UMOJA wa Ulaya (EU) na Umoja wa Mataifa (UN) wamejiunga pamoja kuendesha kampeni ya uelewa wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) nchini Tanzania . Aidha kwa pamoja wamezuru miradi iliyofadhiliwa na EU. Wakiwa Mkoani Iringa wamepata nafasi ya kuzungumza na wanachuo 1,000 kutoka vyuo vikuu vya Iringa na Mkwawa kwenye semina iliyoelezea malengo hayo ya dunia ambayo ni sehemu ya ajenda 2030 ya maendeleo endelevu duniani. Kampeni hiyo imelenga kuwafanya vijana waelewe malengo 17 ya dunia ambayo kwa sasa yana mwaka mmoja tangu yapitishwe na kuwatanabaisha wajibu wao katika kufanikisha utekelezaji wake ndani ya mazingira ya Tanzania. 
Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro (kushoto) akisalimiana na mmoja wa wahadhiri wa chuo hicho alipowasili katika ofisi za Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa (UOI), Prof Joshua Madumulla akiwa ameambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez.(Picha zote na Zainul Mzige wa Moblog)

Semina katika vyuo hivyo ni sehemu ya mpango madhubuti wa Umoja wa mataifa uliozinduliwa Arusha Mei mwaka huu na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Bw. Alvaro Rodriguez wenye lengo la kuwaelimisha vijana zaidi ya 30,000 ifikapo mwaka ujao kuhusu malengo hayo ya dunia. Ujumbe huo wa EU na UN pia ulipata nafasi ya kutembelea miradi mbalimbali inayofadhiliwa na EU ukiwamo wa Boma la Kijerumani ambalo lilikarabatiwa kwa ruzuku ya EU kupitia 'fahari yetu – Southern Highlands Culture Solutions'. Boma hilo ni moja ya majengo ya zamani katika mji wa Iringa na lilijengwa na Wajerumani mwaka 1900 kama hospitali ya kijeshi. Baada ya vita ya Kwanza ya Dunia, jengo hilo lilibadilishwa matumizi na watawala wapya, Uingereza, na kulifanya kuwa jengo la utawala. EU imesema inaona fahari kuwa mmoja wa wawekezaji wakubwa katika sekta ya sanaa na urithi wa kitamaduni nchini Tanzania, ikifadhili miradi 10 iliyo chini ya programu ya 10 ya EDF ya kusaidia masuala ya kitamaduni. 

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa (UOI), Prof Joshua Madumulla akiwa kwenye mazungumzo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro (upande wa kushoto katikati) pamoja na Mtaalam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Hoyce Temu (kushoto) alipotembelewa ofisini kwake na ugeni huo. Kulia ni Meneja wa Mradi wa Fahari Yetu, Jan Kuever pamoja na Katibu Tawala Msaidizi -Miundombinu wa Mkoa wa Iringa, Henry Mditi.

Masuala yanayohusu urithi wa kitamaduni ni muhimu katika kuchagiza ukuaji wa uchumi, ajira na huku ikifuma mahusiano ya kijamii, na kutoa fursa ya kuboresha utalii endelevu mkoani Iringa huku ikileta faida kwa wakazi wa eneo hilo. Bw. Rodriguez, akizungumza katika kampeni hiyo alisema kwamba ajenda 2030 ambayo ni ajenda ya maendeleo endelevu inahitaji ushiriki wa kila mmoja.Aliwapongeza wanachuo hao na wanazuoni kwa kujikita kutambua malengo hayo ya dunia. Aidha aligusia umuhimu wa vijana kushiriki katika masuala ya maendeleo kutokana na ukweli kuwa, kwa taifa kama la Tanzania vijana ni asilimia 60 ya wananchi wote waliopo.Alisema kwamba vijana wanajukumu kubwa la kushiriki katika maendeleo hayo kwa lengo la kuipeleka nchi katika hatua nyingine ya maendeleo. 

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akiwa ameongozana na Katibu Tawala Msaidizi -Miundombinu wa Mkoa wa Iringa, Henry Mditi kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano Chuo Kikuu cha Iringa.

Hata hivyo alisema kwamba ni wajibu wa kila mtu hasa vijana, kuhakikisha kwamba malengo hayo ya dunia yanafanikiwa . Alisema Umoja wa Mataifa kwa kusaidiwa na wadau wake muhimu kama Umoja wa Ulaya, utaendelea kusaidia Watanzania kuwajibika katika shughuli mbalimbali za maendeleo katika kuunga mkono malengo hayo ya dunia. Mmoja wa washiriki alipongeza Umoja na wa Mataifa kwa kuwafikia vijana wa vyuoni na kuwapa semina hiyo. “Ninajisikia mtu mwenye bahati kupata nafasi ya kujifunza maendeleo endelevu kutoka kwa Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini. Nikiwa kama kijana, naona faraja kuona kwamba viongozi wetu wanafuata maelekezo yaliyofafanuliwa kwenye malengo 17 ya maendeleo endelevu; naamini kama tukijitahidi kuyafikia ifikapo 2030, basi Tanzania na duniani kwa ujumla itakuwa eneo jema la kuishi. Na kwa kuwa sasa natambua kuhusu malengo hayo ya dunia, ninaweza kutoa mchango wangu kusaidia kuyafikia -najisikia kuwezeshwa sana.” amesema Mary, mmoja wa washiriki. 

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa (UOI), Prof Joshua Madumulla akisoma taarifa fupi ya Chuo Kikuu cha Iringa mbele ya ujumbe kutoka Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya wakati semina kuhusu malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ambayo ni sehemu ya ajenda 2030 ya maendeleo endelevu duniani kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa.
Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akizungumza kwenye semina ya malengo ya dunia kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa ambapo aliwaasa wakawe mabalozi wazuri wa malengo hayo kwenye jamii zao na wanafunzi wenzao wa vyuo vingine.
Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro akitoa salamu za Umoja wa Ulaya kwa niaba ya Balozi wa Umoja huo, Bw. Roeland Van De Geer wakati wa semina Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa wanachuo wa Iringa iliyowezeshwa na EU.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akiwapiga msasa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa kuhusu Malengo ya Dunia katika semina iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) mjini Iringa.
Mwanafunzi wa mwaka wa tatu anayechukua Shahada ya Sayansi katika Uchumi na Fedha wa Chuo Kikuu cha Iringa, Sarafina Sayi akiuliza swali kwa mkufunzi wa malengo ya dunia Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (hayupo pichani) wakati wa semina hiyo.
Mwanafunzi wa Shahada ya Sayansi katika Uchumi na Fedha wa Chuo Kikuu cha Iringa, Geoffrey Kadori akiuliza swali kwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela wakati wa semina ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ambayo ni sehemu ya ajenda 2030 ya maendeleo endelevu duniani kwa wanafunzi wa Chuo hicho.
Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akijibu swali wakati wa kipindi cha maswali na majibu kwenye semina kuhusu malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa.

Pichani juu na chini ni wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa kutoka vitivo tofauti chuoni hapo waliohudhuria semina ya malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ambayo ni sehemu ya ajenda 2030 ya maendeleo endelevu duniani kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akimkabidhi Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa (UOI), Prof Joshua Madumulla makabrasha na majarida yenye ripoti na taarifa mbalimbali za Umoja wa Mataifa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela ripoti na makabrasha mbalimbali ya Umoja wa Mataifa mara baada ya kuhitimisha semina kuhusu SGDs kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa.
Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela (wa tatu kulia) katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya pamoja na Balozi wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs Champion), Sabinus Paul (kushoto) nje ya ukumbi kulikofanyika semina kuhusu SDGs kwa wanachuo wa Iringa.
Picha ya pamoja na sehemu ya washiriki wa semina hiyo huku wakiwa na mabango ya SDGs.
Muonekano wa nje wa jengo la Makumbusho ya Mkoa na Kituo cha Utamaduni -Iringa Boma ambalo limejengwa kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU).
Kibao cha Makumbusho ya Mkoa wa Iringa kinachoratibiwa na Mradi wa Fahari yetu kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Iringa
Meneja wa Mradi wa Fahari Yetu, Jan Kuever akielezea dhumuni la mradi Fahari Yetu unaolenga kuendeleza utamaduni nyanda za juu kusini kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) aliyeambatana na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro (mwenye suti) ambao ndio wafadhili wa jengo hilo la Makumbusho ya Mkoa wa Iringa. Wengine katika picha ni wahadhiri na maprofesa kutoka Chuo Kikuu cha Iringa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akisaini kitabu cha wangeni ndani ya Makumbusho ya mkoa wa Iringa.
Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika Makumbusho ya mkoa wa Iringa.
Meneja wa Mradi wa Fahari Yetu, Jan Kuever akitoa maelezo picha mbalimbali zinazoelezea historia ya mkoa wa Iringa wakati wa utawala wa Chifu Mkwawa kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro walipotembelea makumbusho ya mkoa wa Iringa
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akisoma historia mbalimbali za enzi za utawala wa kichifu ndani ya Makumbusho ya Mkoa wa Iringa.
Mwongoza wageni katika Makumbusho ya mkoa wa Iringa, Jacob Shenyagwa (mwenye miwani) akitoa maelezo ya picha mbalimbali kwa ugeni huo wa UN na EU uliotembelea makumbusho hiyo iliyojengwa chini ya ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU).
Mwongoza wageni katika Makumbusho ya mkoa wa Iringa, Deonis Mgumba akitoa maelezo ya vifaa mbalimbali vilivyokuwa vikitumika enzi za utawala wa kichifu kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto) na Katibu Tawala Msaidizi -Miundombinu wa Mkoa wa Iringa, Henry Mditi (katikati) walipotembelea makumbusho hayo mjini Iringa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro wakitwanga mahindi kienyeji katika moja ya kinu kilichokuwa kinatumika enzi hizo za utawala wa kichifu kilichopo katika makumbusho hayo.
Mwongoza wageni katika Makumbusho ya mkoa wa Iringa, Matatizo Kastamu akitoa maelezo ya picha mbalimbali zenye kumbukumbu za utawala wa kichifu na historia ya mji wa Iringa kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro.
Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro (kushoto), Mtalaam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu na Meneja wa Mradi wa Fahari Yetu, Jan Kuever wakipitia vipeperushi vyenye maelezo ya kina ya Mradi wa Fahari Yetu unaoendesha Makumbusho na Kituo cha Utamaduni mkoa wa Iringa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro katika picha ya pamoja kwenye sanamu maalum za mavazi ya kipindi cha utawala wa Chifu Mkwawa walipotembelea Makumbusho ya mkoa wa Iringa.
Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.