Na Mwandishi Wetu, Mwanza 

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Dkt Janet Lekashigo ametoa wito kwa wadau kuendelea kushiriki kwenye Jukwaa la madini ili kuleta na kuchochea fikra za nafasi ya ushirikishwaji wa watanzania kwenye sekta ya madini nchini.

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Dkt Janet Lekashigo akitoa neno la ufunguzi kwenye Jukwaa la nne la Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa wattanzania katika sekta ya madini , mkutano huo uliondaliwa na Tume ya Madini nchini, unafanyika kwa siku tatu jijni Mwanza.

Akizungumza kwenye Jukwaa la nne la utekelezaji wa ushirikishwaji wa watanzania katika sekta ya madini unaofanyika jijni Mwanza, Dkt Lekashigo alisema kwamba jukwaa hilo ni kuchochea fikra mpya na majadiliano ya kitaaluma ili kuweza kusaidia watanzania kushiriki kwenye uchumi wa sekta ya madini.

“Jukwaa hili la nne ni la majadiliano , mawazo na kuleta fikra Chanya ili kuchochea mabadiliko ya ushirikishwaji wa watanzania kwenye sekta ya madini ili waweze kunufaika na rasilimali za madini hayo kwenye maeneo yao,” alisema Dkt Lekashigo 

Aliongeza kwamba umuhimu wa Jukwaa hilo ni kuja pia na mapendekezo mbalimbali ya namna bora ya kuwawezesha na kufungua milango ya watanzania wazawa kufanya kazi zaidi za ukandarasi na zabuni kwenye migodi hapa nchini.

Dkt Legashiko alisema kwamba Tume hiyo itaendelea kushirikiana na wadau wote kwenye sekta ya madini hususani sekta binafsi kupitia Maudhui ya Ndani (Local content) kuhakikisha dira ya madini ni maisha ni utajiri inakamilishwa kikamilifu kwa kuwashirikisha watanzania wazawa kwenye sekta ya madini nchini. 

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Madini na Biashara kutoka Tume ya Madini, CPA, Dkt Venance Kasiki, alisema kwamba Tume hiyo imeendelea kutoa mafunzo na elimu kwenye makampuni, taasisi  za elimu mbalimbali na jamii kwa ujumla ili uelewa wa Maudhui ya Ndani (Local Content) ili watanzania wapate uelewa zaidi kuhusu kanuni hiyo.

“Serikali kupitia Tume ya Madini imejikita na ina wataalamu wa kutosha wa kutoa elimu kuhusu Maudhui ya Ndani (Local Content) ili watanzania waweze kupata uelewa na kuingia kwenye sekta ya madini kwa ajili ya kupata kazi za kutoa huduma , ajira na ukandarasi wa shughuli mbalimbali kwenye migodi ambayo ipo hapa nchini,” aliongeza Dkt CPA Kasiki 

Alisema kwamba ni umuhimu kwenye hii ushirikishwaji wa watanzania kwenye sekta ya madini moja ya nyenzo muhimu ni ya kuungana (Joint venture ) kwa maana ya kutunisha mtaji ili kuweza kupata kazi kwenye migodi iliyopo hapa nchini.

Dkt CPA Kasiki alifafanua kwamba serikali iliamua kuja na kanuni ya Maudhui ya Ndani (Local Content)  baada ya kilio cha umma (Public Outcry) kuhusu kwa watanzania hususani jamii inayozunguka migodi kutokunufaika na uwepo wa rasilimali madini.

“Baada ya kilio hicho cha muda mrefu na baadaye kuja kwa sera ya madini ya mwaka 2009 ya kuwawezesha watanzania wazawa kushiriki katika uchimbaji wa madini , kupata kazi za ukandarasi, zabuni na kutoa huduma mbalimbali,” alisema Dkt Kasiki

Dkt CPA Kasiki aliongeza kwamba pamoja na mambo mengine sheria ya madini 2019 na 2022 ili kuja ili kutatua matatizo na kero za ushirikishwaji wa watanzania kwenye sekta ya madini ili kupanua wigo na utatuzi wa changamoto hizo.

Aliongeza kwamba fursa za kukuza mnyororo wa thamani kwa watanzania kupitia sekta ya madini ni kubwa na pamoja mambo mengine fursa za kazi kama vile , mitambo ya migodini , Tehama , ujenzi wa viwanda vya kutoa bidhaa kwenye migodi, usafi na ufuaji wa nguo , famasi na tiba na huduma ya chakula.  

 Mwisho 

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.