BOT yazungumzia uvumi kuhusu 'utajiri' katika sarafu ya sh 500/=
Benki ya Tanzania (BOT) imewataadharisha wananchi kwamba sarafu ya
shilingi 500 haina madini ya aina yoyote na wala haiuzwi kama
inavyodaiwa baadhi ya watu.
Kauli hiyo imetolewa leo na Meneja Uhusiano wa benki hiyo, Zalia Mbeo wakati akitoa ufafanuzi kwa Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, HAB Mkwizu ambaye aliuliza kwamba kuna taarifa kuhusu sarafu hiyo kuuzwa mitaani.
Kaimu Katibu Mkuu huyo ambaye alifungua maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mhe. Celina Kombani.
“Watanzania wanatapeliwa sarafu hii haina thamani yoyote ni uzushi,” alisema Zalia.
Aliongeza kusema kuwa wananchi wadanganywa na watu kuwa sarafu hiyo ikiyeyushwa ina madini ambayo yanaweza kuwapatia fedha nyingi wakati si kweli.
Post a Comment