Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete amemteua Engineer Felchesmi Mramba kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
Taarifa iliyotolewa Ikulu,
Dar es Salaam leo, Jumatatu, Desemba 2, 2013, na Kaimu Katibu Mkuu
Kiongozi, Dkt. Florens Turuka inasema kuwa uteuzi huo umeanza leo hii.
Kabla ya uteuzi wake, Eng. Mramba alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo la TANESCO.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
2 Desemba, 2013
Felichesmi Mramba ateuliwa na Rais kuwa Mkurugenzi Mtendaji TANESCO
03Dec2013
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.