Na Damas Makangale, Dar es Salaam

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema Serikali ipo mbioni kujenga kituo cha kisasa cha maabara (A state of the Art) kwa ajili ya upimaji wa madini katika ukanda wa Afrika Mashariki kupitia Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) jijini Dodoma.

Mavunde aliyasema hayo hivi karibuni jijini Dar es Salaam wakati wa kikao na wahariri wa vyombo vya habari kilicholenga kuelezea mafanikio ya miaka minne ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan madarakani kwenye sekta ya madini hapa nchini.

Waziri Madini, Anthony Mavunde akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali kwenye mkutano wa thamini ya mchango wa sekta ya madini kwa taifa.

“tunakuwenda kujenga kituo cha kisasa kabisa ambacho kitakuwa kinatoa huduma kwenye ukanda wetu huu wa Afrika Mashariki na tutaendelea kujitikiza zaidi kwenye tafiti , tunawekeza zaidi kwenye kufanya utafiti wa madini ili kujua hazina ya madini tuliyo nayo kwenye nchini yetu,” alisema Mavunde.

Aliongeza kwamba hicho kituo kitakuwa kitovu cha upimaji wa madini, yenye maabara za kisasa, vifaa vya teknolojia , ubora na viwango vya kimataifa na kutoa dhamani halisi ya madini yanayopima hapo.

“Tunalenga kuifanya GST kuwa kitovu cha utoaji wa huduma za kimaabara kwa Afrika Mashariki na kusini mwa Jangwa la Sahara. Kwa sasa, tupo katika mazungumzo na taasisi ya GTK kutoka Finland ili kushirikiana na wataalamu wetu kuhakikisha kazi hii inafanyika kwa weledi na ubora wa juu,” amesema Mavunde.

Aliongeza kwamba katika mipango madini wa 2020-2030 (Mining Vision) madini ni maisha na utajiri , wizara imejipanga kuwekeza zaidi kwenye tafiti ili kuendelea kubaini (deposit) kiasi cha madini ambayo tunayo chini ya ardhi na kuweka mikakati ya kufanya uchimbaji kwa kushirikisha wachimbaji wadogo , wakubwa na wa kati na wawezekaji kutoka nje.

Alisema kwamba pamoja na mambo mengine serikali ya awamu ya sita , kupitia wizara ya madini wataendelea kuwawezesha wachimbaji wadogo kwa mitambo  ya kuchoronga miamba na kuwaunganisha na taasisi za kifedha ili waweze kupata mikopo na kupanua shughuli zao za uchimbaji wa madini mbalimbali hapa nchini.

Wahariri kutoka vyombo mbalimbali wakiuliza maswali kwenye mkutano huo

Alisema kwamba kwa upande wake wa viwanda vya ongezaji wa thamani ya madini mpaka vipo saba hapa nchini kwa ajili ya usafishaji na kuongeza thamani ya madini mbalimbali na kuchochea upatikanaji wa ajira kwa vijana wa kitanzania.

Waziri Mavunde alifafanua kwamba mchango wa sekta ya madini kwenye pato la taifa linaendelea kukua ambapo 2023/24 ilikuwa asilimia 9.0% na 2024/2025 tayari ni 10.1% tayari wamevuka lengo ambapo liliwekwa na serikali.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Injinia Yahaya Samamba akizungumza na wahariri kwenye kikao cha thamini ya mafanikio ya wizara hiyo kwenye sekta ya madini kwa miaka minne ya awamu ya sita chini , Dkt Samia Suluhu Hassan 

Aliongeza kwamba serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (Stamico) wapo kwenye mikakati na hatua za mwisho za kujenga kiwanda cha madini chumvi huko Lindi kuweza kuongeza thamani ya madini hayo na kuendelea kutoa ajira kwa watanzania.

Mavunde aliogeza kwamba serikali katika kipindi cha miaka minne ya awamu ya sita imefanya marekebisho na kutunga sheria za maudhui ya ndani (Local content) ambayo imendelea kutoa fursa kwa wazawa kwenye sekta ya madini kwa upatikanaji wa kazi za migodini na marekebisho ya Uwajibikaji wa Jamii (CSR) ilicholenga kuelezea mafanikio ya miaka minne ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.



Amesisitiza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali kuboresha mazingira ya uwekezaji katika sekta ya madini kwa kutumia teknolojia za kisasa na huduma bora za kitaalamu.




Mwisho.


Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.