September 2025

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob John Mkunda, amempandisha cheo Alphonce Simbu kutoka Sajini kuwa Sajinitaji katika hafla iliyofanyika ofisini kwake Makao Makuu ya Jeshi Upanga Jijini Dar es Salaam leo Septemba 25, 2025 baada ya kupata mafanikio ya Mbio za Marathon Tokyo, Japan.

Jenerali Mkunda amesema ushindi wa Simbu wa kutwaa medali ya dhahabu katika Mashindano ya Mbio za Marathon ya Dunia Kilomita 42, zilizofanyika Toyo Japan ni kwa Watanzania wote na Afrika kwa ujumla na kwamba michezo ni sehemu ya kazi jeshini, hivyo Sajinitaji Alphonce Simbu amefanya kazi nzuri na kuwataka Maafisa na Askari wote jeshini kuiga mfano wa Sajinitaji Simbu.


Dr Ibrahim Shaddad met President for IUGS Dr Hassina Mouri is the President of the International Union of Geological Sciences (IUGS) Unesco chair in medical geology in Africa:


  • AMGC's Support: Encouraging more African states to join IUGS.
  • Medical Geology Cooperation: Exploring ways to work together on medical geology initiatives in Africa.
  • Upcoming Visit: Dr. Mouri is expected to visit AMGC in Dar es Salaam for further discussions and familiarization.

This potential partnership could lead to increased knowledge sharing, capacity building, and research in the field of medical geology, ultimately benefiting African nations.



..Yapongeza mchakato wa Ufungaji wa Mgodi wa viwango vya Kimataifa 

Na Mwandishi Wetu, 

Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) umeipongeza kampuni ya Barrick kwa weledi na kuzingatia viwango vya kimataifa katika mchakato wa ufungaji wa mgodi wake wa Buzwagi na kubadilisha matumizi ya eneo hilo na kuwa Kongani Maalum la Uwekezaji (SEZ) ambalo inafungua fursa za kiuchumi nchini.

Mjumbe wa maofisa hao wa TISEZA ukiongozwa na Mkurugenzi  Mkuu wake, Gilead John Teri ilifanya ziara hiyo kikazi jana na kuridhishwa na mchakato mzima wa ufungwaji wa mgodi huo.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) Bw.Gilead John Teri akizungumza na  Kamati ya Utekelezaji wa Kongani Maalum la Uwekezaji wa Buzwagi na Wafanyakazi wa Barrick baada ya kukamilisha ziara ya kikazi ya kutembelea eneo hilo.

Akiwa katika eneo hilo , Bw Teri alipata taarifa fupi ya uwekezaji wa aina mbalimbali ndani ya kongani hilo maalum la Uwekezaji (SEZ) na kukagua maeneo mbalimbali yatakayotumiwa na wawekezaji watakaohitaji kuwekeza katika Kongani hiyo na alitembelea kiwanda cha kuzalisha (Conveyor) ambacho tayari kimeanza kufanya uzalishaji na kutoa fursa za ajira.

Akiongea baada ya ziara hiyo,Bw.Teri alitoa pongezi kwa kampuni ya Barrick nchini kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za serikali kwa kufanikisha ufungaji wa mgodi huo kwa  viwango vya kimataifa na kufungua fursa ya eneo la kimkakati wa kukuza uchumi kupitia uanzishaji wa viwanda na kufungua milango ya biashara.

“Nawapongeza Barrick kwa kuhakikisha mgodi huu unafungwa kitaalamu pia nachukua fursa hii kuwashukuru kamati ya Utekelezaji wa Kongani hii inavyofanya kazi kwa Kushirikiana na mamlaka mbalimbali lengo likiwa kutimiza kufanikisha lengo la serikali la kuhakikisha eneo hili linatumika kimkakati ili liweze kuleta matokeo chanya kwa taifa ”,alisema Teri.

Teri pia alisema ameridhishwa na utangazaji wa eneo hilo unaoendelea ambazo zinabainisha fursa zilizopo na mipango iliyowekwa na serikali kwa ajili ya kutoa huduma kwa kuhakikisha zinapatikana katika eneo moja (One Stop Centre).

Kwa upande wake Meneja wa ufungaji wa Mgodi wa Barrick Buzwagi, Mhandisi Zonnastral Mumbi alisema tayari eneo hilo la kongani ya Buzwagi limepatiwa usajili na serikali kwa ajili ya shughuli hiyo maalum ambapo ukamilikaje wake utachochea ukuaji wa uchumi na ajira kwa vijana hapa nchini.

Meneja wa ufungaji Mgodi wa Barrick Buzwagi, Mhandisi Zonnastral Mumbi akifafanua jambo kwa ujumbe kutoka Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) jinsi mchakato  wa kubadilisha mgodi huo uliofungwa  kuwa  Kongani ya Buzwagi unavyoendlea  wakati ulipofanya ziara kwenye eneo hilo la mgodi.

Aidha Mumbi alieleza ujumbe huo kuwa hadi kufikia sasa wawekezaji  19 wameonyesha nia ya Kuwekeza katika Kongani hiyo huku wawekezaji tano  tayari wameanza mchakato wa usajili na tayari mwekezaji mmoja ameanza uzalishaji .

Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,  Mboni Mhita, alitoa wito  kwa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) kuweka msisitizo katika kutangaza mradi mkubwa wa Kongani  Maalum la Uwekezaji wa Buzwagi ( SEZ) ambao unatarajiwa kuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo ya kiuchumi kwa Mkoa na Taifa kwa ujumla.

Meneja wa ufungaji Mgodi wa Barrick Buzwagi, Mhandisi Zonnastral Mumbi (aliyenyoosha mkono)  akiwatembeza ujumbe kutoka Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) kwenye maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya Kongani Maalum la Uwekezaji wa  Buzwagi.

Aidha,  RC Mboni alibainisha  kuwa Shinyanga ipo tayari kupokea wawekezaji kutokana na mazingira wezeshi yaliyowekwa na serikali pamoja na Mkoa kuwa na rasilimali zote muhimu kwa uwekezaji ikiwemo ardhi, upatikanaji wa maji, umeme, miundombinu ya kisasa ikiwa pamoja na barabara, uwanja wa ndege wa Shinyanga na Kahama, mtandao wa mawasiliano, na  nguvu kazi.

Meneja Utekelezaji wa Mradi  wa Kongani ya Buzwagi  kutoka Barrick, Stanley Joseph akifanya wasilisho kwa ujumbe wa maofisa waandamizi kutoka Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) uliofanya ziara mgodini hapo.

Ujumbe kutoka Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) ulipata fursa kutembelea maeneo ya wawekezaji mbalimbali kwenye eneo la Kongani Maalum la Uwekezaji wa Buzwagi.

Mwandishi Wetu, Beijing, China

Waandishi wa habari waandamizi kutoka Tanzania, Zimbambwe, Sudani Kusini, Ivory Coast and Uturuki wameshiriki mafunzo kwa vitendo nchini China hivi karibuni.

Mafunzo hayo yalihusu maendeleo ya teknolojia na mapinduzi yake ili kuleta matokeo chanya kwenye sekta ya habari na mawasiliano ya umma, na maendeleo ya taifa kwa jumla.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo  yaliyopewa kauli mbiu ya “Semina juu ya usimamizi wa vyombo vikuu vya habari katika nchi zilizo katika mpango wa ukanda na barabara” (Seminar on Senior Management of Mainstream Media in countries along the Belt and Road Initiative, -  ukanda mmoja na  njia moja ) Bw Augustino John Tendwa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) alisema mafunzo hayo yanayoendelea yamejikita katika kuleta fikira, ubunifu na matumizi ya kidigitaki katika kuleta mapinduzi ya tekolojia katika nchi za washiriki.

Afisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bw Augustino John Tendwa (wa kwanza kulia) akishiriki kwenye mafunzo ya mapinduzi ya teknolojia yanavyoweza kuleta matokeo chanya kwenye sekta ya habari na maendeleo ya Tanzania kwa jumla.

Bw Tendwa alieleza kwamba washiriki wa mafunzo hayo ya vitendo walipata fursa ya  kutembelea makao makuu ya kampuni ya kimataifa ya teknolojia – Laird Technologies – kujifunza kwa vitendo maendeleo ya kiteknolojia yanayofanyika nchini China.

Wakiwa jijini Beijing, washiriki waliweza kujionea kwa karibu namna kampuni hiyo inavyoendesha uzalishaji wa vifaa vya hali ya juu vya kielektroniki, vikiwemo vifaa vya mawasiliano ya wireless, udhibiti wa joto, mitetemo na teknolojia ya kupunguza mwingiliano wa sumaku-umeme (EMI shielding).

Picha ya pamoja ikiwaonyesha maafisa habari kutoka Tanzania, Zimbambwe, Sudani Kusini, Ivory Coast and Uturuki wakihudhuria semina ya mafunzo kuhusu teknolojia inavyoweza kutumika kuleta maendeleo kwenye sekta za maendeleo kupitia vyombo vya habari na mawasiliano ya umma.

“Kampuni kama Laird ni mfano halisi wa namna China inavyowekeza katika ubunifu na utafiti wa kisayansi kwa ajili ya maendeleo ya teknolojia duniani. Hii ni fursa ya kujifunza na kutafuta maeneo ya ushirikiano kwa maendeleo ya sekta ya viwanda na teknolojia nchini kwetu,” alisema Bw Tendwa.

Aliongeza kwamba mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo waandishi na maafisa wa serikali kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika kuhimiza maendeleo kupitia ushirikiano wa kimataifa chini ya mpango wa ukanda na barabara.

Ushiriki wa Tanzania kupitia waandishi na maafisa waandamizi kutoka taasisi za serikali na vyombo vya habari ni ishara ya dhamira ya kukuza maarifa, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na atumizi ya teknolojia katika maendeleo ya taifa.














By Staff Writer,

Barrick, in partnership with the government of Tanzania , through its Bulyanhulu mine has continued improving primary education infrastructure environment by adding more classrooms at  Kharumwa English-medium school located in Nyang’hwale District in Geita region. This 

The project, which started on April 30, 2025, is expected to be completed on September 11, 2025.

This year, Nyang’hwale District Council has received Sh100,996,200 to implement the construction of four classrooms, and purchase furniture to address the challenge of classroom shortages.

Speaking at a ceremony to receive Uhuru Torch, which coincided with the laying of the foundation stone of the school, the Leader of Uhuru Torch Race, Mr Ismail Ali Ussi, commended Barrick Bulyanhulu for continuing supporting the government to improve people’s lives through the implementation of development projects in various sectors of the economy, including education.

Leader of Uhuru Torch race,  Mr. Ismail Ali Ussi (left), officially launches the laying of the foundation stone for the construction of classrooms for an English-medium school in Nyang’hwale District, Geita Region. On the right is the District Commissioner, Grace Kingalame.

“I take this opportunity to commend all experts of the Council and Barrick Bulyanhulu Mine for working day and night to ensure Tanzanians benefit from various projects which are implemented in this district,” Mr Ussi said.

Thus, he appealed to all Nyang’hwale residents to send their children to school. “There is no longer an excuse for long distances to school because schools are built everywhere and this is due to the collaboration of the Government and stakeholders like Barrick. Indeed, Barrick, you are supportive of Hon President Dr Samia Suluhu Hassan,” said Mr Ussi.

He explained further that the partnership shown by Barrick through its mines in the country is a clear indication of productive investment for the nation, and he urged other investors to emulate Barrick spirit by contributing to community development projects.

For her part, Nyang’hwale District Commissioner, Hon Grace Kingalame, stressed the importance of working hard and continuing with the spirit of implementing development projects at high standards to meet people’s needs.


Leader of the Uhuru Torch race, Mr. Ismail Ali Ussi, greets  Barrick Bulyanhulu employees shortly after the foundation stone laying ceremony for the construction of English-medium classrooms, an event that took place in Nyang’hwale District, Geita Region.

She emphasized that Barrick, through its Bulyanhulu mine, has been closely cooperating with them in all development projects for the broader interests of the country social wellbeing.

Barrick Representative at the event, Mr Samson Mashala, who is Community Relations Officer at Bulyanhulu Mine said the mine would continue working with the Government to ensure CSR projects were well-implemented to improve people’s lives. “This project is going to address congestion, and improve a study environment,” he said.

He added that the project has reached 85%  of its completion and will boost students' learning environment and contribute to positive outcomes in the education sector in the country.

The project, implemented through the force account system, is expected to reduce the problem of classroom shortages, overcrowding of students in classrooms, and promote a friendly learning environment.

 Na Mwandishi Wetu, 

Kampuni ya Barrick nchini yenye ubia na Serikali ya Tanzania, kupitia Mgodi wake wa Bulyanhulu imeendelea kuboresha mazingira ya elimu ya msingi kwa kuongeza ujenzi wa madarasa katika shule  ya mchepuo wa Kingereza ya Kharumwa iliyopo  Wilaya ya Nyang’hwale, Mkoa wa Geita. Shule hii imejengwa kwa fedha za Uwajibikaji kwa Jamii (CSR). 

Mradi wa kuongeza madarasa  ulianza Aprili 30, 2025, unatarajiwa kukamilika September 11, 2025.

Mwaka huu Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale imepata Sh100,996,200 kwa ajili ya kutekeleza ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa, na kununua samani kwa ajili ya kuondoa changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa.

Akizungumza wakati wa kupokea Mwenge wa Uhuru ulioambatana na kuweka jiwe la msingi katika shule hiyo hivi karibuni, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Bw Ismail Ali Ussi, aliipongeza Kampuni ya Barrick Bulyanhulu kwa kuendelea kuunga mkono jitihaza za Serikali za kuboresha maisha ya wananchi kupitia uwezeshaji wa miradi katika sekta mbalimbali, ikiwemo elimu.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Bw Ismail Ali Ussi (kushoto) akifungua uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa madarasa ya shule ya mchepuo wa kiingereza, Wilaya ya  Nyang’hwale, Mkoani Geita , kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Hiyo, Grace Kingalame.

“Nachukua fursa hii kuwapongeza wataalamu wote wa Halmashauri na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa kufanya kazi usiku na mchana katika kuhakikisha Watanzania wananufaika na miradi mbalimbali inayotekelezwa katika wilaya hii,” alisema Bw Ussi.

Hivyo, alitoa wito kwa wananchi wa Wilaya ya Nhang’hwale kuwapeleka watoto waso shuleni. “Hakuna tena kisingizio cha umbali mrefu wa shuleni kwa sababu shule zinajengwa kila sehemu na hii inatokana na ushirikiano wa Serikali na wadau kama Barrick. Hakika Barrick mnazidi kumheshimisha Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan,” alisema Bw Ussi.

Alifafanua kwamba ushirikiano unatolewa na kampuni ya Barrick kupitia migodi yake hapa nchini kiashiria cha uwekezaji wenye tija kwa taifa na kuwataka wawekezaji wengine kuiga mfano wa kampuni ya Barrick kwa kuchangia miradi ya maendeleo ya wananchi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale, Mhe Grace Kingalame alisisitiza umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii na kuendelea na ari hiyo ya kutekeleza miradi ya maendeleo kwa viwango vya juu ili kukidhi mahitaji ya wananchi.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Bw Ismail Ali Ussi akisalimiana na wafanyakazi Barrick Bulyanhulu mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa madarasa kwa mchepuo wa kiingereza tukio lilifanyika wilaya ya Nyang’hwale Mkoani Geita .

Alisisitiza kwamba kampuni ya Barrick kupitia mgodi wake wa Bulyanhulu wamekuwa wakishirikiana kwa karibu katika miradi yote ya maendeleo kwa maslahi mapana ya Taifa.

Mwakilishi wa Barrick katika hafla hiyo, Bw Samson Mashala, ambaye ni Afisa Uhusiano wa Jamii katika Mgodi wa Bulyanhulu, alisema mgodi utaendelea kufanya kazi na Serikali kuhakikisha miradi ya CSR iliyoibuliwa na wananchi inatekelezwa kwa viwango na kuboresha maisha ya wananchi. “Mradi huu utaondoa shangamoto ya mrundikano wa wanafunzi katika darasa moja na kuboresha mazingira ya wanafunzi.”

Aliongeza kwamba mradi huo umefikia 85% ya ukamilishaji wake na utaongeza chachu ya wanafunzi kujifunza katika mazingira mazuri na kuchangia matokeo Chanya katika sekta ya elimu hapa nchini. 

Mradi umetekelezwa kwa mfumo wa force akaunti unatarajia kupunguza tatizo la madarasa, mrundikano wa wanafunzi wengi kwenye madarasa na kuchochea mazingira rafiki ya kujifunza.

Mwisho 

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.