October 2024

Wanafunzi 6000 wa Shule za Msingi Dar wanufaika na elimu ya usalama barabarani

.Mradi ulioanzishwa na Total Energies Marketing Tanzania

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MRADI wa “VIA Creative” unaolenga kuwapatia elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa Shule za Msingi umewafikia takribani wanafunzi 6000 kwenye Shule za Makuburi, Ubungo, NHC, Buza, Jangwani, Ugindoni na Uzuri katika jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Total Energies, Bw Mamadou Ngom akizungumza na wageni waalikwa , wanafunzi kwenye hafla ya kukabidhi tuzo na vyeti kwa wanafunzi na shule iliyofanya vizuri kwenye shindano wa mradi wa “VIA Creative” wa kutoa elimua ya usalama barabarani hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni .

Mgeni rasmi kwenye hafla hiyo ya kukabidhi tuzo wa wanafunzi waliofanya vizuri na shule  iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni,  Mkuu wa Idara ya Mafunzo ya Trafiki Kinondoni, A.S.P Rose Bernard Maira aliwapongeza Total Energies Marketing Tanzania Limited, TotalEnergies Foundation Pamoja na Nafasi Art Space kwa juhudi zao za kutoa elimu ya usalama barabarani zinastahili kupongezwa na kuigwa na makampuni mengine ili kuchochea usalama wa watoto waendapo na watokapo mashuleni.

“Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani tupo Pamoja nanyi kwenye jambo hili na katika kutoa elimu ya usalama barabarani pamoja na kuzijua sheria, kanuni na taratibu za barabarani kwa wanafunzi na watumia Barabara wote.

“Aidha, tumefurahia kujua kwamba mradi huu pia unalengo la kutimiza mapendekezo ya kuboresha hali ya usalama kwa wanafunzi wa shule iliyoshinda kama trulivyopata kuona kwenye filamu ya wanafunzi hao. Pia niwatakie kila la heri washindi hawa kwenye hatua nyingine ya shindano ambalo wanatarajia kuingia, nawasihi muiwakilishe Tanzania vizuri na mungae Pamoja na kushinda ngazi za shindano la VIA Creative zijazo.” Aliongeza.

Mmoja ya wanafunzi wa Makuburi akipokea tuzo yake kutoka kwa Mgeni rasmi , ASP , Rose Bernard Maira 

Alisema kwamba usalama barabarani ni suala muhimu katika jamii yetu,kila mwaka tunashuhudia ajali nyingi za barabarani ambazo zinaweza kuzuiliwa kwa njia rahisi ya kueneza elimu sahihi ya sheria, alama na utumiaji salama wa barabara.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Total Energies, Bw Mamadou Ngom alisema kwamba shindano hilo ambao lilikuwa kwa njia ya sanaa ya michoro, muziki, maigizo na mashairi kuna ongeza uelewa wa wanafunzi kwenye mambo ya usalama barabarani na kupunguza ajali.

“Tunayo furaha kubwa kuwa hapa leo tukisherehekea mafanikio ya mabalozi wetu wa usalama barabarani kupitia mradi wa VIA Creative amabo tumeshirikiana na Nafasi Art Space ambao wamekuwa wakiwapatia wanafunzi hawa elimu ya usalama barabarani kwa kupitia sanaa,”

“Kupitia mradi huu tumeweza kuunda klabu za mabalozi barabarani 120, 20 kutoka kwenye kila shule. Pia wanafunzi hawa wameweza kutoa mapendekezo yao ya jinsi ambavyo usalama wao wa barabara unaweza kuboreshwa nasi tutatekeleza mapendekezo hayo kwa shule ya msingi ya Makuburi ambao ndio washindi wa kitaifa wa shindano hili kwa mwaka 2024.” Alisema Bw Ngom

Aliongeza kwamba usalama barabarani ni suala muhimu katika jamii yetu,kila mwaka tunashuhudia ajali nyingi za barabarani ambazo zinaweza kuzuiliwa kwa njia rahisi ya kueneza elimu sahihi ya sheria, alama na utumiaji salama wa barabara.

Alisema kwamba  ni jukumu letu sote kuhakikisha tunafuata sheria na kanuni za usalama barabarani ili kuepuka ajali ambazo athari zake kiuchumi na kijamii ni kubwa sana.

“Ningependa kuchukua fursa hii kuwapongeze  wanafunzi wote 120 walioshiriki kwenye mradi huu na kushindanishwa kwenye shindano la VIA Creative, nyinyi nyote ni washindi na mabalozi bora wa usalama barabarani. Tunawaomba muendele kuwafundisha wenzenu, wadogo zenu, na hata wazazi wenu juu ya utumiaji salama wa Barabara Pamoja na sheria na kanuni zake,” alisisitiza.

Bw Ngom aliongea kwamba Total Energies wapo pamoja na Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani  kwenye jambo hilo na katika kutoa elimu ya usalama barabarani pamoja na kuzijua sheria, kanuni na taratibu za barabarani kwa wanafunzi na watumia Barabara wote.

Mkuu wa Idara ya Mafunzo ya Trafiki Kinondoni, A.S.P Rose Bernard Maira akizungumza na wageni waalikwa kwenye hafla ya kugawa tuzo kwa wanafunzi na shule za jijini Dar es Salaam kwenye mradi wa “VIA Creative” unaolenga kutoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi jijini Dar es Salaam. 

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Nafasi Art Space ambaye ni mdau wa mradi huo, Felix Muchira alisema kwamba waliona ni muhimu kutoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi kwa njia rahisi ya maigizo na uchoraji ili waweze kufikisha ujumbe kwa haraka zaidi.

“ajali hapa nchini limeanza kuwa jambo la kawaida na ni jukumu letu sote kuendelea kutoa elimu kwa kushirikiana na serikali na hasa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani kutoa elimu ya michoro, alama na sheria za usalama barabarani kwa Watoto wetu,” alisema Bw Muchira.

Mgeni rasmi wa shughuli hiyo, ASP Rose Bernard Maira akigawa cheti/ tuzo kwa mwalimu wa Shule ya msingi Makuburi iliyoibuka kidedea kwenye shindano la mradi huo 

Shindano hilo la kimataifa la "VIA CREATIVE" ni shindano linalolenga wanafunzi wa shule za msingi wa miaka 4 -19 kwa lengo la kuwapatia elimu ya usalama barabarani kwa njia ya sanaa ya michoro, muziki, maigizo na mashairi na kisha kuwapa fursa wanafunzi hao kuelezea uleewa wao na mapendekezo yao ya usalama barabarani kwa njia ya michoro na maigizo.

Mwaka huo  wa VIA Creative umewafikia wanafunzi 6000 kutoka shule za msingi Makuburi, Ubungo NHC, Buza, Jangwani, Ugindoni na Uzuri zilizopo jijini Dar es salaam na kuendeleza uundaji wa klabu za mabalozi wa usalama barabarani. 


Mwanafunzi kutoka  Shule ya Msingi Makuburi akipita baada ya kupokea cheti chake mbele ya Mkurugenzi Mkuu wa Total Energies, Bw Mamadou Ngom

VIA Creative ni mradi ulioanza mwaka 2022 ambao tangu mwaka huo zaidi ya wanafunzi 22,000 wamefikiwa na mradi huu na kuweza kujenga klabu za mabalozi wa usalama barabarani kwenye shule 100 jijini Dar es Salaam na Bagamoyo.

Hafla ya kukabidhi tunzo kwa wanafunzi walioshinda kwenye msimu huu wa tatu wa VIA Creative zilifanyika kwenye ofisi za TotalEnegies Marketing Tanzania Limited jijini Dar es Salaam ambapo shule ya msingi ya Makuburi Primary school iliibuka mshindi wa kitaifa wa shindano lwa shindano hili na muwakilishi wa Tanzania kwenye ngazi ya kimataifa munamo mwezi Novemba 2024.


Mwanafunzi kutoka  Shule ya Msingi Makuburi akipita baada ya kupokea cheti chake mbele ya Mkurugenzi Mkuu wa Total Energies, Bw Mamadou Ngom.



Baadhi ya wafanyakazi wa Total energies wakifuatilia tukio hilo kwenye hafla hiyo 

Mwisho

 


 

Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa Tanzania, Bi, Esther Cecil Maruma (Katikati) akiwa na watendaji waandamizi wa benki hiyo kwenye picha ya pamoja katika kuadhimisha siku ya huduma kwa wateja hivi karibuni jijini Dar es Salaam. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa Tanzania, Bi, Esther Cecil Maruma (Katikati) akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa sherehe ya wiki ya huduma kwa wateja pamoja naye ni watendaji waandamizi wa benki hiyo.

Bank Of Africa Tanzania, imeungana na sehemu nyingine duniani katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja 2024, chini ya kauli mbiu “Above and Beyond”- na kuahidi kuendelea kutoa huduma bora wake.

Akizungumza kwenye uzinduzi, Mkurugenzi Mtendaji, Esther Cecil Maruma alisema, “Kwetu Bank of Africa Tanzania, wateja wetu tunawapa kipaumbele kikubwa katika kila mipango tunayofanya. Tunaamini kuwa huduma bora ni zaidi ya kuwapatia huduma za kifedha bali ni kujenga uhusiano mzuri na wa muda mrefu. Wiki ya Huduma kwa Wateja 2024 ni fursa ya kutambua na kusherehekea imani ya wateja wetu kwetu pia tukithamini kujitoa kwa wafanyakazi wetu wanaofanya kazi bila kuchoka kutoa huduma bora. Tunatarajia kuendelea kutoa huduma zenye viwango vya juu na wigo mpana kuhakikisha tunafikia malengo makubwa”.

Alisema Kauli mbiu ya mwaka huu ya “Above and Beyond” inadhihirisha dhamira ya benki kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja na kukidhi matarajio yao na kuweka msisitizo  kwa  wafanyakazi wetu kutoa huduma  kwa ufanisi mkubwa wa kipekee.

Katika kudhihirisha dhamira yake ya kutoa huduma bora na kuwa karibu zaidi na wateja wake alisema, Bank of Africa Tanzania karibuni ilianzisha huduma ya “BOA Wakala” inayowezesha wateja kuweka na kutoa fedha bila kulazimika kutembelea matawi yake na kuboresha zaidi  huduma za kibenki kupitia simu ya mkononi (B-Mobile) ili iweze kutumiwa na wateja  kwa urahisi na kwendana na matakwa yao.

Kwa upande wake, Mkuu wa Huduma kwa Wateja wa Bank of Africa, Annaroberta Mango, alisema katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja wafanyakazi wa Benki watapata fursa ya kuongea na wateja kwenye matawi, kupokea maoni yao sambamba na kuwapatia ushauri wa kifedha katika kuimarisha biashara zao.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa Tanzania, Bi, Esther Cecil Maruma wa pili kushoto akitoa zawadi kwa mmoja ya wateja wa benki hiyo , Bw Conrad leo , mwanzo kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji (Uendeshaji ) , Bw Wasia Mushi na mwanzo kushoto ni Mkuu wa Huduma kwa Wateja , Bi Annaroberta Mango.

“Tunajivunia timu yetu ya Wafanyakazi wetu yenye moyo wa kujitolea kufanikisha kutoa huduma bora kwa wateja wetu kila siku. Wiki ya Huduma kwa Wateja pia ni nafasi yetu ya kutambua mchango wao mkubwa. Ni matarajio yetu tutaisherekea pamoja na wateja wetu na kuwashukuru kwa kuichagua Bank of Africa na kuwadhihirishia jinsi tunavyowathamini kwa kuendelea kutuamini,”Mango.

Bw. Conrad Leo, mmoja wa wateja wa  Bank of Africa Tanzania customers, alisema amekuwa mteja wa Benki hiyo kwa kipindi cha miaka mitano na anafurahia na kuridhika na huduma zinazotolewa na benki na anapokuwa na changamoto za kibiashara amekuwa akipatiwa suluhisho.

Katika wiki ya Huduma kwa Wateja Benki  itakuwa na shughuli mbalimbali zitakazoshirikisha wafanyakazi na wateja ikiwemo kuwashukuru wateja, kuwazawadia wafanyakazi,mafunzo zaidi kwa wafanyakazi kutoa huduma kwa wateja na kushiriki huduma za  kijamii na kutoa msaada kwa jamii.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa Tanzania, Bi, Esther Cecil Maruma (kushoto) akikata keki pamoja na mmoja ya wateja wa benki hiyo, Bw Conrad leo (Katikati) kwenye sherehe ya wiki ya huduma kwa wateja , kulia ni Wasia Mushi, Naibu Mkurugenzi Mtendaji (Uendeshaji ) wa benki hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa Tanzania, Bi, Esther Cecil Maruma (Katikati) akiwa pamoja na watendaji waandamizi wa benki hiyo kwenye maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa Tanzania, Bi, Esther Cecil Maruma akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wiki ya huduma kwa wateja jijini Dar es Salaam hivi karibuni

...Waahidi kuendelea kutoa huduma bora, viwango vya kimataifa 

....Kwenye gesi waunga mkono juhudi za Dkt Samia suluhu hassan nishati safi, mazingira 

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Kampuni ya mafuta ya Total Energies imefungua wiki ya huduma kwa wateja kwa kutoa ahadi ya kuendelea kutoa huduma bora ya mafuta yenye viwango vya juu, vilainishi vya injini na vifaa vya magari kwa viwango vya kimataifa, Makangale Satellite inaripoti.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kwenye uzinduzi wa kituo cha mafuta cha makanya magomeni jijini Dar es Salaam, Total Energies, Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano , Getrude Mbakile alisema kwamba kampuni hiyo imejipanga kuendelea kutoa huduma kwa wateja wake vya viwango vya kimataifa.

Mmoja wa mawakala wa Total Energies, kutoka Arasco Energies, Mohamed Binzoo akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni Total energies magomeni makanya wakipeana zawadi baada ya kufungua rasmi kituo hicho mafuta leo, kwenye sherehe za wiki ya huduma kwa wateja, jijini Dar es Salaam.


“Tunawashukuru sana wateja wetu kwa kuendelea kutuamini na kutupa ushirikiano wa kutosha kwenye sekta hii muhimu ya usafirishaji , magari, vifaa na vipuri vya vyombo vya moto sie tutaendelea kutoa vifaa na vilainishi vya mafuta kwa ajili ya magari yao kwa uaminifu mkubwa, aiongeza Bi Mbakile kwa msititizo 

Aliongeza kwamba kwa kufungua kituo cha mafuta eneo la magomeni , makanya jijini ni juhudi za makusudi za kampuni hiyo kuleta huduma zao karibu na wateja wao ili waweze kupata huduma zote kwa urahisi zaidi na za uhakika.

“Kituo hiki kimezinduliwa rasmi leo lakini kina miezi mitatu tu tangu kianze kufanya kazi na mwitikio wa wateja wetu ni mkubwa mno kutoka na huduma zinazotolewa hapa ni za viwango vikubwa , alisema Bi Mbakile.

Naye, Mkurugenzi wa kampuni ya Arasco Energies, ambao ni wakala mkubwa wa Total energies, Bw Thabit Ameir alisema kwamba kampuni hiyo Total energies imefungua kituo hicho kipya katika juhudi za kuwaletea wateja wao karibu na huduma zao za mafuta na vilainishi mbalimbali vya mafuta kwenye magari, pikipiki na vyombo vingine vya moto.

“Tutaendelea kutoa huduma bora kabisa zenye viwango vinavyokubalika duniani na kusherekea wiki ya huduma kwa wateja tumeamua kufungua kituo hiki hapa magomeni makanya ili kusogeza huduma hizi karibu na watanzania,” alisema Bw Ameir 

Kwa upande , Afisa Masoko wa kampuni hiyo anashughulikia gesi , Bw Allan Ngogolo alisema kwamba kwa upande wa gesi kampuni hiyo itaendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita , chini Dkt Samia Suluhu Hassan kuhusu nishati safi ya kupikia ya gesi na kutunza mazingira.

“Tunatoa wito kwa mawakala wakubwa na wadogo waje kufanya biashara na sisi si tu mafuta hata gesi na kuhakikisha kwamba huduma hii ya nishati safi inaendelea kusambazaa hadi maeneo ya pembezoni , mikoani na vijini nchini kote,” alifafanua.

Ngogolo aliongeza kwamba nia ya kampui na kuona watanzania wengi hasa wa vijini wanaanza kutumia nishati za safi kwa ajili ya kupikia na kuondokana na matumizi ya mkaa na kuni ambao unasababisha uchafu wa mazingira.



Mwisho

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.