Ripoti ya
Kamati ya Mifugo,Utalii, Uwezeshaji na Habari imeitaka Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar kuipitia upya mikataba ya Ujenzi wa Miundombinu na Uendeshaji wa
mitambo ya Digital kati ya Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo na
Kampuni ya AGAPE.
Akiwasilisha
Muhtasari wa Ripoti ya Kamati hiyo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi
Chukwani, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mlinde Mbarouk Juma amesema kumekuwa na
malalamiko mengi na shutuma mbali mbali kutoka kwa makundi tofauti ya
jamii kuhusiana na mradi huo hivyo Kamati haikuridhishwa na utendaji wa
Kampuni hiyo.
Amesema kuwa Wawekezaji wa AGAPE wameshindwa
kufanya kazi na kuitia hasara serikali kwa kutumia wataalamu na rasilimali za
serikali na hatimae kushindwa kukidhi mahitaji wa wananchi.
Aidha Kamati
imesikitishwa sana na mikataba ya usimamizi na uendeshaji kati ya Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na
Michezo na wawekeza wa AGAPE kwamba
haufahamiki vizuri katika utendaji wake.
“Kamati
imegundua kwamba Shirika la Utangazaji Zanzibar halikushirikishwa kikamilifu
katika maamuzi wala mapato yanaypatikana katika mradi huo wa Digital”,
alifahamisha Mwenyekiti huyo.
Kamati hiyo
pia imesikitishwa na matumizi mabaya ya Jengo la zamani la ZBC ambalo limebadilishwa
na kufanywa kuwa nyumba ya starehe kinyume na matumizi yake ambalo hukodishwa
na kufanyiwa shughuli mbali mbali za kijamii zikwemo harusi na siku ya kuzaliwa
(birth day)na kupoteza haiba yake.
Hata hivyo
Kamati hiyo imeshitushwa na taarifa za uvamizi uanoendelea katika shamba la
Mifugo Pangeni katika Mkoa wa Kaskazini Unguja na kusema kuwa vitendo hivyo
vimeshamiri katika maeneo mbali mbali ambavyo huleta hasara kwa serikali.
Akichangia
Ripoti ya Kamati hito Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Nassor Salim Ali (Jazira)
ameomba serikali kuwapatia maposho yao kwa wakati waandishi wa Habari
wanaohudhuria katika kikao cha Baraza la Wawakilishi .
Post a Comment