiweza kifedha, katika maswala mbalimbali ya kisheria, kijamii na kiuchumi.
Legal Services Facility (LSF) imeyawezesha mashirika sita yasiyokuwa ya kiserikali kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa Urban Legal Empowerment katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam
Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.