Utagharimu takribani shilingi Bilioni 4.8 za kitanzania
Na Mwandishi Wetu, Kahama Shinyanga
Mgodi wa
Barrick Buzwagi ambao uko katika mchakato wa kufungwa umefadhili mradi wa ujenzi wa chujio la maji
ya mvua eneo la mwendakulima wilayani
Kahama mkoani Shinyanga unaoghalimu takribani shilingi Bilioni 4.8 kwa ajili ya kuwapatia wananchi wa mji wa
kahama maji safi na salama.
Akiongea wakati wa hafla ya kupokea mwenge
ulioambatana na kuweka jiwe la msingi la ujenzi huo wa mradi wa maji, Meneja wa
Ufungaji wa Mgodi wa Buzwagi ,Zonnastraal Mumbi alisema mgodi katika hatua zake za mwisho za ufungaji
umeamua kufadhili mradi huo ili kuondoa tatizo la upatikanaji wa maji kwenye
Wilaya ya Kahama.
“haya ni matokeo ya ufungaji wa mgodi wa
Buzwagi kwa kuamua kufadhili mradi mkubwa kabisa wa maji ya mvua kwa
kutengeneza miundombinu ya uvunaji , ukusanyaji na usambazaji wa maji ya mvua
kwa ajili ya matumizi wa wananchi wa mji ya Kahama,” alisema Mumbi.
Aliongeza kwamba moja ya dhamira ya
kampuni ya Barrick inayoendeha shughuli zake nchini kwa ubia na Serikali
kupitia kampuni ya Twiga Minerals ni kuunga mkono jitihada za Serikali
kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama.
“Mgodi wa Buzwagi umefadhili mradi huu wa
maji ya mvua kwa 62% kwa ajili ya kuhakikisha kwamba miundombinu ya kisasa na
bora inajengwa kwenye mradi huu kama sehemu za kuleta matokeo Chanya kwa
wananchi wa mji wa kahama,” alisisitiza
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Usambazaji
Maji na Usimamizi wa Mazingira, ,
Mamlaka ya Maji Safi wa Mazingira Kahama
(KUWASA)Mhandisi , Magige Marwa , alitoa pongezi kwa kampuni ya Barrick nchini kwa kufadhili mradi huo mkubwa ambao
ukikamilika utaondoa changamoto ya upatikanaji maji safi na salama wilayani
Kahama,
Aliongeza kwamba mradi wa ujenzi wa chujio
la maji mwendakulima unatazamiwa kuhudumia zaidi ya 66% ya wakazi waishio
manispaa ya Kahama na una uwezo wa kuzalisha lita milioni 10 kwa siku.
“Mradi huu unatarajiwa kukamilika Desemba
mwaka huu na mpaka sasa 78% ya mradi mzima umeshakamilika kutokana na kasi ya
ujenzi wa mradi huu mkubwa kwenye mji huu wa kahama,” alisisitiza
Mhandisi Marwa alifafanua kwamba mradi huo
wa chujio la maji ya mvua 62% imefadhiliwa na mgodi wa Barrick- Buzwagi na 38%
ni KUWASA kupitia Wizara ya Maji na Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa
Tanzania.
Kwa upande wake , kiongozi wa mbio za
mwenge , Ismail Ali Ussi alisema wizara ya maji inaendelea kufanya vizuri na
kutekeleza kwa vitendo maono ya Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya
kumtua mama ndoo kichwani kwa kupeleka huduma ya maji mijini na vijijini.
“Nachukua fursa hii kuwapongeza wataalamu
wote wa wizara na mamlaka za maji hapa kahama kwa kufanya kazi usiku na mchana
katika kuhakikisha watanzania wanapata maji safi na salama,” amesema.
Kwa upande wake , Mkuu wa Wilaya ya
Kahama, Frank Nkinda alisisitiza kwamba umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii na
kuendelea na ari hiyo ya kutekeleza miradi ya huduma za wananchi kwa viwango
vya juu ili kukidhi mahitaji ya wananchi.
Mwisho
Post a Comment