Mchungaji mmoja huko nchini Afrika Kusini, Lethebo Rabalago anatumiwa dawa ya mbu ya kupuliza kama njia ya uponyaji kwa waumini wake wanaokwenda kanisani kwake kwa ajili ya maombi ya matatizo mbalimbali ya kiroho.Image result for lethebo rabalago
 
Mchungaji anaamini kwamba dawa hiyo ya mbu ya kupuliza inaweza kumponya mwanadamu na kumwezesha mtu kupata upako wa bwana baada ya kuombewa na kupuliziwa kama sehemu ya ufunuo wa kutoka kwenye dimbwi la dhambi na mikosi.
 
Lethebo Rabalago, kutoka kwenye kanisa la Mount Zion General Assembly (MZGA) katika mji wa Limpopo, alituma picha kwenye mitandao ya kijamii kama vile Facebook na kuonyesha akitumia dawa hiyo kali ya kuua mbu kama nyenzo yake ya uponyaji.
 
Siku chache zilizopita kwenye mitandao ya kijamii kulijaa taarifa za mchungaji huyo anayetumia dawa hiyo ya mbu kama njia ya uponyaji kwa waumini wake hapo kanisani, baada ya kutuma picha hizo mijadala ilikuwa ikiendelea kwenye mitandao sehemu kubwa ya Afrika kuhus aina hiyo ya maombezi.
 
Mmoja wa waumini aliyepitia huduma alinukuliwa akisema kwamba “Nilikuja hapa na maumivu sehemu ya nyuma na tumbo, lakini sasa baaada ya maombezi ya mchungaji nimepata uponyaji wa kutosha na pua yangu iliumia tangu wiki iliyopita na baada ya mchungaji kuniombea na kunipuliza dawa nimepata nafuu kubwa,” alinukuliwa akisema.
Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.