Arusha, Januari 29, 2026
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Dkt. Bill Kiwia, leo (Januari 29, 2026) amefanya ziara katika Ofisi za Makao Makuu ya Compassion International Tanzania (CIT) zilizopo jijini Arusha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Dkt. Bill Kiwia na Bi. Mary Lema Mkurugenzi wa Compassion Internation Tanzania (CIT) wakibadilishana hati za makubalino.Ziara hii ni moja ya mikakati ya HESLB ya kutafuta wadau wa kimkakati ili kuongeza vyanzo mbadala vya ufadhili (alternative financing) kwa wanafunzi katika elimu ngazi ya kati na elimu ya juu nchini.
Dhana hii inaendana na maono ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha vijana wa kitanzania wanafikia ndoto na malengo yao kielimu.
Aidha, katika ziara hiyo Dkt. Kiwia na Bi. Mary Lema Mkurugenzi wa Compassion Internation Tanzania (CIT) wamesaini tamko la nia ya kushirikiana (Statement of Intention to Collaborate) ili kuweka utaratibu madhubuti wa kuwatambua wanafunzi wanaotoka katika mazingira magumu ili wapewe kipaumbele katika utoaji wa Mikopo. Aidha mashirikiano haya yatalenga kutafuta vyanzo mbadala vya rasilimali fedha kwa ajili ya kuongeza wigo wa wanufaika wa mikopo na ruzuku kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum, Yatima na wanaotoka katika Kaya masikini. 


Post a Comment