August 2015

DSC_0159
Mashua zenye tanga zinazojaza upepo zikichanja mbuga katika mawimbi makali kwenye bahari ya hindi kwenye fukwe za Yatch Club wakati wa mashindano ya mbio za Mashua za Mercedes Benz Cup 2015 yaliyodhaminiwa na kampuni ya CFAO Motors kwa miaka 9 sasa, yaliyomalizika mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).

Na Mwandishi wetu
KLABU ya Yatch ya Dar es salaam iliyopo Msasani jijini Dar es salaam inatafuta fedha kuwezesha washiriki wake wanne katika mbio za mashua za kisasa kwenda kushiriki michezo ya All Africa games itakayofanyika baadae mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa katika mahojiano na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa patashika ya siku mbili ya mbio za mashua za kisasa zinazosukumwa na matanga yanayopokea upepo na zile ambazo hazina.

Mbio hizo ambazo zimedhaminiwa na CFAO Motors kupitia bidhaa yake ya Mercedes Benz Cup 2015 zilishirikisha watu 30 wakiwa ndani ya mashua 15 za aina tofauti.
Ofisa mmoja wa klabu hiyo Andrew Bogd alisema kwamba ushiriki wa watanzania katika mashindano ya kimataifa hautakuwa wa kwanza kwani wameshashiriki katika mchezo hiyo Afrika Kusini na Morocco mwaka jana.

Alikuwa akizungumzia mafanikio ya klabu hiyo katika kuufanya mchezo huo kujulikana kwa wazawa wa Tanzania ambao wanapenda michezo ya katika maji hasa ya kukimbiza mashua.
Katika mbio hizo ambapo kulikuwa na washindi takribani zaidi ya saba kwa kuzingatia daraja mshindi wa mashua zenye tanga inayojaza upepo alikuwa Al Bush akishirikiana na Robert Fine. Mshindi wa Pili wa ngazi hiyo alikuwa Michael Sulzer aliyekuwa katika mashua na Andreas Schmidt na ushindi wa tatu ulikwenda Roland Van de Ven akiwa na Peter Scheren.
 
DSC_0162
Washiriki wakipambana na mawimbi wakati wa mashindano ya mbio za mashua za Mercedes Benz Cup 2015 yaliyomalizika mwishoni mwa juma jijini Dar.
 
Washindi hao walikabidhiwa tuzo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa CFAO Motors, Eric Potin ambaye safari hii katika udhamini wao walikuwa wanatangaza gari la Mercedes GL –CLASS.
Washindi wengine katika kategori ya mashua za kisasa za kawaida walikuwa Andrew Boyd akiwa na Max Pennan Kok wakati washindi wa pili walikuwa David Scott akiwa na Cassie Dietliefs na washindi wa tatu walikuwa Cyrille Girardin na Gemma Quickenden.

Mercedes Benz ambao wanadhamini mashindano mbalimbali ya mashua za kisasa za ngazi mbalimbali duniani, wamekuwa wakidhamini michuano hiyo ya Dar es salaam kwa mara ya 9 sasa.
Msemaji wa Yatch Club, Bogd akizungumzia michuano hiyo iliyokuwa ya siku mbili alisema iliyiojaa changamoto kubwa hasa siku ya kwanza ambapo mabahari walioonesha umahiri kukabiliana na upepo mkali na kuongoza mashua zao katika muda waliopaswa kuufikia wakishindana katika mfumo wa juu hadi chini au kwenda kwa mfumo wa pembetatu.
Siku ya kwanza ya mbio hizo Jumamosi upepo ulivuma kwa kasi ya noti 20 kwa saa.

“ …haikuwa kazi rahisi siku ya kwanza. Lakini hiyo ndio raha ya mchezo huu.Bahari inapokuwa ‘ngumu’ ambapo waendesha mashua hao ni kama vile wanataka kutemwa kutoka kwenye mashua, hivyo wakilazimika kutumia maarifa yao kuidhibiti, ndio raha ya mchexzo wenywe” alisema Bogd.
 
1st spinnaker boat - Al Bush and Robert Fine
Mshindi wa mashua zenye tanga inayojaza upepo Al Bush akishirikiana na Robert Fine wakirejea katika fukwe za Yatch Club jijini Dar es Salaam wakati wa mashindano hayo ya mbio za Mashua za Mercedes Benz yaliyodhaminiwa na Kampuni ya CFAO Motors kupitia bidhaa ya Mercedes Benz Cup 2015 mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam.

Washiriki walilazimika kufanya hatua saba za mbio hizo ambapo kila hatua ilikuwa ni dakika 40.
Pamoja na washiriki hao kupewa zawadi ofisa huyo alitaka watu zaidi kushiriki katika mashindano hayo ambayo kwa jinsi siku zinavyoenda watanzania wengi zaidi wanafika kujifunza mashindano hayo ambayo yanahitaji maarifa na pia kuzingatia usalama kwa kutumia mashua za kisasa za aina tofauti.

Katika mashindano hayo huwa kunakuwa na mashua kubwa na nyingine za kati na ndogo.
Aidha alisema kwamba wanaanzaa kufundisha mchezo huo kuanzia miaka minane na kwamba huwezi kufundisha udhibtii wa mashua kwa mtu mzima kwani kuna hatua mbalimbali zinazojenga uzoefu wa mchezo wenyewe.

Alisema watoto ambao sasa wameshapita umri wa kuendesha mashua za kati wameshaanza kushiriki na kwamba wanatoa changamoto kubwa kwa washiriki wenye umri mkubwa katika mchezo huo.
Dar es Salaam Yacht Club ambayo hufanya mashindano ya mashua ya kisasa zikiwemo catamaran, Cadets, yachts na Lasers ilianzishwa mwaka 1933 katika bandari ya Dar es salaam, mwaka 1967 ilihamishiwa ilipo sasa la Leopard’s Cove, ghuba ya Msasani.

Panmoja na kufanya shughuli za mbio za mashua pia wana bwawa la kuogelea, baa na mgahawa.

IMG_2786
Ofisa Mtendaji Mkuu wa CFAO Motors, Eric Potin aliyeipa mgongo 'camera' akijaliana jambo na Mkurugenzi wa fedha wa CFAO Motors, Aldo Pagani (aliyesimama kushoto katikati) pamoja na Meneja Masoko wa CFAO Motors, Shekha Said. Wengine ni maofisa wa Yatch Club jijini Dar, kabla ya zoezi la kukabidhi vikombe na zawadi kwa washiriki.

Spinnaker Winners, Al Bush and Robert Fine
Ofisa Mtendaji Mkuu wa CFAO Motors, Eric Potin (kushoto) akikabidhi kikombe kwa washindi wa kwanza wa mashindano ya Mercedes Benz Cup 2015, Al Bush aliyeshirikiana na Robert Fine, huku Mkurugenzi wa fedha wa CFAO Motors, Aldo Pagani akishuhudia tukio hilo.

MercedesCupWinners, Al Bush and Robert Fine with Andrew Boyd and Max Pennan Kok
Washindi wa Mercedes Benz Cup 2015, Al Bush, Robert Fine waliosindikizwa na Andrew Boyd wa Yatch Clup (wa pili kushoto) pamoja na Max Pennan Kok wakifurahia kikombe chao katika picha ya pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa CFAO Motors, Eric Potin (kushoto) na Mkurugenzi wa fedha wa CFAO Motors, Aldo Pagani (kulia).

IMG_2908
Washindi wa Mercedes Benz Cup 2015, Al Bush, Robert Fine katika picha ya pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa CFAO Motors, Eric Potin (kushoto), Mkurugenzi wa fedha wa CFAO Motors, Aldo Pagani (wa tatu kulia), Meneja Masoko wa CFFAO Motors, Shekha Said (wa pili kulia) pamoja na Meneja Mauzo wa matairi CFAO Motors, Pietre Van Eeden (kulia).
Spinnaker Runner Up Michael Sulzer
Ofisa Mtendaji Mkuu wa CFAO Motors, Eric Potin akimpongeza mchezaji wa mashindano ya mbio za mashua za Mercedes Benz Cup 2015, Michael Sulzer kwa ushiriki wake.
Non-Spinnaker Runners Up David Scott and Casey Dietliefs
Mshindi mdogo kuliko wote wa mashua za kawaida shindano la Mercedes Benz Cup 2015, Casey Dietliefs (katikati) aliyeshirikiana na David Scott (kushoto) wakipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa fedha wa CFAO Motors, Aldo Pagani (kulia).

DYC Commodore Brian Grant and CFAO Aldo Pangani
Mkurugenzi wa fedha wa CFAO Motors, Aldo Pagani (kulia) akisaidiwa na Mwenyekiti wa Dar Yatch Club, Brian Grant wakati akikata utepe kuzindua gari iliyotolewa na kampuni ya CFAO Motors kwa Dar Yatch Club kama shukrani ya ushirikiano baina ya CFAO Motors na Dar Yatch Club.

IMG_2839
Mkurugenzi wa fedha wa CFAO Motors, Aldo Pagani na Meneja Masoko wa CFAO Motors, kwa pamoja wakizindua gari hiyo wakati wa mashindano ya Mercedes Benz Cup 2015.

DYC Commodore Brian Grant
Mwenyekiti wa Dar Yatch Club, Brian Grant akiwasha gari hiyo kuashiria uzinduzi rasmi.

IMG_2804
Mmoja wa wananchama wa Yatch Club akiangalia gari aina ya Mercedes Benz GL Class iliyowekwa katika viwanja vya Yatch Club kama nembo ya udhamini wa mashindano ya mbio za mashua za Mercedes Benz.

IMG_2823
Pichani juu na chini ni washiriki wa mashindano ya mbio za mashua za Mercedes Benz na familia zao wakisubiri zoezi la kukabidhiwa zawadi na vikombe kutoka kwa wadhamini wa mashindano hayo CFAO Motors mwishoni mwa juma.

IMG_2824   IMG_2913
Washiriki wa mashindano ya mashua ya Mercedes Benz Cup 2015 katika picha ya pamoja.

TANGAZO LA KUONGEZA MUDA WA UDAHILI
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwaarifu wahitimu wa stashaada kuwa limeongeza muda wa kutuma maombi ya Mafunzo ya  Shahada kwa  awamu ya tatu  hadi tarehe 31 Agosti 2015.
KUMBUKA kuwa mfumo utajifunga ifikapo tarehe tajwa hapo juu. Watu wote wenye sifa za kujiunga na mafunzo haya wakiwamo wenye matokea ya muda (provisional results) wanaombwa kuitumia fursa hii muhimu kama inavyoelekezwa kwenye tovuti ya Baraza :bofya hapa
Imetolewana: 
Baraza la Taifa la ElimuyaUfundi (NACTE)
8 Agosti 2015

PUBLIC NOTICE
The National Council for Technical Education (NACTE) would like to inform all graduates for Ordinary Diploma (NTA Level 6) or Equivalent that the deadline for application into Bachelor Degree programmes through the Central Admission System (CAS) has been extended to 31st August 2015.
NOTE that the system will automatically close after the mentioned deadline. All eligible applicants including those with provisional results are therefore advised to use this opportunity to apply for admission. Via council website by click here
By
National Council for Technical Education (NACTE)
8 August 2015

To Manchester United:
I write this note to thank all the Manchester United family for the great support received during the year I've been part of this Club.
 
When Manchester United chose me as part of their team I felt extremely honoured because I knew what this Club means and how it trusted me.
 
Nevertheless, I'm aware things didn't work as we all expected and believe me, I feel really sorry about it. However in the career of a football player sometimes the unexpected and unwanted may happen.

Angel Di Maria
"I'm really sorry about it": Di Maria penned an open letter to fans



Anthony and Catherine Costner
Shot dead: Anthony and Catherine Costner
A young couple were found shot dead in their car, with their toddler alive in the back seat, after responding to a call for help from someone they knew, police said.

Anthony Costner, 24, and wife Catherine, 22, from Georgia, were found inside the car, which was in a ditch with its headlights on, around 2am on Thursday.

The young dad had been shot multiple times and died at the scene, in Powder Springs, while Catherine was taken to hospital with a gunshot wound but later died,

The couple's three-year-old daughter was also found in the car with them, but was unharmed.
Anthony and Catherine Costner

Anthony Costner, 24, and wife Catherine, 22, were gunned down in front of their three-year-old daughter

Family: The couple's daughter was in the car with them
Catherine’s mother said her daughter received a call for help in the middle of the night from someone she knew.
Cynthia Quinn told WXIA: "When they went to help these people, for whatever reason, a gun was pulled and my son-in-law and my daughter are now dea.

“Her husband was shot in the face, the head and the hand. She was shot in the stomach, all in front of my granddaughter.”

Catherine’s brother told the Atlanta Journal-Constitution the couple seemed nervous as they left their home for the last time.
Police have not named any suspects and are investigating the deaths as a homicide.

Source www.dailymirror.co.uk

Januzaj set for Sunderland switch?

Sunderland are in talks with Manchester United over a possible loan deal for Adnan Januzaj.

 

Parish issues Palace warning

Crystal Palace are scaring off suitors interested in Yannick Bolasie and Dwight Gayle by putting huge prices on their head.
Chairman Steve Parish wants well over £20million for winger Bolasie and MirrorSport understands Parish has slapped a £10m price tag on striker Gayle’s head.

Soldado offered Spurs lifeline
Mauricio Pochettino wants to keep Roberto Soldado.
Tottenham boss Pochettino insists the Spanish striker remains part of his plans.

 Barton open to Newcastle return
Joey Barton has admitted he would love to one day play for Newcastle United again - but only IF the powers at the club change their approach.

 Where art thou, Victor?
 David De Gea took a full part in Manchester United training as they prepare for their Premier League opener with Tottenham on Saturday - but fellow keeper Victor Valdes was absent.

 Karim with a chance  
Arsenal haven’t given up on landing Karim Benzema despite Rafa Benitez’s claims he is staying at Real Madrid.


SALAH DEAL DONE?
It seems as though a deal to take Chelsea midfielder Mohamed Salah to Roma is on the verge of completion, judging by the player’s social media activity.


PAPER TALK

  • Tottenham want to strengthen their attack by signing £15m Charlie Austin from QPR and they plan to offload Roberto Soldado and Emmanuel Adebayor before making their move. (Daily Mirror)  
  •  Manchester United have been cleared to sign Pedro in a £22m deal but Barcelona will not release him until after their European Super Cup clash with Sevilla. (Daily Mail) 





















By Staff Writer 

BARCLAYS Bank Tanzania has started a one week training to its 100 Corporate Clients on risk management, deliverance, foreign exchanges rates, corporate cash flow and their understanding on local and international market with the aims of empowering them to protect their business when there is fluctuation of the shilling against dollar in the market.
 
Speaking to reporters in a news conference yesterday in Dar es Salaam, Head of Trading and Treasury Execution, Idd Davis said that the bank’s will conducted a one week training to corporate customers to make them understandings the market and protect their business.

He said that the training will support a client in managing the risks associated with foreign exchange hullabaloo and interest rate volatility and to provide them with sustainable solution in their businesses.

“the training will be very useful to them because it will make them understands the local and international market and expands the knowledge on how to mitigate the risk in the course of business,” he said  
 Davis added that the seminar is also looking forward at inculcating the culture of understanding the movements of exchange rates and how to deal with them without discouraging their business.
 
He said that the training will also touch on the recent fluctuation of the dollar against the shilling and how business people can cope and control the situation at the local level without disturbing the business and cash flows.
“Trading and treasury department always support clients with the structuring and execution of tailor made solutions, post trade support and analyzing the existing positions,” he added 

On his part, the facilitator of Training, Peter Skerritt from South Africa said that the growing trend of pricing goods and services for Tanzanians in US dollars its affects the country’s economy and consumers in the country.
He stated that ’dollarisation’ of the local economy had contributed heavily to the steady weakening of the shilling in the financial market affects business people and local citizens.

A facilitator at the event, a South African based derivatives and financial risk specialist said that Barclays always conducted training to its clients in East and Central Africa and build their capacity on the international financial markets.

He added that Tanzanians should push for increased production of goods and services for export, to earn more foreign currency and subsequently strengthen the shilling.

Skerritt underscored that the East African Community through its ambitious to have a single currency in the region will stabilize the shillings in both member states and fostering social and economic development.

Barclays Bank has 11 branches in Dar es Salaam alone and a network of 44 automated teller machines plus 11 more branches countrywide.

Ends

IMG_1116
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akimkaribisha ofisini kwake Mwakilishi wa mtandao wa FANPRAN, Sithembile Ndema kwa ajili ya kusaini kitabu cha wageni kabla ya kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).

Na Mwandishi wetu
JUMLA ya dola za Marekani milioni 802.15 zimetolewa na nchi wahisani katika kusaidia mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi katika kipindi cha miaka miaka mine iliyopita.
Hayo yalielezwa na Mkurugenzi wa Kituo cha Mabadiliko ya tabia nchi Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Profesa Pius Yanda wakati alipokuwa akitoa mada kuhusu utafiti alioufanya yeye na wenzake kuhusu mchango wa uwezeshaji mapambano hayo kutoka nchi marafiki.
Alisema kiasi hicho cha fedha ni sawa na wastani wa dola milioni 200 kila mwaka zilizokuwa zikipelekwa katika sekta mbalimbali nchini.
Alisema utafiti walioufanya ambao ulilenga kuona kiasi cha fedha zilizotoka kwa wafadhili kwa ajili ya miradi mbalimbali ni awamu ya pili ya utafiti ambao awali ulijikita kuona bajeti ya taifa inavyotumika kukabili mabadiliko ya tabia nchi.
Profesa Yanda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere cha Mazingira amesema kwamba sehemu kubwa ya fedha ipo katika miradi ya maendeleo ambayo utekelezaji wake pamoja na kutosema kwamba unakabili mabadiliko ya tabia nchi, matokeo yake ndiyo yanayobainisha.
IMG_1128
Mkurugenzi wa Kituo cha Mabadiliko ya tabia nchi Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Profesa Pius Yanda (kushoto) akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (wa pili kushoto) huku wengine wakishuhudia zoezi hilo, Kulia ni Mwakilishi wa FANPRAN, Sithembile Ndema na wa pili kulia Mtafiti msaidizi kutoka ESRF, Ian Shanghvi.

Alitolea mfano kuwa miradi ya kusambaza umeme vijijini ( REA) nchini ambayo ilipata fedha nyingi katika miaka ya 2011 na 2012 ni miradi ya maendeleo lakini hatima yake ni kuzuia ukataji hovyo wa miti kwa ajili ya nishati.
Akifafanua fedha hizo zaidi alisema kwamba Tanzania mwaka 2010 jumuiya ya kimataifa zilitoa dola za Marekani milioni 171.93, mwaka 2011 dola za Marekani milioni 225.35, mwaka 2012 dola za Marekani milioni 229.74 na mwaka 2013 Tanzania ilipata dola za Marekani milioni 175.14.
Utafiti huo ambao uligharamiwa na COMESA, EAC na SADC umewasilishwa katika mkutano wa kitaifa wa uwezeshaji wa miradi ya kukabili tabia nchi kwa mfumo wa ndani ambapo pia Mwakilishi wa mtandao wa FANRPAN, Sithembile Ndema alikuwepo kuelezea maana ya mikutano ya kisera katika nchi zinazounda mtandao huo.
Mtandao huo ambao ulianzishwa mwaka 1994 baada ya mkutano wa mawaziri wa kilimo wa nchi za SADC, EAC na COMESSA na makao makuu yake kuwa nchini Zimbabwe ulianza kazi mwaka 1997 na sasa makao makuu yapo nchini Afrika Kusini.
Mtandao huo umelenga kuwezesha mataifa ya Afrika kuendesha kilimo na ufugaji unaozingatia mabadiliko ya tabia nchi na hivyo kutunza mazingira na kuongeza tija.
Mikutano ya aina hiyo pia inafanyika Uganda, Ethiopia, Kenya na Zambia.
Profesa Yanda alisema kwamba pamoja na fedha hizo kuonekana nyingi kiukweli ni haba kutokana na hali halisi ilivyo sasa na hasa ikizingatiwa kwamba kunatakiwa pia fedha za mabadiliko tabia nchi yenyewe badala ya kutumia miradi ya maendeleo ambao matokeo ni kukabili mabadiliko ya tabia nchi.

IMG_1149
Mshehereshaji Hanif Tuwa kutoka ESRF, akitoa mwongozo wa yatakayojiri kwenye mkutano wa kitaifa wa kujadili sera ya uwezeshaji kifedha mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za ESRF.

Alisema takwimu walizopata kuhusu fedha zilizofika nchini kutoka katika jumuiya ya kimataifa zililingana na taarifa zilizopo Hazina na kuonesha kwamba fedha hizo zilienda kutumika katika makadirio yaliyokusudiwa.
“tofauti iliyopo ni tafsiri ya miradi ya mabadiliko ya tabianchi. Miradi ya maendeleo, inatamkwa kama miradi ya maendeleo lakini ukiangalia mwishoni ni miradi hiyo kusaidia katika kukabili mabadiliko ya tabia nchi” alisema katika mahojiano baadae na na waandishi wa habari.
Alisema kama Mkurugenzi wa Kituo cha mabadiliko ya tabia nchi anashauri serikali kuhimiza wananchi wake kuendelea kusimamia mazingira vyema huku wakulima na wafugaji wakisikiliza maofisa ugani kwa ajili ya kuwa na kilimo na ufugaji bora usioharibu mazingira..
Alisema tafiti mbalimbali zinaonesha kuwepo kwa athari kubwa ya mabadiliko ya tabia nchi ambapo sasa hata sehemu za baridi za nyanda za juu zimeanza kuwa na magonjwa ya Malaria huku wakulima wakiwa hawajui muda wa kupanda kutokana na mabadiliko ya joto na pia unyeshaji wa mvua.
Alisema pia nyanda za juu sasa zinakabiliwa na wadudu waharibifu wa mazao vitu ambavyo awali havikuwepo.
Alisema kwamba bado taifa linahitaji kufanya tafiti nyingi zaidi na kuzitumia kuelimisha umma kuhusu nini kinatokea na nini kinastahili kufanywa kukabili mabadiliko hayo.
IMG_1174
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akihutubia mkutano wa kitaifa wa kujadili sera ya uwezeshaji kifedha mabadiliko ya tabia nchi. Mkutano huo umefanyika jana jijini Dar es salaam katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za ESRF na kujadili taarifa ya utafiti uliofanywa kwa miaka minne kuhusiana na uwezeshaji. 

Mkutano huo wa kitaifa ulifunguliwa na Mkurugenzi wa Taasisi huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) Dk. Tausi Kida ambaye alisema lengo la mkutano huo ni kuchambua utafiti uliofanywa na kuja na maazimio yatakayosaidia kuboresha kilimo na kuhifadhi mazingira katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.
Aliwaambia washiriki kuiangalia kwa makini tafiti ya Profesa Pius Yanda na kuhakikisha kwamba wanakuwa na uelewa wa maudhui na kuwezesha kutoa dira ya utekelezaji katika siku za usoni.
Alisema wakati taifa linajipanga kutekeleza mpango wake wa maendeleo wa kuelekea katika uchumi wa viwanda suala la mabadiliko tabia nchi haliwezi kuachwa na hivyo wajumbe wa mkutano walitakiwa kuangalia na kuja na mapendekezo yao.
Mapendekezo hayo ni pamoja na kuwa na kilimo na ufugaji wenye tija unazoingatia ufanisi katika hifadhi ya mazingira na namna uwezeshaji wa ndani unavyoweza kuendeleza mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.
Alisema ni muhimu kilimo kuwa ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
ESRF ni taasisi yinayojishughulisha na tafiti mbalimbali za jiuchumi na kijamii zinazotoa mwelekeo wa utekelezaji wa sera na kanuni mbalimbali za maendeleo na ustawi wa jamii.
Pmaoja na kuratibu mkutano huo pia ilitoa nafasi ya ukumbi wake kutumika na kutoa mwelekeo wa mkutano na umuhimu wake katika mpango wa pili wa maendeleo wa taifa ambao unatakiwa uzingatie mabadiliko ya tabia nchi.
IMG_1161
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akisoma hotuba na kuwakaribisha washiriki wa mkutano wa kitaifa wa kujadili sera ya uwezeshaji kifedha mabadiliko ya tabia nchi. Kulia ni Mwakilishi wa FANPRAN, Sithembile Ndema na kushoto ni Mkurugenzi wa Kituo cha Mabadiliko ya tabia nchi Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Profesa Pius Yanda.

IMG_1203
Mwakilishi wa FANPRAN, Sithembile Ndema akielezea mradi wa COMESA wa uwezashaji wa ndani wa fedha kwa ajili ya mabadiliko ya tabia nchi katika mkutano huo.
IMG_1249
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (katikati) na Mkurugenzi wa Kituo cha Mabadiliko ya tabia nchi Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Profesa Pius Yanda (kulia) wakifuatilia ka umakini 'presentation' ya Mwakilishi wa FANPRAN, Sithembile Ndema (hayupo pichani).
IMG_1318
Mkurugenzi wa Kituo cha Mabadiliko ya tabia nchi Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM), Prof. Pius Yanda, akitoa mada ya ufadhili wa kimataifa wa uwezeshaji wa kifedha wa mabadiliko ya tabianchi Tanzania katika mkutano huo.
IMG_1370
Pichani juu na chini washiriki wakichangia mawazo yao kuhusu namna sera ya uwezeshaji kifedha mabadiliko ya tabia nchi inavyopaswa kuwa katika mkutano huo.
IMG_1343
IMG_1150
Pichani juu na chini ni washiriki kutoka taasisi mbalimbali za serikali na zisizo za serikali, watafiti, na wadau wa maendeleo waliohudhuria mkutano wa kitaifa wa kujadili sera ya uwezeshaji kifedha mabadiliko ya tabia nchi.
IMG_1155
IMG_1231 IMG_1260
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano wa kitaifa wa kujadili sera ya uwezeshaji kifedha mabadiliko ya tabianchi.
IMG_1256
Picha ya pamoja ya washiriki.


By Waandishi Wetu, Mwananchi
Dar es Salaam. Mkutano Mkuu wa Chadema, kwa kauli moja, umempitisha waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuwa mgombea wake wa urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, papo hapo mwanasiasa huyo akasema Chadema itachukua nchi asubuhi.
Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward
Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa (katikati) akiwa ameshikana mikono na mgombea mwenza, Juma Duni Haji (kushoto) baada ya wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho  kuwapitisha kugombea nafasi hizo, Dar es Salaam jana. Kulia ni mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Sharif Hamad Picha na Emmanuel Herman
Lowassa alipitishwa kuwania urais kwa mwavuli wa Ukawa kwa kuungwa mkono na vyama vyote katika “safari ya uhakika”.
Mbunge huyo wa zamani wa Monduli, aliyejiunga na Chadema Julai 28 akitokea CCM, akiwa na mgombea mwenza, Juma Duni Haji aliyejiunga pia na Chadema akitokea CUF, walipitishwa kwa kupigiwa kura ya ‘ndiyo’ na wajumbe wote wa mkutano mkuu huo uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
Kabla ya kujiunga na Chadema, Duni alikuwa Makamu Mwenyekiti wa CUF – Zanzibar na Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).
Kiongozi huyo amelazimika kujiuzulu nyadhifa zote ili kuwa mgombea mwenza wa Lowassa kutokana na sheria za vyama vya siasa na uchaguzi nchini kutaka mgombea urais na mgombea mwenza watoke chama kimoja cha siasa.
Lowassa aliyekuwa amevaa shati jeupe na suruali nyeusi alifika ukumbini hapo saa 5.25 asubuhi akiwa katika msafara wa magari manane na kupokewa na mamia ya wajumbe wa mkutano huo huku wakiimba, ‘rais. rais, rais, rais”.
Katika msafara huo, Lowassa akiwa na familia yake, aliambatana na waliokuwa makada wa CCM ambao pia walijiunga na Chadema akiwamo aliyekuwa mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Mgana Msindai.
Wengine ni aliyekuwa Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk Makongoro Mahanga, aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye, huku Naibu Katibu Mkuu wa  Chadema – Zanzibar, Salum Mwalimu akisema kuwa viongozi hao wamepewa kadi za chama hicho kwa niaba ya wenzao watakaojiunga na Chadema siku chache zijazo.
Mkutano huo uliokuwa na shamrashamra za kila aina, ulihudhuriwa na viongozi wakuu wa vyama vinavyounda Ukawa; NCCR–Mageuzi, NLD na CUF isipokuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa bado amewekwa kando wakati mchakato huo wa kwenda Ikulu ukiendelea.
Wengine waliohudhuria ni mabalozi na wawakilishi wa nchi mbalimbali, viongozi wa vyama vya siasa vya nchi jirani, wabunge na viongozi wa dini, akiwamo Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zacharia Kakobe na Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta), Gratian Mukoba.
Lowassa: Tutachukua nchi asubuhi
Akihutubia mkutano huo mkuu wa Chadema kwa mara ya kwanza, Lowassa alisema chama hicho kupitia Ukawa kitachukua nchi mapema asubuhi Oktoba 25.
Alisema Watanzania wanajua kuwa Chadema wamepania, wamejipanga na wana uhakika wa kukamata dola mwaka huu.
“Nilianza na safari ya matumaini, lakini sasa nasema hii ni Safari ya Mabadiliko nje ya CCM, tutakamata nchi mapema kabisa asubuhi,” alisema Lowassa.
Hata hivyo, Lowassa alitahadharisha kuwa kuing’oa CCM ni kazi kubwa kama hakutakuwa na mipango na malengo huku akisema hakujiunga na chama hicho akiwaza kushindwa na kwamba hana msamiati wa kushindwa na wala hakwenda kwa bahati mbaya, bali alijiridhisha na kukubaliana na familia yake hadi kufikia uamuzi huo.
“Nimekuja Chadema nikijua kuwa kazi ya chama ni kushika dola na kama si hivyo, hakuna sababu ya kuwa chama, nimejiandaa vizuri kushika dola… watu wanasema Chadema haiwezi, Tanu ilipewa nchi ikiwa na miaka saba, sasa ninyi mna miaka 23,” alisema na kushangiliwa.
Aliongeza,“Najua kazi ni kubwa na mnajitolea, ndiyo maana chama kina nguvu na moyo kama CCM ya zamani si ya sasa, ndiyo maana tumeikimbia,” alisema Lowassa.
Alisema atapita kila jimbo kutengeneza mipango ya ushindi kwa kufanya kampeni za kistaarabu huku akionya... “Mradi wasiibe kura zetu.”
Duni aipiga kijembe CCM
Mgombea mwenza, Duni Haji aliirushia kijembe CCM kuwa inafanya wananchi wawe maskini ili iendelee kuwatawala.
Akizungumza baada ya kuteuliwa na chama hicho kuwa mgombea mwenza, Duni alisema, CCM haiwezi kuwasaidia wananchi kutoka kwenye umaskini kwa sababu sera yao ni umaskini.
“Miaka ya 70 hatukuwa na neno changudoa, jambazi wala panya road. Haya yamekuja kutokana na kushindwa kwa utawala wa CCM. Ukawa tumedhamiria kuchukua madaraka ya nchi hii ili kuleta mabadiliko,” alisema.
Alisema wananchi wamejenga imani na matumaini kwa makubaliano yaliyofanyika jangwani, walipotia saini hati ya makubaliano inayoruhusu vyama kukubaliana kusimamisha mgombea mmoja kwenye kila nafasi ya uongozi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Akimzungumzia mgombea urais, Duni alisema: “Siyo jambo rahisi kufanya uamuzi mgumu kama aliofanya Lowassa. Wengi bado wapo CCM licha ya kuwa hawapendi mfumo wa chama chao, alichokifanya Lowassa ni ujasiri mkubwa.”
Hata kwake, alisema halikuwa jambo rahisi kuihama CUF na kujiunga na Chadema. Alisema kuwa alikubaliana na viongozi wake, Profesa Lipumba na Maalim Seif Sharif Hamad aende Chadema ili Ukawa ilete ukombozi katika Taifa.
“Profesa Lipumba ananipenda sana na ananikubali haswa… na anajua kuwa hiki ni kifaa. Lakini alikubali nijivue uanachama wa CUF ili niende Chadema kuongeza nguvu ya kuleta mabadiliko, nina imani Ukawa tutashika dola ifikapo Oktoba 25,” alisema.
Alisisitiza kuwa Ukawa ndiyo ufumbuzi wa matatizo ya Watanzania akisema umoja huo unaungwa mkono na wananchi wengi, hivyo hana shaka kwamba utashinda katika uchaguzi ujao.
“Nilikuwa mwanachama wa ASP nilipokuwa kidato cha pili. Nilipoona mambo yanabadilika nami nilibadilika. Lengo kuu la kupigania uhuru lilikuwa ni Mwafrika kumtawala Mwafrika mwenzake ili amlinde, lakini lengo hilo sasa limepotea.
“Ninashangaa kuona askari wa kimaskini aliyepewa bunduki kuwalinda wananchi, anageuka na kuwapiga risasi maskini wenzake, huu ni udhalimu uliotengenezwa na Chama cha Mapinduzi,” alisema.
Ajenda zabadilika
Awali, Mbowe alitangaza kubadili ajenda za mkutano huo ili kuifanya siku ya jana kuwa ya kihistoria, ikiwa ni pamoja na kuwahoji wajumbe wa mkutano kama wanataka kupiga kura ya ‘ndiyo’ au ‘hapana’ au kura ya siri kupitisha mgombea urais na mgombea mwenza na kujibiwa, “Tunataka kura ya ndiyo na hapana.”
“Tunapopigania ndoto ya Taifa lazima tukubaliane kushirikiana na ili ndoto itimie tunamhitaji kila Mtanzania ambaye yupo tayari kushiriki nasi kutafuta ndoto hiyo, waliopo CCM na wasio na vyama vya siasa. Tunahitaji Watanzania wa makabila yote, dini na rangi zote,” alisema Mbowe.
Alisema Mungu yupo na Chadema na katika aina yake ya utendaji wa miujiza kila jambo linalotokea katika chama hicho linatokana na mpango wake.
“Ili tulibadilishe Taifa hili, hatuwezi kujenga uadui wa kudumu. Ili tuyapate mabadiliko ya kweli tunamhitaji kila mmoja ambaye Mungu amempa karata zake, nguvu zake na kupewa kidogo na kikubwa na kwa pamoja tutaunda jeshi la pamoja,” alisema.
Alisema katika safari hiyo wakubaliane kuwa ndoto ya Taifa ni kubwa kuliko mahitaji ya kila mmoja.
“Ushirika wetu una maana pale ambapo tutakubaliana kila mmoja wetu kwa nafasi yake, kuanzia udiwani, ubunge na urais na kazi nyingine yoyote ya kuongoza Watanzania.
“Haya mambo (ya kusimamisha mgombea mmoja) yanahitaji kujitoa, ndoto ya Taifa haiwezi ikatimia kama kila mmoja atatanguliza matakwa yake binafsi. Fursa ni nadra na hiyo fursa inayopatikana kwa u-nadra huo isipotumika historia itatuhukumu,” alisema.
Alisema viongozi wa Chadema ni lazima wajitolee ili kwa pamoja, kupitia Ukawa waweze kufika safari yenye malengo ya kutimiza ndoto ya Taifa.
“Lakini ndoto hii si ya mtu mmojammoja, familia mojamoja au ukoo. Ni ndoto ya Taifa,” alisema.
Alisema Chadema kinapokea wanachama kutoka chama chochote wenye malengo safi na kuwa kwa miaka 25, kimepigana kuingia Ikulu huku viongozi wake wakijitolea.
“Kwenye safari hiyo ya miaka 25 wapo waliokufa, waliopata vilema, waliofukuzwa kazi kwa kusimamia walichokiamini, waliofungwa magerezani na wapo waliohama nchi. Safari hii haikuongozwa na Chadema pekee, iliongozwa na vyama vyote vinavyounda Ukawa.
“Wapo tunaowaita magamba nao wakaamua kimagamba magamba wafunge safari ya matumaini. Wakafunga safari yao wakiitafuta haki na kweli katika nchi hii,” alisema Mbowe.
Alisema walioanza safari ya matumaini waliongozwa na dhamira kwa lengo la kujitoa unyonge na kujifungua minyororo ya chama chao, ili kuitafuta haki na dhamira yao nje ya chama chao.
“Chadema na Ukawa nchi nzima, watu hawa (walioanza safari ya matumaini) hatuna haki na sababu ya kuwahukumu, tuna kila sababu ya kuwatia moyo na kuwaunga mkono na kuwakaribisha miongoni mwetu ili ndoto ya Taifa hili ikatimie,” alisema.
Alisema wanaojiunga Chadema na waliopo ndani ya chama hicho wote ni binadamu na kwamba watakaojiunga na chama hicho na Ukawa wataishi kama wanavyoishi wanachama wa vyama vinavyounda umoja huo.
“Sisemi wanaokuja Chadema hawana dhambi wote, hata sisi wana–Chadema tuna dhambi zetu, uongo?” aliuliza Mbowe na kujibiwa na wanachama, ‘ndiyooo.’
“Sisi ni nani, hiki ni chama cha siasa na siasa ni watu. Chama cha siasa si mahakama.”
Alisema kuna kila sababu ya chama hicho kujenga utamaduni uliozoeleka wa kuwakaribisha Watanzania wengine katika chama hicho ambao wanaamini kupitia Chadema na Ukawa kuwa ndoto ya Taifa inakwenda kutimia.
Alisema Chadema imejengwa kwa kufuata misingi ya kidemokrasia na kifamilia na ndani ya chama hicho, hakuna aliye mkubwa kuliko mwingine.
“Tukikubaliana kusonga mbele tunasonga mbele. Mnaokuja Chadema tusaidieni kulinda umoja wetu na yale mabaya mliyokuwa nayo katika chama chetu cha zamani tumewasamehe na huku mtuletee mazuri yote mliyopata katika chama chenu cha zamani...”
“Vyama vya siasa ni vyombo vya uchaguzi ni magari na madaraja ya kutuvusha kwenda katika ndoto ya Taifa.
“Watu wanashangaa leo kuambiwa kuwa Duni ndiyo mgombea mwenza wa Ukawa. Huyu (Duni) mpaka jana (juzi), alikuwa waziri katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ila kwa sababu ya uzito wa ndoto ya Taifa, ameona ajiuzulu uwaziri ili kusaidia kufanikisha ndoto,” alisema.
Akizungumzia katiba ya chama hicho kuhusu kupitisha mgombea urais alisema, “Katiba ya Chadema imetoa maelekeo jinsi ya kumpata mgombea urais na mgombea mwenza. Kifungu cha 7.16, kinazungumzia kazi za Kamati Kuu, ikiwamo ya kufanya utafiti wa wagombea wa urais na mwenza na kuwasilisha ripoti kwa Baraza Kuu kwa ajili ya mapendekezo kwa Mkutano Mkuu. Kamati Kuu ilifanya utafiti.”
Alisema katika utafiti huo, Kamati Kuu kwa kauli moja, ilipendekeza kwa Baraza Kuu la chama hicho Lowassa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema na ikapendekeza vyama vinavyounda Ukawa kutoa mapendekezo yao kuhusu uamuzi huo.
“Halikuwa jambo jepesi na tulipishana kauli hadi usiku wa manane. Utafiti wetu mbalimbali ulituambia kwamba Lowassa akipeperusha bendera kupitia Ukawa na kundi lake kubwa ndani ya CCM ndoto za Taifa hili zinakwenda kutimia.”
“Wote, akiwamo Dk Slaa walikubali. Tulimwalika Lowassa katika kikao cha Kamati Kuu ya Chadema na kumhoji, pengine watu wa pembeni walishauri tofauti lakini vikao vya chama viliamua kuwa Lowassa ndiyo mgombea,” alisema.
Akizungumza wakati akifunga mkutano huo alisema, “Tumekubaliana kuunganisha nguvu kwa utaratibu huu, wapo wabunge ambao watakosa nafasi, watakaokosa nafasi naomba tuvumiliane na hii ni kwa wanaogombea udiwani, ubunge na urais. Watu ni wengi na utaratibu huu lazima utawaacha wengine kando. Watakaoachwa waendeleze moto wa kukiimarisha chama.”
Mkutano wenyewe
Mkutano huo ulianza kwa wajumbe wengi kutiririka katika eneo la ukumbi huo kuanzia saa tatu asubuhi wakisubiri kugawiwa sare za mkutano huku asilimia kubwa wakiwa wamevaa vitambulisho vyenye picha na maandishi... ‘Lowassa 2015.’
Viongozi wakuu na wageni maalumu walianza kuwasili saa 4:10 asubuhi wakiongozana na Kaimu Katibu Mkuu, Salum Mwalimu na kufuatiwa na wenyeviti wenza wa Ukawa, Maalim Seif na Mbowe.
Wafanyabiashara nao hawakusita kutafuta riziki pale walipojitokeza kuuza nguo na mapambo mbalimbali kama skafu, kofia, beji na mabango yenye picha ya Lowassa.
Tofauti na ilivyozoeleka, idadi ya wafuasi nje ya ukumbi haikuwa kubwa kumsindikiza Lowassa na hata alipoingia saa 5.25 asubuhi hawakuwa wameugundua msafara na baada ya kung’amua walianza kuimba “rais, rais, rais.”
Asilimia kubwa ya wafuasi waliojitokeza, walivalia fulana za chama hicho zenye mistari ya rangi nyekundu, nyeupe, bluu na nyeusi huku wengine wakiwa wamevalia fulana zenye maandishi ya 4u Movement na “Zuia goli la mkono 2015”.
Barabara ya Sam Nujoma, hadi eneo lote la Mlimani City ulipokuwa ukifanyika mkutano huo lilipambwa kwa bendera za Chadema na kuchagizwa na sare na wajumbe hao kiasi cha kufanya rangi zinazotumiwa na chama hicho kutawala.
Ulinzi uliimarishwa kila kona ukihusisha askari polisi na walinzi wa chama hicho, “Red Brigade” ambao walikuwa na kazi ya kuwarudisha nyuma wafuasi waliokuwa wakiwakimbilia viongozi mbalimbali kwenda kuwasalimia.
Eneo lote la Mlimani City lilijaa magari kiasi cha baadhi ya wajumbe wa mkutano huo kukosa maegesho na kulazimika kuegesha nje.
Kabla ya kumkaribisha Mbowe, Mwalimu alielezea shughuli na mikakati mbalimbali iliyofanywa na chama hicho katika kujiimarisha na kuongeza uimara na Ukawa.
Alisema Ofisi ya Katibu Mkuu ilifanya mambo makuu matatu ambayo ni kutoa hamasa kwa makada wote, kufanya oganaizesheni mbalimbali za chama na kutekeleza agizo la kufanya usajili wa makada wapya kutoka vyama vingine, hususan CCM.
Katika oganaizesheni, alisema walifanya mafunzo kwa viongozi wote wa chama na watiania na kuimarisha kanda 10 za chama hicho.
Huku akifananisha usajili wa wafuasi kutoka vyama vingine kuingia Chadema na usajili wa mpira wa miguu barani Ulaya, Mwalimu alisema:
“Mheshimiwa mwenyekiti usajili uliotufanyia katika dakika za majeruhi siyo ushindi wa ligi kuu pekee, bali wa ligi ya mabingwa Ulaya.”
Imeandikwa na Fidelis Butahe, Ibrahim Bakari, Nuzulak Dausen na Peter Elias

Chanzo cha habari na gazeti makini la kila siku la mwananchi

After 17 years as husband and wife, Will Smith and Jada Pinkett-Smith are getting divorced, a new report by Radar Online claims.
“For Will and Jada, holding it together these past few years has been tough because their marriage has been on life support for a long time,” an insider says.

Will and Jada
(Photo Credit: Getty Images)
The insider continues, “They’re exhausted from trying to maintain the façade of a happy union. They’ve decided to pull the plug in a carefully choreographed manner, [and] agree announcing their split at the end of the summer is the right move.”
RELATED: Blake and Miranda, Jen and Ben and More — 7 of the Most Devastating Celebrity Breakups
Will, 46, and Jada, 43 — who are parents to 17-year-old Jaden and 14-year-old Willow — are reportedly in the process of working out a settlement that will protect their combined $240 million fortune.
Earlier this summer, the couple shocked fans when the Magic Mike XXL actress hinted at her “open marriage” during an interview with Howard Stern.
 Will smith jada pinkett smith divorce
Source: http://www.intouchweekly.com/posts/will-smith-jada-pinkett-smith-divorce-64928


Na Damas Makangale, Makangale Satellite Blog

“Kila mwaka idadi ya watumiaji wa dawa za kulevya nchini hasa kwa vijana wenye umri mdogo kabisa kati ya miaka 15 mpaka 25 inakadiliwa kufika 10,000 hadi 11,000 kila mwaka nchini ni idadi kubwa na hali inatisha,’ anasema Afisa kutoka Kitengo cha Kudhibiti dawa za kulevya nchini, Moza Makumbuli 
 
..Ni baadhi ya watumiaji wa dawa za kulevya wakihudhuria moja semina zinazoendeshwa nchini
Wiki iliyopita Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya Nchini ( Drug Control Commission) kiliandaa semina ya siku moja kwa wadau mbalimbali kutoka kwenye vyombo vya habari, magereza, Polisi, Mashirika yasiyo kuwa ya Kiserikali, Madaktari na wizara ya afya na lengo la semina hiyo ilikuwa kuwapa wadau matokeo ya utafiti ya watumiaji wa dawa za kulevya cocaine na heroin nchini.

Akizungumza na wanasemina hiyo, Bi Makumbuli amesema kwamba utafiti huo ulifanyika katika mikoa 12 ya Tanzania bara kwa kufanya mahojiano na watumiaji, waathirika, wananchi wa kawaida, polisi na watu mbalimbali pamoja na watoa taarifa ikiwemo na utafiti wa mahali husika.

Amesema kwamba utafiti huo ulifanyika katika mikoa ya Mtwara, Dodoma, Morogoro, Pwani, Kilimanjaro, Tanga, Arusha, Mwanza, Mbeya, Shinyanga, Geita na kigoma.

Lengo linguine la utafiti huo wa kisayansi ni kuongeza uelewa wa athari za matumizi ya dawa za kulevya, hatari ya watumiaji kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi na tatizo la wagonjwa wa akili nchini inayochangiwa na matumizi ya dawa za kulevya nchini.

Bi Makumbuli aliongeza kwamba matumizi ya dawa ya kulevya kwa njia ya kujidunga kwa sindano imeongezeka maradufu Duniani na Kusini Mwa Jangwa La Sahara ambapo takribani watu milioni 13 wanatumia dawa hizo za kulevya kati ya heroin na cocaine duniani na kusini mwa jangwa la sahara takribani watu milioni 1.5 wapo kwenye matumizi ya dawa hizo.

Alifafanua kwamba tatizo la madawa ya kulevya nchini halikupata nafasi ya kuhifadhi kitakwimu au taarifa zake nyingi hazijapata nafasi ya kuwekwa vizuri kwenye kumbukumbu (Well documented) kwa muda mrefu na ndiyo kikwazo kwa serikali kuamua, kupanga na kuchangua mikakati madhubuti ya kupambana na ongezeko hilo la uuzwaji na utumiaji wa madawa hayo ya kulevya nchini.

“kwenye utafiti wetu tumegundua kwamba sehemu nyingi za pwani (Coast Region) na pembezoni mwa barabara (Along the road corridor) zimeathirika sana kwa vijana wengi kujihusisha na uuzwaji na utumiaji wa madawa hayo ya kulevya na wengi kazi zao ni makodakta wa daladala, wapiga debe, wavuvi sehemu za pwani na wengine ni vibaka na wanawake wanajihusisha na biashara ya ukahaba,” aliongeza.

Kwa upande wake, Mratibu wa Programu ya kudhibiti dawa za kulevya kutoka kitengo hicho cha serikali, Bw Joel Ndayongeje amesema kwamba mapambano dhidi ya dawa za kulevya bado yana safari ndefu hapa Tanzania kutokana na kusongwa na vikwazo lukuki vikiwamo vya sheria dhaifu, ukosefu wa sera ya Taifa ya udhibiti na kuendekezwa kwa vitendo vya rushwa katika vyombo vya dola.

Bw Ndayongeje aliongeza kwamba kwenye utafiti wao waligundua pia mikoa inayoongoza kwa matumizi makubwa ya dawa za kulevya nchini ni 5,190,  Tanga, 3,300 Mwanza, 2,700 Arusha, 1,539 Morogoro, 1,096 Dodoma, 820 Mbeya, 563 Kilimanjaro, 319 Shinyanga, 108 Geita, 100 Kigoma na watu 65 mtwara. 

Amesema kwamba katika miaka ya hivi karibuni matumizi ya dawa za kulevya kwa wanawake yameongezeka mara ya mwisho ulifanyika na kupata matokeo ya asilimia 6% lakini utafiti wa hivi karibuni kwa kushirikiana na Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na magonjwa cha wa marekani (US Centres for Disease and Prevention (CDC) nchini idadi ya wanawake kwenye matumizi ya dawa za kulevya kwa sasa ni asilimia 20%
Pamoja na mambo mengine Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliwahi kukiri kuwa tatizo la dawa za kulevya hapa nchini ni kubwa, linalohitaji nguvu kubwa ya mataifa yote duniani.

“Mapambano dhidi ya dawa za kulevya hayatafanikishwa na nchi moja bali nchi zote duniani,” amesema Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakati akiliahirisha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma, Septemba 6, mwaka jana.
Kutokana na ukubwa wa tatizo hilo, Pinda anasema Serikali inafikiria kuanzisha mahakama maalumu ili kuharakisha mashauri ya dawa za kulevya.

“Nina imani tukijipanga vizuri inawezekana… tutafika mahala tufikirie mahakama maalumu ya dawa za kulevya ambayo itakuwa na kazi moja tu ya kusimamia mashauri yanayohusu dawa za kulevya,” anasema.

Kadhalika, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi, anasema Serikali inaandaa mapendekezo ya kufuta Sheria ya Dawa za Kulevya na kutungwa mpya itakayokidhi mahitaji ya kushughulikia ipasavyo makosa ya dawa za kulevya.

Wakati Serikali ikitangaza msimamo wake huo, meli iliyosajiliwa Tanzania (upande wa Zanzibar) iliripotiwa kukamatwa nchini Italia ikiwa imesheheni tani 30 za dawa za kulevya zenye thamani ya paundi milioni 50, sawa na Sh bilioni 123 za Tanzania.

Kutokana na mazingira hayo, Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya nchini (DCC) kwa upande wake, inaona pia kuna haja ya Serikali kutangaza dawa za kulevya kuwa adui namba moja kama hatua mojawapo ya kuonesha ukubwa wa tatizo hilo hapa nchini lakini watafanya hivyo endapo tu kutakuwa na ushahidi wa kitafiti na kitakwimu ili kuweza kujenga hoja hiyo.

Heroin na madhara yake
Heroin ni aina ya dawa ya kulevya ya unga inayopumbaza mfumo wa fahamu. Dawa hiyo inatokana na mmea uitwao ‘opium poppy’. Imekuwa ikiingizwa hapa Tanzania ikitokea nchi za Mashariki ya mbali.

Mitaani heroin huitwa majina mengi kama vile unga, brown shugar, ngoma, ubuyu, mondo, ponda, dume, farasi, n.k.
Cocaine na madhara yake
cocaine ni dawa ya kulevya inayotengenezwa kutokana na mmea wa coca ambao hustawi zaidi katika nchi za Amerika ya Kusini. Kitaalamu mmea huo hujulikana kwa jina la erythroxylon coca.

Cocaine, kwa mujibu wa watafiti , huwa katika unga mweupe au katika hali ya mawe madogo madogo. Inajulikana kwa majina mengi kama vile snow, star dust, keki, unga, big c, bazooka, white sugar na unga mweupe.

Hapa Tanzania cocaine hupatikana kwa shida kwa sababu ya bei yake ni nadra sana kupatikana nchini.


Anataja madhara ya cocaine kuwa ni kuathiri mfumo wa fahamu wa binadamu, kutokwa na damu puani, kuwa na mafua makali yasiyopona, kukosa hamu ya chakula, kupanuka kwa mboni za macho, mchafuko wa damu na kupata majipu, kuongezeka kwa mapigo ya moyo na shinikizo la damu.

Madhara mengine ya cocaine ni mtu kuchanganyikiwa, kukosa ufanisi kazini, kuwa na hisia za kuwapo kwa vijidudu mwilini, magonjwa ya ini, kuharibika kwa mishipa ya fahamu, kuharibika kwa moyo, figo na mapafu, kikohozi cha muda mrefu, kupasuka kwa mishipa ya damu kichwani kunakoweza kusababisha kiharusi au kifo na kumweka mtu katika hatari ya kuambukizwa virusi vya Ukimwi.
 
Mtumiaji wa kujinduga akitumia dawa hizo
Mwisho.







Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.