SPIKA Mstaafu, Anna Makinda ameiomba serikali na mamlaka husika kuanza mchakato wa kusukuma mabadiliko ya sheria ya ndoa ili kupanua wigo wa haki za wanawake na watoto nchini.
 
Image result for ndoa
 
Akizungumza katika kongamano la wanawake lilioandaliwa na Mfuko wa msaada wa kisheria nchini (LSF) jana jijini Dar es Salaam, Makinda alisema kwamba sheria ya ndoa ya mwaka 1971 imepitwa na wakati na inahitaji marekebisho makubwa ili kutoa haki kwa wanawake nchini.
 
“Hii sheria ya ndoa inawatenga sana wanawake nchini katika swala la mirathi na kuacha watoto wengi wakiteseka ni wakati muafaka sasa kwa wanaharakati kusaidia na wabunge ili kuleta marekebisho hayo kwa manufaa ya nchini nzima,” alisema Makinda ambaye ni spika mstaafu.
 
Alisema kwamba marekebisho hayo makubwa au kuandikwa upya kwa sheria ya ndoa itakuwa hatua moja kubwa katika kulinda haki za wanawake za kumiliki mali, kama vile mashamba na kadhalika.
 
Alisisitiza kwamba swala la mirathi ni tatizo kubwa sana nchini ambapo wanawake wengi wamepoteza mali zao walizochuma na wenzi wao wakati wa ndoa.
 
“Nikiwa mbunge, waziri na baadaye spika tulipambana vikali katika kubadilisha sheria ya ardhi ili kuwapa watu wa hali ya chini kupata nafasi ya kumiliki ardhi, sasa na hii sheria ya ndoa inapaswa kushughulikiwa kwa haraka ili kuweza kutoa matokeo chanya kwa jamii,” aliongeza.
 
Alifafanua kwamba marekebisho hayo ya sheria ya ndoa yatasaidia kunusuru maelfu ya wanawake ambao wanateseka kutokana na kila aina ya unyanyasaji wa kijinsia na vipigo ambavyo vinaongezeka kila kona ya nchini.
 
Aliomba mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kushirikiana na serikali katika majadiliano hasa katika mambo ya mirathi na ndoa ili kuhakikisha upatikanaji wa marekebisho hayo yanapatikana haraka.
 
“ni muhimu pia maswala haya ya haki za wanawake na watoto kufundishwa katika shule za msingi na sekondari ili kupeleka elimu hiyo ya uraia kwa wanafunzi nchini nzima, ila ni muhimu kushirikiana na serikali ili kufanikisha hayo,” aliongeza 
 
Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu, Mfuko wa Msaada wa Kisheria (LSF), Bw, Kees Groenendijk alisema kwamba mfuko lengo lake kuu ni kuongeza haki na usawa kwa wanawake nchini kupitia uwezeshaji wa fedha na mafunzo.
 
“Kutokana na mustadha huo, mfuko uliamua kwamba mfuko kusaidia mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali yanayotoa msaada wa kisheria kwa jamii hasa wanawake ambao wapo katika wilay zote za Tanzania Bara,” alisisitiza.
 
Alisema tangu mfuko huo uanze zaidi ya wanawake 2,000 walifikiwa kwa msaada wa kisheria ambao ni asilimia 60% ya wanawake nchini nzima.
 
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) Bi, Tike Mwambipile alisema kwamba serikali ni lazima kuanzisha kitengo maalum cha kushughulikia matatizo ya ndoa na mirathi katika mifumo ya utoaji haki nchini.
Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.