Afisa Mkuu Mtendaji wa kampuni ya
kuunda magari ya Volkswagen Martin Winterkorn amejiuzulu baada ya habari
kutokea kuwa magari ya kampuni hiyo yalikuwa yamefanyiwa ukarabati
kuyawezesha kukwepa ukaguzi wa utoaji wa gesi hatari kwa mazingira
nchini Marekani.
"Naomba msamaha mimi binafsi kwamba tumevunja heshima kwa wateja wetu na umma kwa jumla," alisema Winterkorn.
Hisa za kampuni hiyo zilishuka kwa asilimia 18 baada ya kufichuka kwa habari hizo.
Kampuni hiyo ya magari kutoka Ujerumani ilishinikizwa kurudisha magari yake nusu milioni siku ya ijumaa.
Shirika la kuhifadhi mazingira Marekani lilipata kifaa hicho katika magari ya Audi A3,VW jetta, Beetle, Golf na yale ya aina ya Passat.
Mbali na kuyarejesha magari hayo kwa ukarabati, kampuni hiyo pia itakabiliwa na faini za mabilioni ya madola na viongozi wake huenda wakashtakiwa.
Shirika hilo la mazingira linasema kila gari ambalo halikuzingatia sheria ya hewa safi itapigwa faini ya dola 37,500.
Inakadiriwa kuwa magari 482,000 yameuzwa na kamapuni hiyo tangu mwaka 2008 na huenda faini hizo zikafika dola bilioni 18.
Chanzo na bbc.com/swahili
Post a Comment