Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Charles Mkumbo.
Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza linamshikilia mfanyabiashara maarufu Jijini humo Juma Mahende, anayemiliki Mabasi ya J4 kwa tuhuma ya kuwapiga risasi watu wawili na kuwapotezea maisha, katika eneo la Boma lililopo kata ya Nyakato Jijini humo.

Ni nyumbani kwa Marehemu Cloud Skalwanda, eneo la Nyasaka kata ya Kiloleli wilayani Ilemela Jijini Mwanza, ambako ndugu, jamaa na marafiki wa Marehemu, wamekutana kuomboleza msiba huo.

Tukio hilo limetokea majira ya saa nne usiku wa kuamkia leo katika eneo la Boma lililopo kata ya Nyakato, baada ya mtuhumiwa Juma Mahende kumuita Marehemu Cloud Skalwanda, na mwenzake Ally Mohamed mkazi wa kata ya Igoma kuzungumza masuala ya kibiashara.

Baada ya tukio hilo nyumbani kwa Marehemu Ally Mohamed kata ya Igoma, simanzi na vilio pia vikatawala, huku chanzo cha mauaji hayo kikielezwa kuwa marehemu hao walikuwa wakimdai mtuhumiwa shilingi milioni 25/=.

Wakizungumzia mauaji hayo kwa masikitiko makubwa huku wakibubujikwa na machozi, kaka wa marehemu Ally Mohamed Abeid aitwaye Ramadhan Mohamed Abeid pamoja na dada wa marehemu Claude, Bi. Aziza Steven Sikalwanda wamevitaka vyombo vya dola kuhakikisha vinatenda haki katika uchunguzi wa suala hilo.
Mjane wa marehemu Ally Mohamed Abeid, Bi. Dominata Gabriel pamoja na mmiliki wa nyumba aliyokuwa anaishi marehemu Ally Mohamed Abeid iliyoko eneo la Igoma Bw. Roger Rwegasira wanaeleza walivyopokea taarifa za kuuawa kwa watu hao.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Charles Mkumbo, amesema kuwa tayari Jeshi la Polisi mkoani hapa, linamshikilia mtuhumiwa Juma Mahende kwa uchunguzi zaidi.

Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.