April 7, 202505:34:15 AM

MADEREVA wa bajaji mkoani Singida,wameshauriwa kujenga utamaduni wa kutii bila shurti sheria za usalama barabarani,ili pamoja na mambo mengine,kuondoa uwezekano wa kutokea kwa ajali zinazosababisha vifo na uharibifu mkubwa wa mali.
 
Aidha, wametakiwa kutii bila shurti kanuni na taratibu zilizowekwa na SUMARTA,ili kupunguza uwezekano wa kutokea kwa migomo na kufunga barabara.
Usafiri wa Bajaji
 
Wito huo umetolewa juzi na meja Stan wa kitengo cha usalama barabarani mkoani Singida,wakati akizungumza na madereva wa bajaji wa kituo cha soko kuu mjini hapa ambao walifunga barabara ya mtaa wa Mukhandi kutumika.
 
Meja Stan aliwataka kuheshimu maamuzi ya SUMATRA kwa kuwapa vituo vya kupakia abiria,ili kuepuka kutokea kwa migongano baina yao na bodaboda na hata hiece.
 
“Kama wewe SUMATRA imekupangia kituo chako kuwa ni cha stand ya mabasi cha zamani,sheri,ukipakia abiria anakuja hapa soko kuu,sheria inakutaka ukimshusha tu,uondoke hapo mara moja kurudi kwenye kituo chako”,alisema.
 
Meja Stan alisema abiria huyo akimaliza shughuli zake soko kuu,atapanda bajaji au usafiri mwingine kwenda anakotaka.
 
Akifafanua zaidi,alisema kuwa sheria hairuhusu dereva wa bajaji ambaye soko kuu sio kituo chake asubiri abiria pale,ili amalize shughuli zake halafu ampeleke sehemu nyingine anakokwenda.Wajibu wake ni kumshusha na yeye kurudi kwenye kituo chake.
 
Wakati huo huo,meja Stan amewataka wajenge utamaduni wa kutumia viongozi wao kuwasiliana na uongozi wa halmashauri ya manispaa ya Singida,ili kujadiliana pamoja kutatua kero mbalimbali na kuzipatia ufumbuzi wa kudumu,ikiwemo ya ufinyu wa maegesho.
 
MWISHO.
Labels:

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

Post a Comment

    Author Name

    Contact Form

    Name

    Email *

    Message *

    Powered by Blogger.