DODOMA: Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) limewataka wadau wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi nchini (TVET) kutumia viwango vipya vya ubora pamoja na miongozo iliyoboreshwa ili kuzalisha wahitimu wenye ujuzi, umahiri na uwezo wa kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya uchumi na jamii.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) Dkt.Mwajuma Lingwanda.

Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa NACTVET, Bernadetta Ndunguru, ameyasema hayo wakati wa warsha ya utoaji taarifa kuhusu viwango vya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi (TVET) pamoja na miongozo mbalimbali kwa wadau wa tasnia hiyo, iliyofanyika leo Novemba 18, 2025 mkoani Dodoma.

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa NACTVET, Dk. Mwajuma Lingwanda, amesema Baraza litaendelea kuandaa, kupitia na kuboresha miongozo kadri inavyohitajika ili kuhakikisha kunakuwepo mazingira bora ya kujenga rasilimali watu yenye ujuzi stahiki kulingana na malengo ya serikali na matarajio ya soko la ajira.

Aidha, amesema wamedhamiria kuendelea kufanya warsha kama hizo mara kwa mara kadiri itakavyowezekana, kwa lengo la kukutana, kufahamiana, kujadili na kushirikiana kuhusu malengo ya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi.

Warsha hiyo imeshirikisha wadau kutoka Vyuo vya Ufundi (TET), Vyuo vya Ufundi Stadi, Vyuo vya Maendeleo ya Jamii, Shule za Sekondari Mkondo Amal, pamoja na wawakilishi na viongozi mbalimbali kutoka wizara mbalimbali ikiwemo Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.







This is the most recent post.
Older Post

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.