Welcome in Makangale Satellite Blog
Mteja wa Bank of Africa-Tanzania (BOA),Bw.Dolvin Salvatory Olomi, kutoka Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro,amebahatika kuibuka mshindi wa jumla wa shilingi milioni 5 kupitia kampeni iliyomalizika iitwayo “Miamala ni Fursa.”
Kampeni hiyo, iliyoanza Juni hadi Septemba 2025, iliwezesha zaidi ya washindi 60 nchi nzima kujinyakulia zawadi, huku wateja wakipata zawadi za kila wiki za Shilingi 50,000 kwa kutumia huduma za kidigitali zinazotolewa na Benki. Kampeni ilifikia kilele kwa droo kubwa ya mwisho, ambayo ilitoa zawadi kubwa ya Shilingi 5 milioni kwa mtumiaji bora wa huduma ya kidijitali—aliyetangazwa rasmi kuwa mshindi mkuu kupitia droo ya bahati nasibu hiyo.
"Kushinda Shilingi milioni 5 kwa kutumia huduma ya benki kwa njia ya simu kumebadilisha maisha yangu," alisema Bw Olomi, ambaye alitoa shukurani zake za dhati kwa Bank of Africa-Tanzania, kwa kukuza ushirikishwaji wa kifedha kupitia kampeni za kibunifu na zenye kuleta manufaa kwa wateja wake.
Kampeni ya “Miamala ni Fursa” ilizinduliwa Juni 4, 2025, na ilianzishwa ili kuhimiza utumiaji wa huduma za benki kidijitali kwa kufanya miamala ya kila siku, ikijumuisha uhamishaji wa fedha kutoka benki kwa matumizi mbalimbali, kufanya malipo ya ankra,kununua muda wa maongezi au umeme. Kampeni hii ni sehemu ya dhamira pana ya benki ya kuunga mkono ajenda ya Serikali ya Tanzania ya matumizi ya huduma za kidijitali na kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma za fedha kwa wote.
Ofisa Mkuu wa Huduma za Kidijitali wa Bank Of Africa-Tanzania ,Lameck Mushi alisema: "Mafanikio ya kampeni ni ishara tosha kwamba Watanzania wako tayari kutumia huduma za kibenki za kidijitali ambazo ni rahisi, zinaweza kufikiwa na ni zenye manufaa. Kupunguza ada ya uhamisho kutoka benki kwa matumizi mbalimbali kwa zaidi ya asilimia 50% na kufanikisha kuongeza matumizi ya huduma za kifedha kwa njia ya simu kufanya miamala, na msisimko wa kushinda zawadi uliongeza zaidi."
Bw Mushi aliongeza: "Iwe unaishi maeneo ya mjini au vijijini, matumizi ya huduma za Kibenki kwa njia ya simu yalimpatia kila mmoja fursa ya kushinda. Kampeni hii ni uthibitisho kwamba huduma ya benki ya kidijitali inaweza kuwa ya kila mtu."
Benki pia ilihamasisha wafanyakazi wake katika matawi mbalimbali nchini kuelimisha wateja, watumiaji wapya, na kutoa msaada wa kiufundi muda wote wa kampeni.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano , Nandi Mwiyombella alisema kampeni ya "Miamala ni Fursa” ilikuwa zaidi ya kujitangaza. “Tumewawezesha wateja si tu kwa zawadi za pesa taslimu, lakini pia kuwahakikishia pia wateja wetu kuwa huduma zetu za kidijitali ni zenye uhakika na wanaweza kuzitumia bila wasi”.
Bank of Africa Tanzania inawashukuru washiriki wote na inampongeza mshindi wa jumla wa zawadi kutoka Moshi, pamoja na washindi wengine wa kila wiki waliozawadiwa kwa matumizi ya huduma za kidigitali zinazotolewa na benki.
Wakati benki inao mkakati wa kuleta kampeni za kunufaisha wateja siku za mbele,itaendeleza dhamira yake kuongeza ujumuishaji wananchi katika sekta rasmi za kifedha na kuwezesha wananchi kunufaika na mapinduzi ya teknolojia na ya kidigitali.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob John Mkunda, amempandisha cheo Alphonce Simbu kutoka Sajini kuwa Sajinitaji katika hafla iliyofanyika ofisini kwake Makao Makuu ya Jeshi Upanga Jijini Dar es Salaam leo Septemba 25, 2025 baada ya kupata mafanikio ya Mbio za Marathon Tokyo, Japan.
Dr Ibrahim Shaddad met President for IUGS Dr Hassina Mouri is the President of the International Union of Geological Sciences (IUGS) Unesco chair in medical geology in Africa:
This potential partnership could lead to increased knowledge sharing, capacity building, and research in the field of medical geology, ultimately benefiting African nations.
..Yapongeza mchakato wa Ufungaji wa Mgodi wa viwango vya Kimataifa
Na Mwandishi Wetu,
Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) umeipongeza kampuni ya Barrick kwa weledi na kuzingatia viwango vya kimataifa katika mchakato wa ufungaji wa mgodi wake wa Buzwagi na kubadilisha matumizi ya eneo hilo na kuwa Kongani Maalum la Uwekezaji (SEZ) ambalo inafungua fursa za kiuchumi nchini.
Mjumbe wa maofisa hao wa TISEZA ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wake, Gilead John Teri ilifanya ziara hiyo kikazi jana na kuridhishwa na mchakato mzima wa ufungwaji wa mgodi huo.
Akiwa katika eneo hilo , Bw Teri alipata taarifa fupi ya uwekezaji wa aina mbalimbali ndani ya kongani hilo maalum la Uwekezaji (SEZ) na kukagua maeneo mbalimbali yatakayotumiwa na wawekezaji watakaohitaji kuwekeza katika Kongani hiyo na alitembelea kiwanda cha kuzalisha (Conveyor) ambacho tayari kimeanza kufanya uzalishaji na kutoa fursa za ajira.
Akiongea baada ya ziara hiyo,Bw.Teri alitoa pongezi kwa kampuni ya Barrick nchini kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za serikali kwa kufanikisha ufungaji wa mgodi huo kwa viwango vya kimataifa na kufungua fursa ya eneo la kimkakati wa kukuza uchumi kupitia uanzishaji wa viwanda na kufungua milango ya biashara.
“Nawapongeza Barrick kwa kuhakikisha mgodi huu unafungwa kitaalamu pia nachukua fursa hii kuwashukuru kamati ya Utekelezaji wa Kongani hii inavyofanya kazi kwa Kushirikiana na mamlaka mbalimbali lengo likiwa kutimiza kufanikisha lengo la serikali la kuhakikisha eneo hili linatumika kimkakati ili liweze kuleta matokeo chanya kwa taifa ”,alisema Teri.
Teri pia alisema ameridhishwa na utangazaji wa eneo hilo unaoendelea ambazo zinabainisha fursa zilizopo na mipango iliyowekwa na serikali kwa ajili ya kutoa huduma kwa kuhakikisha zinapatikana katika eneo moja (One Stop Centre).
Kwa upande wake Meneja wa ufungaji wa Mgodi wa Barrick Buzwagi, Mhandisi Zonnastral Mumbi alisema tayari eneo hilo la kongani ya Buzwagi limepatiwa usajili na serikali kwa ajili ya shughuli hiyo maalum ambapo ukamilikaje wake utachochea ukuaji wa uchumi na ajira kwa vijana hapa nchini.
Aidha Mumbi alieleza ujumbe huo kuwa hadi kufikia sasa wawekezaji 19 wameonyesha nia ya Kuwekeza katika Kongani hiyo huku wawekezaji tano tayari wameanza mchakato wa usajili na tayari mwekezaji mmoja ameanza uzalishaji .
Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita, alitoa wito kwa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) kuweka msisitizo katika kutangaza mradi mkubwa wa Kongani Maalum la Uwekezaji wa Buzwagi ( SEZ) ambao unatarajiwa kuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo ya kiuchumi kwa Mkoa na Taifa kwa ujumla.
Aidha, RC Mboni alibainisha kuwa Shinyanga ipo tayari kupokea wawekezaji kutokana na mazingira wezeshi yaliyowekwa na serikali pamoja na Mkoa kuwa na rasilimali zote muhimu kwa uwekezaji ikiwemo ardhi, upatikanaji wa maji, umeme, miundombinu ya kisasa ikiwa pamoja na barabara, uwanja wa ndege wa Shinyanga na Kahama, mtandao wa mawasiliano, na nguvu kazi.
Meneja Utekelezaji wa Mradi wa Kongani ya Buzwagi kutoka Barrick, Stanley Joseph akifanya wasilisho kwa ujumbe wa maofisa waandamizi kutoka Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) uliofanya ziara mgodini hapo.Mwandishi Wetu, Beijing, China
Waandishi wa habari waandamizi kutoka Tanzania, Zimbambwe, Sudani Kusini, Ivory Coast and Uturuki wameshiriki mafunzo kwa vitendo nchini China hivi karibuni.
Mafunzo hayo yalihusu maendeleo ya teknolojia na mapinduzi yake ili kuleta matokeo chanya kwenye sekta ya habari na mawasiliano ya umma, na maendeleo ya taifa kwa jumla.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo yaliyopewa kauli mbiu ya “Semina juu ya usimamizi wa vyombo vikuu vya habari katika nchi zilizo katika mpango wa ukanda na barabara” (Seminar on Senior Management of Mainstream Media in countries along the Belt and Road Initiative, - ukanda mmoja na njia moja ) Bw Augustino John Tendwa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) alisema mafunzo hayo yanayoendelea yamejikita katika kuleta fikira, ubunifu na matumizi ya kidigitaki katika kuleta mapinduzi ya tekolojia katika nchi za washiriki.
Bw Tendwa alieleza kwamba washiriki wa mafunzo hayo ya vitendo walipata fursa ya kutembelea makao makuu ya kampuni ya kimataifa ya teknolojia – Laird Technologies – kujifunza kwa vitendo maendeleo ya kiteknolojia yanayofanyika nchini China.
Wakiwa jijini Beijing, washiriki waliweza kujionea kwa karibu namna kampuni hiyo inavyoendesha uzalishaji wa vifaa vya hali ya juu vya kielektroniki, vikiwemo vifaa vya mawasiliano ya wireless, udhibiti wa joto, mitetemo na teknolojia ya kupunguza mwingiliano wa sumaku-umeme (EMI shielding).
“Kampuni kama Laird ni mfano halisi wa namna China inavyowekeza katika ubunifu na utafiti wa kisayansi kwa ajili ya maendeleo ya teknolojia duniani. Hii ni fursa ya kujifunza na kutafuta maeneo ya ushirikiano kwa maendeleo ya sekta ya viwanda na teknolojia nchini kwetu,” alisema Bw Tendwa.
Aliongeza kwamba mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo waandishi na maafisa wa serikali kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika kuhimiza maendeleo kupitia ushirikiano wa kimataifa chini ya mpango wa ukanda na barabara.Ushiriki wa Tanzania kupitia waandishi na maafisa waandamizi kutoka taasisi za serikali na vyombo vya habari ni ishara ya dhamira ya kukuza maarifa, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na atumizi ya teknolojia katika maendeleo ya taifa.
By Staff Writer,
Barrick, in partnership with the government of Tanzania , through its Bulyanhulu mine has continued improving primary education infrastructure environment by adding more classrooms at Kharumwa English-medium school located in Nyang’hwale District in Geita region. This
The project, which started on April 30, 2025, is expected to be completed on September 11, 2025.
This year, Nyang’hwale District Council has received Sh100,996,200 to implement the construction of four classrooms, and purchase furniture to address the challenge of classroom shortages.
Speaking at a ceremony to receive Uhuru Torch, which coincided with the laying of the foundation stone of the school, the Leader of Uhuru Torch Race, Mr Ismail Ali Ussi, commended Barrick Bulyanhulu for continuing supporting the government to improve people’s lives through the implementation of development projects in various sectors of the economy, including education.
“I take this opportunity to commend all experts of the Council and Barrick Bulyanhulu Mine for working day and night to ensure Tanzanians benefit from various projects which are implemented in this district,” Mr Ussi said.
Thus, he appealed to all Nyang’hwale residents to send their children to school. “There is no longer an excuse for long distances to school because schools are built everywhere and this is due to the collaboration of the Government and stakeholders like Barrick. Indeed, Barrick, you are supportive of Hon President Dr Samia Suluhu Hassan,” said Mr Ussi.
He explained further that the partnership shown by Barrick through its mines in the country is a clear indication of productive investment for the nation, and he urged other investors to emulate Barrick spirit by contributing to community development projects.
For her part, Nyang’hwale District Commissioner, Hon Grace Kingalame, stressed the importance of working hard and continuing with the spirit of implementing development projects at high standards to meet people’s needs.
She emphasized that Barrick, through its Bulyanhulu mine, has been closely cooperating with them in all development projects for the broader interests of the country social wellbeing.
Barrick Representative at the event, Mr Samson Mashala, who is Community Relations Officer at Bulyanhulu Mine said the mine would continue working with the Government to ensure CSR projects were well-implemented to improve people’s lives. “This project is going to address congestion, and improve a study environment,” he said.
He added that the project has reached 85% of its completion and will boost students' learning environment and contribute to positive outcomes in the education sector in the country.
The project, implemented through the force account system, is expected to reduce the problem of classroom shortages, overcrowding of students in classrooms, and promote a friendly learning environment.
Na Mwandishi Wetu,
Kampuni ya Barrick nchini yenye ubia na Serikali ya Tanzania, kupitia Mgodi wake wa Bulyanhulu imeendelea kuboresha mazingira ya elimu ya msingi kwa kuongeza ujenzi wa madarasa katika shule ya mchepuo wa Kingereza ya Kharumwa iliyopo Wilaya ya Nyang’hwale, Mkoa wa Geita. Shule hii imejengwa kwa fedha za Uwajibikaji kwa Jamii (CSR).
Mradi wa kuongeza madarasa ulianza Aprili 30, 2025, unatarajiwa kukamilika September 11, 2025.
Mwaka huu Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale imepata Sh100,996,200 kwa ajili ya kutekeleza ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa, na kununua samani kwa ajili ya kuondoa changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa.
Akizungumza wakati wa kupokea Mwenge wa Uhuru ulioambatana na kuweka jiwe la msingi katika shule hiyo hivi karibuni, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Bw Ismail Ali Ussi, aliipongeza Kampuni ya Barrick Bulyanhulu kwa kuendelea kuunga mkono jitihaza za Serikali za kuboresha maisha ya wananchi kupitia uwezeshaji wa miradi katika sekta mbalimbali, ikiwemo elimu.
“Nachukua fursa hii kuwapongeza wataalamu wote wa Halmashauri na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa kufanya kazi usiku na mchana katika kuhakikisha Watanzania wananufaika na miradi mbalimbali inayotekelezwa katika wilaya hii,” alisema Bw Ussi.
Hivyo, alitoa wito kwa wananchi wa Wilaya ya Nhang’hwale kuwapeleka watoto waso shuleni. “Hakuna tena kisingizio cha umbali mrefu wa shuleni kwa sababu shule zinajengwa kila sehemu na hii inatokana na ushirikiano wa Serikali na wadau kama Barrick. Hakika Barrick mnazidi kumheshimisha Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan,” alisema Bw Ussi.
Alifafanua kwamba ushirikiano unatolewa na kampuni ya Barrick kupitia migodi yake hapa nchini kiashiria cha uwekezaji wenye tija kwa taifa na kuwataka wawekezaji wengine kuiga mfano wa kampuni ya Barrick kwa kuchangia miradi ya maendeleo ya wananchi.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale, Mhe Grace Kingalame alisisitiza umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii na kuendelea na ari hiyo ya kutekeleza miradi ya maendeleo kwa viwango vya juu ili kukidhi mahitaji ya wananchi.
Alisisitiza kwamba kampuni ya Barrick kupitia mgodi wake wa Bulyanhulu wamekuwa wakishirikiana kwa karibu katika miradi yote ya maendeleo kwa maslahi mapana ya Taifa.
Mwakilishi wa Barrick katika hafla hiyo, Bw Samson Mashala, ambaye ni Afisa Uhusiano wa Jamii katika Mgodi wa Bulyanhulu, alisema mgodi utaendelea kufanya kazi na Serikali kuhakikisha miradi ya CSR iliyoibuliwa na wananchi inatekelezwa kwa viwango na kuboresha maisha ya wananchi. “Mradi huu utaondoa shangamoto ya mrundikano wa wanafunzi katika darasa moja na kuboresha mazingira ya wanafunzi.”
Aliongeza kwamba mradi huo umefikia 85% ya ukamilishaji wake na utaongeza chachu ya wanafunzi kujifunza katika mazingira mazuri na kuchangia matokeo Chanya katika sekta ya elimu hapa nchini.
Mradi umetekelezwa kwa mfumo wa force akaunti unatarajia kupunguza tatizo la madarasa, mrundikano wa wanafunzi wengi kwenye madarasa na kuchochea mazingira rafiki ya kujifunza.
Mwisho
Na Mwandishi wetu-Arusha,
Kampuni ya Barrick yenye ubia na Serikali kupitia kampuni ya Twiga imetunukiwa cheti cha tuzo kwa kudhamini kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kilichomalizika leo jijini Arusha.
Tuzo hiyo ilikabidhiwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati , Dkt Dotto Biteko ambaye alikuwa mgeni rasmi wa kufunga kikao hicho cha siku nne ambapo pia alitoa tuzo kwa taasisi nyingine zilizodhamini mkutano huo.
Akiongea kuhusu udhamini huo kabla ya kukabidhiwa cheti cha tuzo,Meneja wa Barrick nchini Dkt.Melkiory Ngido alisema kampuni imedhamini kikao hicho kama mdau mkubwa wa maendeleo inayoamini kuwa sekta binafsi na Serikali zikishirikiana zinaweza kuleta matokeo Chanya kwenye uchumi wa nchi kama inavyoonyesha kwenye Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025-2050.
Dkt.Ngido pia alisema kuwa Barrick imekuwa ikitekeleza falsafa ya 4R ya Rais Samia kwa vitendo ambayo imeleta ufanisi katika uendeshaji wa shughuli zake nchini kwa kushirikiana na Serikali ambapo imekuwa kioo cha uwekezaji wenye mafanikio nchini.
“Kupitia uwekezaji wetu na uendeshaji wa shughuli zetu kwa ubia na Serikali tumepata mafanikio makubwa baadhi yake yakiwa ni kuwa kinara wa kulipa kodi na tozo mbalimbali ,kutoa gawio nono kwa Serikali,kunufaisha wazabuni wa ndani na kupanua wigo wa ajira kwa watanzania, matumizi ya teknolojia za kisasa na kufanikisha miradi mikubwa ya kijamii hususani katika sekta za elimu,afya,miundombinu kupitia fedha za CSR zinazotolewa na migodi yake ya Bulyanhulu na North Mara”.
Dkt.Ngido pia alisema kuwa kampuni inaendelea kufanya tafiti mbalimbali za kijiolojia kwa lengo la utambuzi wa maeneo mapya ya uchimbaji na imeweza kurefusha maisha ya migodi yake kwa muda mrefu zaidi na kuendelea kunufaisha taifa.
Mwisho
Dar es Salaam, Tanzania -
Bank of Africa
Tanzania joins diplomatic figures, business people, invited dignitaries and
other cultural representatives to celebrate 26th anniversary
of His Majesty King Mohammed VI’s accession to the throne of the Kingdom of
Morocco as of its efforts to foster bilateral ties between Tanzania
and Morocco.
Bank of Africa Tanzania proudly took part in the 26th anniversary celebration, the commemorative event, held in Dar es Salaam recently which among other things brought together distinguished delegates, diplomacy and other representatives to mark this important occasion.
Bank of Africa Tanzania is a subsidiary of the BANK OF AFRICA Group, a pan-African banking network headquartered in Morocco, with operations in 17 African countries and a strategic presence in France.
The Group is majority-owned by BANK OF AFRICA - BMCE, Morocco’s second-largest private bank. The bank reaffirmed its commitment to strengthening bilateral ties between Tanzania and Morocco through financial cooperation and cultural engagement.
The celebration underscored the growing relationship between the two nations, with Bank of Africa Tanzania standing as a bridge between East Africa and North Africa, fostering economic integration and shared prosperity.
Bank of Africa Tanzania remains committed to promoting regional development through strategic partnerships and impactful community engagement, in line with the group’s broader mission across Africa and beyond.
Staa wa zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa, Thierry Henry, ametangazwa rasmi kuwa balozi mpya wa kimataifa wa kampuni ya michezo ya kubashiri mtandaoni, Betway, wakati huu ambapo ligi kuu za barani Ulaya zinarudi dimbani kwa msimu mpya.
Katika
nafasi yake hiyo mpya, Henry anatarajiwa kuwa kiungo muhimu kati ya mashabiki
wa soka na mchezo wenyewe, kupitia maudhui maalum na mitazamo ya kitaalamu
atakayoshiriki kwa ushirikiano na kampuni hiyo.
Henry
alianza soka lake la kulipwa nchini Ufaransa akiwa na AS Monaco, kabla ya
kujiunga na Juventus kwa kipindi kifupi na kisha kutua Arsenal mwaka 1999,
ambako alijizolea umaarufu mkubwa kwa kuwa mfungaji bora wa muda wote wa klabu
hiyo. Aliisaidia Arsenal kutwaa mataji mawili ya Ligi Kuu England (EPL), ikiwemo
msimu wa ‘Invincibles’ mwaka 2003/04, na mataji matatu ya FA Cup.
Katika ngazi ya kimataifa, Henry alikuwa sehemu ya kikosi cha Ufaransa kilichoshinda Kombe la Dunia mwaka 1998, na pia alitwaa taji la Euro 2000. Tangu astaafu soka, amekuwa kocha na mchambuzi maarufu wa soka katika vituo vya runinga mbalimbali.
“Soka
siku zote limekuwa mchezo wa kasi na msisimko, na hayo ndiyo mambo ambayo
Betway huwapatia mashabiki kwa namna ya kipekee,” alisema Henry. “Ninatarajia
kushiriki kwenye kitu kikubwa kinachowaunganisha watu na mchezo wanaoupenda.”
Tangazo
hilo limetolewa wakati ambapo Ligi Kuu England (EPL), La Liga na ligi nyingine
kubwa barani Ulaya zinarejea, kipindi ambacho huwa na ushawishi mkubwa kwa
mashabiki na wadau wa soka duniani kote.
Kwa
mujibu wa taarifa ya kampuni hiyo, uteuzi wa Henry unaonesha dhamira ya
kuendelea kuwekeza kwenye soka la kimataifa. Betway tayari ni mshirika wa klabu
kadhaa maarufu ikiwemo Arsenal, na inaendesha shughuli zake katika masoko
mbalimbali ya Afrika, Ulaya na Amerika.
Mwisho
Utagharimu takribani shilingi Bilioni 4.8 za kitanzania
Na Mwandishi Wetu, Kahama Shinyanga
Mgodi wa
Barrick Buzwagi ambao uko katika mchakato wa kufungwa umefadhili mradi wa ujenzi wa chujio la maji
ya mvua eneo la mwendakulima wilayani
Kahama mkoani Shinyanga unaoghalimu takribani shilingi Bilioni 4.8 kwa ajili ya kuwapatia wananchi wa mji wa
kahama maji safi na salama.
Akiongea wakati wa hafla ya kupokea mwenge
ulioambatana na kuweka jiwe la msingi la ujenzi huo wa mradi wa maji, Meneja wa
Ufungaji wa Mgodi wa Buzwagi ,Zonnastraal Mumbi alisema mgodi katika hatua zake za mwisho za ufungaji
umeamua kufadhili mradi huo ili kuondoa tatizo la upatikanaji wa maji kwenye
Wilaya ya Kahama.
“haya ni matokeo ya ufungaji wa mgodi wa
Buzwagi kwa kuamua kufadhili mradi mkubwa kabisa wa maji ya mvua kwa
kutengeneza miundombinu ya uvunaji , ukusanyaji na usambazaji wa maji ya mvua
kwa ajili ya matumizi wa wananchi wa mji ya Kahama,” alisema Mumbi.
Aliongeza kwamba moja ya dhamira ya
kampuni ya Barrick inayoendeha shughuli zake nchini kwa ubia na Serikali
kupitia kampuni ya Twiga Minerals ni kuunga mkono jitihada za Serikali
kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama.
“Mgodi wa Buzwagi umefadhili mradi huu wa
maji ya mvua kwa 62% kwa ajili ya kuhakikisha kwamba miundombinu ya kisasa na
bora inajengwa kwenye mradi huu kama sehemu za kuleta matokeo Chanya kwa
wananchi wa mji wa kahama,” alisisitiza
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Usambazaji
Maji na Usimamizi wa Mazingira, ,
Mamlaka ya Maji Safi wa Mazingira Kahama
(KUWASA)Mhandisi , Magige Marwa , alitoa pongezi kwa kampuni ya Barrick nchini kwa kufadhili mradi huo mkubwa ambao
ukikamilika utaondoa changamoto ya upatikanaji maji safi na salama wilayani
Kahama,
Aliongeza kwamba mradi wa ujenzi wa chujio
la maji mwendakulima unatazamiwa kuhudumia zaidi ya 66% ya wakazi waishio
manispaa ya Kahama na una uwezo wa kuzalisha lita milioni 10 kwa siku.
“Mradi huu unatarajiwa kukamilika Desemba
mwaka huu na mpaka sasa 78% ya mradi mzima umeshakamilika kutokana na kasi ya
ujenzi wa mradi huu mkubwa kwenye mji huu wa kahama,” alisisitiza
Mhandisi Marwa alifafanua kwamba mradi huo
wa chujio la maji ya mvua 62% imefadhiliwa na mgodi wa Barrick- Buzwagi na 38%
ni KUWASA kupitia Wizara ya Maji na Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa
Tanzania.
Kwa upande wake , kiongozi wa mbio za
mwenge , Ismail Ali Ussi alisema wizara ya maji inaendelea kufanya vizuri na
kutekeleza kwa vitendo maono ya Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya
kumtua mama ndoo kichwani kwa kupeleka huduma ya maji mijini na vijijini.
“Nachukua fursa hii kuwapongeza wataalamu
wote wa wizara na mamlaka za maji hapa kahama kwa kufanya kazi usiku na mchana
katika kuhakikisha watanzania wanapata maji safi na salama,” amesema.
Kwa upande wake , Mkuu wa Wilaya ya
Kahama, Frank Nkinda alisisitiza kwamba umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii na
kuendelea na ari hiyo ya kutekeleza miradi ya huduma za wananchi kwa viwango
vya juu ili kukidhi mahitaji ya wananchi.
Mwisho
Washindi 20 wa kwanza katika kampeni ya ‘Miamala ni Fursa’ wazawadiwa
Bank of Africa -Tanzania imetoa zawadi kwa washindi wake 20 wa kwanza wa wiki kupitia kampeni ya huduma za kibenki kwa njia ya kidigitali iitwayo “MIAMALA NI FURSA”, ambapo kila mmoja amepokea zawadi ya Sh50,000 kwa kutumia huduma za kibenki kwa njia ya simu za mkononi kupata huduma za huduma za kifedha.
Akizungumza kuhusu maendeleo ya kampeni hiyo iliyozinduliwa Juni 4, 2025, Afisa Mkuu wa Huduma za Kidigitali wa Bank of Africa-Tanzania, Bw Lameck Mushi, alisema kuwa mwezi mmoja tangu kuanza kwa kampeni hiyo ya miezi mitatu, imepokelewa vyema na umma wa Watanzania.
Bw Mushi alieleza kuwa kampeni hiyo inalenga kuhamasisha matumizi ya jukwaa la benki kupitia simu kwa kuwazawadia wateja wanaofanya miamala ya kila siku. Juhudi hizi ni sehemu ya dhamira ya benki yao kuendeleza matumizi ya huduma za benki kidigitali na kuendeleza ujumuishwaji wa kifedha nchini Tanzania.
“Tunafurahia mwitikio mkubwa tulioupokea hadi sasa. MIAMALA NI FURSA tayari imefanya huduma za kibenki kupitia simu kuwa za kuvutia na muhimu katika maisha ya kila siku ya wateja wetu,” alisema Bw Mushi.
Akiendelea, alisema ukweli kwamba “Wateja wanashinda zawadi za fedha kwa kufanya miamala ya kulipa bili au kutuma fedha unaonyesha kuwa vitendo vidogo, lakini vya mara kwa mara vina mchango mkubwa. Zaidi ya hapo, tumeongeza unafuu kwa wateja wetu kwa kupunguza ada za miamala ya Bank-to-Wallet kwa zaidi ya asilimia 50."
Kila wiki, wateja watano watakaokamilisha miamala mitatu ya Bank-to-Wallet (B2W) na muamala mmoja wa ziada (malipo ya bili, ununuzi wa muda wa maongezi au umeme) kupitia B-Mobile watakuwa na nafasi ya kushinda.
Mwisho wa kampeni hii, ambayo itaendelea hadi Septemba 2025, mshindi mkuu atajinyakulia zawadi ya pesa taslimu Sh5 milioni.
Afisa Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa RejaReja Asupya Nalingigwa, alisisitiza: “Lengo letu ni kufanya huduma za kibenki ziweze kufikiwa kwa urahisi, ziwe na manufaa na ziwaguse wateja wetu kwa ukaribu zaidi. Iwe uko mjini au kijijini, mradi una B-Mobile, unaweza kushiriki na kushinda.”
Ili kuhakikisha ushirikishwaji wa wote, Bank of Africa-Tanzania imehamasisha timu zake za matawi kote nchini kusaidia kuwaunganisha wateja wapya na kutoa mafunzo ya kutumia huduma hizo za kidigitali. Timu maalumu ya msaada wa kiufundi pia ipo tayari kusaidia kutatua changamoto zozote za upatikanaji na kuhakikisha uzoefu mzuri kwa watumiaji wote.
Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano Nandi Mwiyombella, aliongeza: “Kampeni hii si kuhusu zawadi pekee, bali ni kuhusu kuwapa nguvu wananchi. Kwa kuhamasisha matumizi ya huduma za kidigitali kwa njia shirikishi na rahisi, tunawasaidia Watanzania wengi zaidi kushiriki katika mfumo rasmi wa kifedha.”
Kwa zawadi zaidi za fedha na washindi wapya kutangazwa kila wiki, Bank of Africa -Tanzania inawaalika wateja wake wote kufanya miamala, kushinda, na kufurahia huduma za kibenki kwa urahisi kupitia simu zao.
Kuhusu BOA Bank (T) Limited
BOA-Tanzania ni benki ya biashara binafsi inayotoa huduma kwa wateja wa kampuni kubwa, wateja wa kati (SME) na wateja wa rejareja nchini Tanzania. Ilianza shughuli zake Juni 2007 baada ya kununua Eurafrican Bank iliyokuwa ikifanya kazi nchini tangu Septemba 1995.
Benki hii ni sehemu ya kundi la Benki ya Afrika, ambalo lilianza shughuli zake mwaka 1982 nchini Mali.
Kundi hili linafanya kazi katika nchi 19 za Afrika, ikiwa ni pamoja na Afrika Magharibi, Afrika Mashariki, Afrika ya Kati, pamoja na ofisi za uwakilishi Paris (Ufaransa), Hispania, London (Uingereza) na China. Tangu mwaka 2010, Benki ya Afrika imekuwa chini ya umiliki mkubwa wa BMCE Bank, benki ya tatu kwa ukubwa nchini Morocco, inayotoa huduma katika nchi 31 na mabara 4.
Kwa sasa, BOA-Tanzania ina matawi 17 ya rejareja, yakiwemo 8 Dar es Salaam na 9 katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Zanzibar na miji mingine mikubwa.
Mawasiliano ya Vyombo vya Habari:
Tovuti: www.boatanzania.com
Beatrice E. Mirigo – Maendeleo ya Bidhaa & Mawasiliano
Barua Pepe: beatrice.mirigo@boatanzania.
Simu: +255 699 000 260
Mwisho………..